Subscribe Us

WALIMU WA SHULE BINAFSI NA SERIKALI WAMEUNGANA KWA PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO MASHULENI

Na. Kadala Komba Dodoma
Mwenyekiti wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Ester Manyanda Akizungumza na Waandishi wa Habari lengo la kukutana pamoja Walimu wa Shule Binafsi
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma,Josephine Mwaipopo akizungumza Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Wamiliki wa Shule wakipokea vyeti kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo
Picha ya Pamoja kwa washiriki na Wadau wadhamini wakiwa na Mgeni Rasmi
WALIMU wa Shule binafsi za Awali na Msingi toka Mikoa mbalimbali Nchini wakiwemo wamiliki wa Shule hizo wamekutana Jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza malezi na makuzi ya watoto ili kuwalinda na vitendo viovu dhidi ya ukatili na maadui kwa mustakabali wa maisha yao ya Sasa na baadae. Hatua hiyo imekuja kufuatia kuongezeka kwa wimbi la vitendo vya ukatili katika Jamii dhidi ya Watoto ambavyo vinazidi kuongezeka kila siku. Mwenyekiti wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Ester Manyanda Akizungumza kwa niaba ya Walimu na Wamiliki wa shule binafsi katika Tamasha hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza Jijini Dodoma alisema tunaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana kupambambana na vitendo vya ukatili vinavyotokea kwenye Jamii inayotuzunguka kwakufanya hivyo ni mwanzo mzuri ili kuwa na Taifa lenye malezi bora. Aidha Mkuu wa shule ya Kimataifa ya Almes, Reuben Kiloy ametumia nafasi hiyo kuwaomba Wadau mbalimbali wakiwemo Elimu na Jamii kuwaunga mkono. Kiloy alisema kuwa malengo ya kukutana ni kuwaleta pamoja na kuwaunganisha walimu wa shule binafsi ili kuwapa walimu fursa ya kujifunza malezi na makuzi ya watoto ili kuwalea na kuwafundisha vema ikiwa ni pamoja na kuwalinda watoto dhidi ya maadui na vitendo viovu n hatarishi kwa maendeleo ya watoto. "Lengo lingine la kukutanisha walimu hapa ni kutoa mchango madhubuti katika kuhamasisha jamii kuelimisha watoto wetu katika mazingira yasiyokinzana na utamaduni,mila na desturi za kitanzania,"alisema. Kwaupande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma,Josephine Mwaipopo akizungumza Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,alisema kuwa kama Serikali wamekuwa wakifanya jitihada kubwa katika kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo kutoa Elimu kwa Jamii kwa vitendo . "Serikali imekua ikitoa miongozo mbalimbali kwajili ya uanzishaji shule za watoto kuanzia miaka 0 hivyo miongozo hiyo ikifuatwa watoto watalindwa na watakua katika makuzi sahihi,"alisema. Alisema kuwa masuala ya ukatili wa kijinsia na ukatili wa watoto umekua mkubwa kwasasa hivyo ni vizuri kutoa elimu zaidi kwa jamii na wazazi ilikukomesha vitendo hivyo. "Mamlaka za Serikali za mtaa zimewekewa sheria za kuhakikisha watoto wanalindwa katika maeneo yao,"alisema. Pamoja na hayo afisa ustawi huyo aliwataka watanzania kujenga tabia ya kuasili watoto kwani watoto waliopoteza wazazi ni wengi na wanakosa malezi sahihi kwakukosa walezi. Aidha Katibu wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Rehema Andrew Amesema sisi kama walimu wa shule binafis tutaendelea kutoa mchango madhubuti katika jamii kuhamasisha watoto wetu wanakuwa katika mazingira yasiyokinzana na utamaduni mila na desturi za kitanzania. Mwisho

0 Comments:

Post a Comment