Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

TANROADS YATUMIA SHILINGI TRILIONI 1.37 KUKAMILISHA MIRADI 14 KWA KIPINDI CHA SERIKALI AWAMU YA SITA.

Na Moreen Rojas, Dodoma Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema imefanikiwa kukamilisha jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 katika kipindi cha awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wenye gharama ya shilingi Trilioni 1.37. Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na vipaumbele vya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23. Mha.Mativila ametaja miradi hiyo ilivyokamilika kuwa ni miradi ya barabara ya Kidahwe_Kasulu (km 63) Mkoa Kigoma,Nyakanazi_Kibondo kabingo (km50) Mkoa Kigoma,Mbinga _Mbamba Bay (km66) Ruvuma,Njombe _Moronga section (km 53.9),Njombe Moronga_Makete section (km 53.30) Njombe Makutano _Natta(Sanzate)Section (km50) _Mkoa wa Mara Waso_Sale Jct section (km49)Arusha. Pia ametaja na Miradi ya madaraja makubwa iliyokamilika kuwa ni Tanzanite Bridge Dar_es_Salaam(km 1.03),Ruhuhu bridge along Kitai_Lituhi road in Ruvuma Region (m 98), Magara Bridge in Manyara region (m 84),Mara Bridge in Mara Region (m 940), Msingi Bridge Singida (m 100), Sibiti Bridge Singida (m 82), na Wami Bridge Pwani m 514. Aidha Mativila amesema kuwa jumla ya miradi 44 ya barabara yenye urefu wa kilometa 1,523 yenye gharama ya shilingi Trilioni 3.8 ipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi nchi nzima. "Miradi hii inahusisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani na inayogharamiwa kupitia washirika mbalimbali wa maendeleo" Amesisitiza Mativila. Vilevile Mha.Mativila amesema kuwa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha msalato unaojumuisha ujenzi wa wa njia ya kurukia ndege na majengo ya abiria unaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika(AFDB) kwa gharama ya shilingi Bilioni 360. Pia Mha.Mativila amesema kuwa miradi ya barabara 62 iko katika hatua mbalimbali za manunuzi kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami. "Barabara hizi zinajumuisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani pamoja na fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo" Amesema Mativila. Ametaja miradi mingine kuwa ni Miradi ya EPC + F ambayo wizara ya ujenzi kupitia TANROADS imeanza utekelezaji wa miradi ya EPC + F yenye urefu wa kilometa 2,533 km, Makampuni yaliyokuwa "shortlisted" yamealikwa tarehe 22 September,2022 kuwasilisha zabuni tarehe 22 Novemba 2022. Katika mwaka wa fedha 2021/22 kati ya Julai 2021 hadi mei 2022 jumla ya mikataba 20 inayohusisha miradi ya ujenzi wa Barabara na viwanja vya ndege inayogharamiwa kwa fedha za washirika na maendeleo ilisainiwa.
Mhandisi Rogatus Mativila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na vipaumbele vya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23.

RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA SENSA NA MUONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO HAYO JIJINI DODOMA

Na. Kadala Komba Dodoma

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Hamza  Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa  Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi  ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo leo Oktoba 28,2022 jijini Dodoma.kushoto ni Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene


Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene,amesema kuwa Rais Samia  Suluhu Hassan anatarajia kutangaza   Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi  ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo.

Hayo ameyasema amesemwa leo Oktoba 28,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Oktoba 31,2022 historia itaandikwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma

Waziri Simbachawene amesema kuwa uzinduzi huo ni tukio muhimu katika historia ya maendeleo ya nchi ndio maana Serikali imeamua kuhakikisha kunakuwa na uwakilishi wa wananchi wa makundi yote ili waweze kushiriki katika tukio hili la kihistoria.

 

Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene,akizungumza na waandishi wa habari


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Hamza  Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (
 

NAIBU WAZIRI MERYPRICA MAHUNDI AMETOA OYO KALI KWA WALE WANAOCHEPUSHA MAJI



     
Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na wananchi wa kijiji cha Mpanga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Oktoba 27, 2022. 


Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akiwa na Mawaziri wenzake wa wizara za kisekta wakati wa mkutano wa hadhara kwenye kijiji Mpanga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Oktoba 27, 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akicheza na wananchi wa kijiji cha Mpanga katika halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe waliokuwa wakifurahia kijiji chao kubaki kwenye eneo la hifadhi ya Pori la Akiba la Mpanga Kipengele wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ilipofanya ziara katika mkoa wa Njombe Oktoba 27, 2022. 



