Subscribe Us

*FURSA KWA WANAWAKE KUKOPA DOWOSA RIBA ASILIMIA 1 KWA MWEZI*


Na. Kadala Komba Dodoma

Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Amewataka wanawake kujiunga na DODOMA WOMEN SACCOS (DOWOSA) kwa maendeleo ya uchumi wetu Dowosa ni Saccos ya kujiunga ninauhakika kwa Dowosa ni chombo cha kuchochea kukuwa kwa uchumi katika jamii na Taifa wanachama na viongozi zingatieni mambo muhimu hili chama kiwe endelevu Alisema .
"Hivyo toweni Elimu ya  kutosha kwa wanawake waweze kujiwekea hakiba ya kila mwezi na ununuzi wa hisa kwani uwekezaji mdogo wa hisa unaasili mtaji wa Saccos.

Hayo yamejiri wakati Mkutano Mkuu wa pili wa Dodoma Women Saccos Limited mwishoni mwa wiki katika  Jengo la Hazina Ukumbi wa Kambarage -Wizara ya Fedha Dodoma.

Mhe. Mbonipaye Mpango alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya hawamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu kwa kuweka mazingira rafiki ya uwazishwaji na uendeshaji wa Saccos ambayo  imewezesha Dowosa kuanzishwa kama Saccos nyingine Dowosa itaenda kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika ngazi ya familia ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla kutokana na uraisi wa kupata huduma za fedha kwa gharama nafuu asilimia 1 nisawa na bure unakopa milioni Ishirini (20 )unalipa laki mbili  (2 ) kwa mwezi ni fedha ndogo sana imani yangu wanawake wengi watahamasika kujiunga na Dowosa.


Naye Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule  Amempongeza Amempongeza Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa kipaombele kwenye mambo ya wanawake sio wanawake wa Dodoma tu ila nchi nzima umekuwa na upendo na wanawake nimeona Sehemu nyingi unazokaribishwa unakuwa nao bega kwa bega tunakushukuru sana ili linaonesha kabisa unafurahia maendeleo ya wanawake.

Kwaupende wake Kitorina Kipa Mwenyekiti Dodoma Women Saccos alisema  malengo ya kuanzisha Saccos hii ni kuwakwamua wanawake kiuchumi kutokana na wanawake wengi wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutokana na kukopa mikopo kwenye baadhi ya taasisi za fedha zenye masharti magumu na Riba kubwa.

Alisema wanawake wengi hasa wajasiriamali wadogo wamekuwa wakinyanyasika sana wengine kuuziwa vitu vyao vya ndani na wengine kuvunjika kwa ndoa zao na wengine kupoteza kupoteza maisha kutokana na kushindwa kulipa mikopo hiyo maalufu kausha Damu au mikopo umiza, hivyo Saccos hii imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wanawake wajasilimali wa Dodoma kupata mikopo kwa masharti nafuu na kwa riba ndogo ya Asilimia moja (1) tu kwa mwezi alisema .


MWISHO 



Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa pili wa Dodoma Women Saccos Limited
 


Kulia Kitorina Kipa Mwenyekiti Dodoma Women Saccos katikati ni Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule Nyuma ni Bodi ya Bodi ya Dodoma Women Saccos Limited

Kitorina Kipa Mwenyekiti Dodoma Women
Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi
 

Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule Akimkabidhi Zawadi Mgeni Rasmi Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania    



Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule Akitazama Zaidi aliyokabidhiwa na Dodoma Women Saccos Limited



Wanachama wa Dodoma Women Saccos Limited kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka



Mwenyekiti wa muda wa mkutano  AZiza Mumba

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dododoma Mhe.Fatma Toufiq Akipokea cheti cha Mkopaji Bora

Bodi ya Dodoma Women Saccos Limited

0 Comments:

Post a Comment