Home »
» UDAILI WA WANAFUNZI (DMI) KUONGEZEKA IFIKAPO 2025_2026 HADI WANAFUNZI ELFU
UDAILI WA WANAFUNZI (DMI) KUONGEZEKA IFIKAPO 2025_2026 HADI WANAFUNZI ELFU
Na Johndickson Gaudin Dodoma
Chuo cha Baharia Dar es salaam (DMI) kinatarajia kudaili wanafunzi takribani Elfu 20 Hadi 23 ifikapo mwaka 2025_2026 hii ikiwa ni juhudi za chuo hicho katika kuhakikisha kina zalisha wanafunzi wenye weledi katika sekta ya Ubaharia.
Hayo yamebainishwa na kaimu Mkuu Wa Chuo hicho Dkt. Tumain Shaban Kwenye Mkutano na waandishi wa Habari hii Leo February 09 2023 jijini Dodoma ambalo amesema jitihada hizo nikwaajili ya kuhakikisha wanazalisha wanafunzi wengi na kuacha kuchukua mabaharia kutoka nje ya nchi.
Dkt.Shaban amesema kupitia serikali ya awamu ya sita chuo hicho kimeweza kupata fedha takribani shilingi bilion 6.5 kwaajili kununulia vifaa vya kufundishia ambavyo ni mashine pamoja na mitambo Mbalimbali"Serikali imefungua zaidi milango ya kupata mikopo Kwa wanafunzi wetu kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu Jambo ambalo limeongeza idadi ya wanafunzi.
"Kwa mwaka 2022_2023 wanafunzi 1705 wamepata mikopo ukilinganisha na mwaka 2021_2022 ambapo wanafunzi 850 ndio walipata mikopo "
,amesema Dkt Shaban.Aidha amesema kupitia serikali ya awamu ya sita kimeweza kupata maeneo Mbalimbali ya kujenga matawi ya chuo hicho ikiwa nipamoja na mkoa wa Lindi na Mwanza matawi ambayo yatawezesha kufikisha elimu ya Ubaharia katibu na wananchDkt Shaban ameongeza kuwa chuo hicho kinafanya utafiti na kutoa ushauri elekezi Kwa serikali na taasisi binafsi,pia chuo hicho kinafanya usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri vya majini."Shughuli zinazofanywa ni usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri majini Tathimini ya maji katika vyanzo vya maji baadhi ya vyombo hivyo nipamoja na MV Kigamboni, MV . SAR, M.V MWONGOZO,"amesema Dkt Shaban
kaimu Mkuu Wa Chuo hicho Dkt. Tumain Shaban Kwenye Mkutano na waandishi wa Habari hii Leo February 09 2023 jijini Dodoma
Related Posts:
MCHUNGAJI CHARLES PROSPERITY KUHESABIWA HAKUNA MAHUSIANO NA MAMBO YA GIZA KISHETANIWA YA USHETANINa. Kadala Komba Dodoma MCHUNGAJI kiongozi Charles A. Prosperity wa kanisa la The Covenant Place lililopo kisasa Relini Dodoma amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ya watu na makazi ambalo linatal… Read More
MATUKIO KATIKA PICHA ;BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WANASIASA WALIOHUDHURIA JUBILEI YA MIAKA 50 MATUKIO KATIKA PICHA: Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wanasiasa waliohudhuria adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya miaka 50 ya Jimbo Katoliki Singida pamoja na Miaka 25 ya Upadre wa Mhashamu Edward Elais Mapunda Askofu … Read More
MBUNGE DITOPILE TUNAKUSHUKURU RAIS KWA KUTUPATIA WAKULIMA MBOLEA YA RUZUKU Na. Kadala Komba Dodoma MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkulima, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya katika sekta ya Kilimo ambapo kwa mara ya kwanza b… Read More
ASKOFU DKT. MWAKIPESILE: MUWE TAYARI KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU NA. MWANDISHI WETU. Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dkt. Brown Abel Mwakipesile ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 … Read More
WAKAZI WA GAIRO MKOANI MOROGORO WAVAMIA LORI LA MAFUTA #MOROGORO: Wakazi wa Gairo mkoani Morogoro wamevamia tena lori la mafuta lililopinduka ili kujipatia mafuta. - Majeraha ya ajali kama hiyo iliyotokea miaka miwili iliyopita nakuuwa zaidi ya watu 100 bado hayajapona na idadi … Read More
0 Comments:
Post a Comment