Home »
» PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI IMEZINDULIWA KATA YA MPAMANTWA WILAYA YA BAHI
PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI IMEZINDULIWA KATA YA MPAMANTWA WILAYA YA BAHI
Na. Kadala Komba Bahi
Mkuu wa Takukuru Halmashauri Wilaya ya Bahi Erick Kilawe Amesema hii Programu ya TAKUKURU RAFIKI imeanzishwa Maalumu hili kutoa fursa kwa kila Mtanzania kushirikiana na Serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo ni kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Hayo yamejili Jijini Dodoma Wilaya ya Bahi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Takukuru Rafiki ikizinduliwa kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Wilaya na kata amesema Programu hii inaakisi maana ya rafiki kwa kubeba dhana ya kuwa karibu na ushirikiano wa dhati na karibu na kila mwananchina wadau kwa itatekelezwa kwa kuwa na vikao katika ngazi ya kata kwa lengo la kutambua kero zilizopo kwenye utoaji au upokeaji wa huduma kama za Afya au Elimu pamoja na mchakato wa kutekeleza miradi ya maendeleo ujenzi wa miundombinu ya maji.
Kwaupande wake Mchunguzi mkuu Takukuru Emmanuel Masawe Ametoa wito kwa Wananchi na wadau kushirikiana kuzuia vitendo vya Rushwa katika utoaji wa huduma kwa umma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Programu hii ya "TAKUKURU RAFIKI" Usikae pembeni tushirikiane katika ili kwa pamoja tunaijenge Tanzania.
Aidha Mhe. Diwani kata ya mpamatwa ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuwapatia semina namna ambavyo taasisi hiyo inanyo fanaya kazi kwa karibu na wananchi katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuu wa Takukuru Halmashauri Wilaya ya Bahi Erick Kilawe
Mhe. Diwani kata ya mpamatwa
MATUKIO MBALIMBALI KWENYE PICHA YA UZINDUZI WA PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI
0 Comments:
Post a Comment