Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Umoja wa makampuni binafsi ya ulinzi Tanzania (UKUTA) wameiomba serikali kufungia makampuni bubu kwani wanafungua kampuni hizo bila kufuata sheria jambo ambalo ni sawasawa na kuhujumu uchumi kwa kushindwa kuwa wazalendo.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndg.Abel Dendwa wakati wa mkutano Mkuu wa tatu wa taasisi ya makampuni binafsi ya ulinzi Tanzania(UKUTA) uliofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel jijini hapo.
Aidha ameongeza kuwa wanatoa mwezi mmoja kwa makampuni hayo wawe wamejitathimini kuweza kujiunga na na umoja huo ili waweze kutambulika na sio kufanya kazi kinyume na matakwa ya umoja huo.
"Nitumie fursa hii kuiomba serikali kilio chetu kwa wakurugenzi tuwe na sheria inayo tuongoza kwa maana sheria itatuamulia huyo mwenye kampuni bubu tunaweza kukabiliana nae vipi kufungiwa ili wafuate sheria kwani tunaendelea kuhubiri umoja tunakataa kutengana" Amesisitiza Katibu Abel
Naye John Joseph Muwakilishi wa mkurugenzi Mkuu Takukuru amesema wao kama taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa ni jukumu lao kuelimisha jamii kwani Rushwa ni dhambi na madhara ya Rushwa ni makubwa.
"Niwaombe tujikite katika kusimamia sheria na taratibu,sisi sote ni serikali,lakini kama taasisi kuelimisha umma ni jukumu letu,msingi na wajibu wetu ni kuwafuata wananchi walipo kuwapa elimu ya Rushwa na tumeanzisha klabu za kupinga Rushwa shule za msingi,sekondari na vyuo vikuu hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya madhara ya Rushwa na imani yangu ni kwamba kama kila mtu anatimiza wajibu wake basi ni rahisi kufuata sheria na taratibu zake bila kushurutishwa" Ameongeza Joseph
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo (UKUTA) Amani Mbijima ambaye pia ni Mkurugenzi wa Patmercy Security Co LTD amesema makampuni ya ulinzi binafsi yamekuwa wakikumbana na Changamoto hasa kwenye utaratibu wa ufatiliaji wa malipo kwenye tasisi kwani wamekuwa wakilazimila kupeleka risti kabla ya malipo hali aliyoisema ni shida kwao.
Amesema kwa Upande wao wanavyolazimishwa kutoa risti ya EFDs kabla ya malipo imekuwa ni shida kwao kwani wanavyotoa risti wanaonekana wamelipwa na wao kutakiwa kulipa kodi kulingana na sheria ya mlipa kodi.
Changamoto nyingine ni pamoja malipo wanayolipwa yapo chini ambapo kima cha chini wanachotakiwa kulipwa Shilingi 148000 tofauti na viwango wanavyotakiwa kulipwa na hiyo yote ni kutokana na kukithili kwa makampuni bubu.
" Kumezuka makampuni bubu hali inayopelekea kutukwisha sisi makampuni ya ulinzi binafsi tuliosajaliwa na kutambuliwa kwani makampuni hayo bubu ndio yamevunja bei na kutupelekea na sisi kukosa soko wamekuwa wakifanya kazi kiholela bila makubalinao na hata wakikubalina wanakubaliana kwa bei ya chini na kusababaisha na sisi kushindwa kuwalipa walinzi, " Amesema
Na kuongeza" Sasa tuna kwenda kushirikina na mamlaka husika ili makampuni hayo kuondolewa Mara Moja katika jamii kwani ndio yamekuwa yakileta Shinda na kupeleka kuharibu sifa yetu, "Amesema
Home »
» TUNAIOMBA SERIKALI ITUSAIDIE KUFUNGIA MAKAMPUNI BUBU(UKUTA).
0 Comments:
Post a Comment