Home »
» FAIDA FUND YAPATA MAFANIKIO YA MAUZO HAWAMU YA KWANZA
FAIDA FUND YAPATA MAFANIKIO YA MAUZO HAWAMU YA KWANZA
Na. Johndickson Gaudin Dodoma
Mfuko wa Uwekezaji wa pamoja FAIDA FUND umefanikiwa kuwa Mfuko wa kwanza wa aina yake kupata mafanikio makubwa katika kipindi cha mauzo ya awali ikilinganishwa na lengo lililowekwa la kuanzishwa kwake.
Hayo yamebainishwa leo Februari 9,2023, Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investiments (WHI), Dkt. Fred Msemwa mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Watumishi Housing Investiments katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Msemwa amesema Mfuko huo umeyalenga makundi yote ya kijamii na lengo lake likiwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji wa pamoja wakiwemo watoto, wakulima, wavuvi, watumishi wa umma, wafanyakazi, makampuni na taasisi.“Faida Fund imenzishwa chini ya sheria ya masoko ya Mitaji na dhamana sura 79 ya sheria za Tanzania, Mfuko huu unasimamiwa na mamlaka ya masoko na dhamana (Capital Market and Securities Authority - CMSA) ambaye ndiye mdhibiti wa Sekta,”
amesema.
Amesema mfuko huo umekuja sokoni kuongeza nguvu na kuchochea tabia ya kuwekeza ukiwa na lengo kuwawezesha watanzania kiuchumi kwa kukuza mitaji yao.“Mwekezaji anaweza kufungua akaunti ya uwekezaji kwa kutumia menyu kuu ya serikali ya *152*00# au kwa kutumia WekezaWHI App ambayo inapitikana kwenye simu janja au kwa kutumia mfumo wa FAS (Fund Administration System) ambao umebuniwa na Mamlaka ya serikali Mtandao,”amesema.Aidha ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake WHI imejenga jumla ya nyumba 983 katika maeneo mbalimbali ambazo zimeuzwa kwa watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.Vilevile amesema Watumishi Housing Investiments imeendelea kuwauzia nyumba kwa mkopo nafuu watumishi wa umma ambao walikuwa hawawezi kununua nyumba kwa mkopo kutoka taasisi zingine katika soko.“Hii imewanufaisha watumishi haswa kanda ya kati na chini wakiwemo wauguzi na watumishi wa manispaa,
”amesema.Watumishi Housing Investment (WHI) ni taasisi ya umma iliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), iliyoanzishwa mwaka 2014 kupitia mifuko ya Pensheni kwa watumishi wa umma (PSSSF), Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF), shirika la Nyumba la Tatumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), iliyoanzishwa mwaka 2014 kupitia mifuko ya Pensheni kwa watumishi wa umma (PSSSF), Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF), shirika la Nyumba la Taifa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investiments (WHI), Dkt. Fred Msemwa mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Watumishi Housing Investiments
0 Comments:
Post a Comment