Na.Kadala Komba
Dodoma
MAMLAKA
ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema majibu ya vipimo vya
vinasaba (DNA) hutolewa ndani ya siku 21 huku uchunguzi hufanyika kwenye
kuangalia uhalali wa wazazi na masuala ya jinai ikiwamo ubakaji na
ulawiti.
Pia, katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga sh.biliom 22 kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa mitambo na
vifaa vya kisasa vya kimabaara ili kuboresha huduma
Akizungumza
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2021/22 na vipaumbele vya bajeti ya 2022/23, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Fidelice Mafumiko, alisema gharama ya kipimo hicho ambayo imedumu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10 ni sh.100,000 kutokana na serikali kubeba mzigo wa gharama zingine.
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2021/22 na vipaumbele vya bajeti ya 2022/23, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Fidelice Mafumiko, alisema gharama ya kipimo hicho ambayo imedumu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10 ni sh.100,000 kutokana na serikali kubeba mzigo wa gharama zingine.
Alisema
kwa uhalisia kipimo hicho gharama yake ni sh.700,000 hadi 800,000
kutokana na ughari wa kemikali lakini kwa muda mrefu serikali imebeba
gharama hizo ili wananchi wapate huduma.
“Zile
kemikali zinazosaidia kufanyika kipimo ni za ghari na kuna kemikali
moja huwa tunanunua kila baada ya miezi mitatu ni Dola za Marekani 6,000
lakini ikitokea suala la janga huisha kabla ya muda huo,”alisema.
Alisema
kama mtu anataka kupima vinasaba vya baba, mama na mtoto ni Sh.300,000
na wamepeleka mapendekezo serikalini iongezeke kidogo ili kusaidia
kuhudumia watu bila kuathiri uendeshaji wa mitambo na gharama za
kemikali.
“Sehemu kubwa
ya DNA inatumika kwenye masuala ya jinai kama masuala ya ulawiti,
ubakaji, au hata wizi, kwa hiyo sio kwamba DNA inatumika kuonesha wazazi
halisi lakini inasaidia kwenye masuala hayo ya jinai,”alisema.
Kuhusu
uchunguzi wa jinsi tata, alisema mamlaka hiyo inapofanya uchunguzi huo
huwasilisha matokeo kwa madaktari bigwa walioomba ufanyike.
“Kama
inatokea wasiwasi mtu anasema haelewi jinsi yake kama ni ya kike au ya
kiume sisi tuna uwezo huo wa kuona hii ni ya kiume au ya kike mara moja,
kwa hiyo tunafanya uchunguzi wenye weledi unaotawaliwa na kutunza siri
kwa anayefanyiwa uchunguzi na kupeleka majibu kwa aliyeomba kifanyike
kipimo,”alisema.
Awali,
alisema katika Mwaka wa Fedha 2021/22 vibali vya uingizaji wa kemikali
viliongezeka kufikia 63,588 ikilinganishwa na vibali 49,234
vilivyotolewa mwaka wa fedha 2020/21 ikiwa ni ongezeko la vibali 14,354.
“Mbali
na utoaji vibali vya kemikali, Mamlaka katika kipindi cha Mwaka wa
Fedha 2021/22 imefanikiwa kusajili wadau wanaojihusisha na shughuli za
kemikali 1087 ikilinganisha na wadau 1057 waliosajiliwa kwa mwaka fedha
2020/21 ikiwa ni ongezeko la wadau 30,”alisema.
Kwa
upande wake, Mkuu wa kitengo cha huduma na sheria wa mamlaka hiyo,
Daniel Ndiyo, alisema mahakama zimekuwa zikitumia ushahidi wa vinasaba
na kutoa wito kwa jamii inapotokea mtu amefanyiwa ubakaji au ulawiti
asikimbilie kunawa ili kurahisisha upimaji wa kipimo hicho.
“Huwa
zinachukuliwa mbegu za kiume na kuletwa kwa Mkemia ili zipimwe, na kwa
wengine ambao huwa wanasababisha ujauzito kwa hiyo mtoto akizaliwa huwa
tunaletewa sampuli kwa ajili ya kumpima mama baba na mtoto na kama
matokeo hutumika kama ushahidi,”alisema.
Alisema kipimo hicho hutumika kwenye kesi nyingi za mirathi, jinai na ndoa.
Mwisho.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Fidelice Mafumiko,akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mamlaka
hiyo.
0 Comments:
Post a Comment