 

Na Munir Shemweta, WANMM WANGING’OMBE

Meryprica mahindi ameonya wale wote wanaochepusha maji kwa ajili ya kufanya shughuli zao ikiwemo kumwagia mashamba na kueleza kuwa, kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

Meryprica alisema hayo Oktoba 27, 2022 wakati kamati ua mawaziri nane wa wizara za kisekta kushughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi ilipokwenda kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mpanga katika halmashauri ya wilaya ya Wanging,’ombe mkoani Njombe.

Aliwataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza maeneo maji yanapoanzia na kufuata sheria pale wanapotaka kutumia na kusisitiza  wanaochepusha maji kiholea waache kuacha mara moja.

‘’kuna utaratibu na siyo kama nazuia maji yasitume lakini kuna bodi ya maji ya mto rufiji inafanya kazi vizuri na kuna taratibu zake ukitaka kumwagilia maji nenda ofisi zao na unapewa  utaratibu na unakuwa mtanzania mzalendo.

“wewe unayelima na kumwagia mazao yako ufanikiwe basi usiwe kikwazo kwa watumiaji wengine wa maji majumbani kwa sababu ukitaka kuyavuta yote shambani kesho yake mradi, majengo makubwa na usambazaji mabomba yenye thamani ya mabilionji ya fedha itakwama, wewe unachepusha maji kwenye chanzo yatafikaje kwenye matenk na kusistiza tuache kuchepusha maji, alisema Meryprisca.

Aidha, alionya wananchi wanaolima ‘vinyungu’ kwenye vyanzo vya maji kuacha tabia hiyo na kueleza kuwa, mtu yeyote anayelima maeneo ya vyanzo maji ni adui namba moja wa zile jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu anasababisha maji kukauka na kusababisha miundo mbinu inayotolewa kwa ajili ya miradi ya maji kukosa thamani.

Kwa mujibu wa Meryprisca, shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ni mwiko na haviruhusiwi kwa kuwa zinasababisha maji kukauka huku lengo la serikali kupitia wizara yake  likiwa kuendelea  kupata maji zafi na salama.

Pia Naibu wa Waziri wa Maji aliwataka wananchi kulinda na kutunza wanatunza vyanzo vya maji na kuacha kabisa kufanya shughuli zozote za kibinadanamu kwa kuwa zinaweza kuharibu vyanzo hivyo alivyovieleza vinahitaji uoto wa asili ili viweze kuimarika.

 
 

KATAMBI AMEWATAKA VIJANA KUJITAMBUA NA KUTHUBUTU

Na. Kadala Komba Dodoma
 
 
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,  amewataka vijana kujitabua ,kuwa na uthubutu pamoja na kujiwekea malengo ,Amesema uwezi kupewa lifti kama umekaa nyumbani wakatio unasafari ya kwenda Daresalam lazima usogee Barabarani ukisimama tu wanajua wewe ni msafiri utapewa lifti .

Hayo yamejili jijini Dodoma Wilaya ya Chamwino wakati wa Kongamano la Vijana la fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya Vijana.

Katambi Amesema Lengo la Kongamano hili ni kumwezesha kijana kujitambua na atambue nafasi yake kwenye Jamii,

“kila kijana anatakiwa kupambana kivyake lakini akumbuke Serikali yetu ni Moja”

Aidha Naibu Waziri Katambi amewasisitiza Vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha tabia ya kuwa Tegemezi kwa Wazazi wao,

Ameongeza kuwa Vijana wengi wanafikra ya utegemezi hawataki kufanya kazi hawataki kujituma, Amesema Kama mnavyofahamu, vijana duniani kote ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kujenga uchumi wa mataifa yao. 

"Ili tuwe na Taifa lenye Nguvu tunahitaji Vijana wachapakazi wanao jituma hata vitabu vya Dini vimewataka Vijana kufanya kazi” Alisema Mhe. Katambi

Kwa upande wake Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora. Amewasisitiza Vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali Amesema Serikali hii ya hawamu ya sita imejipanga kutokomeza dibwi la Vijana wasio na kazi za kufanya, wasio na Ajira.

 "Ajira inaweza ikawa kwenye kilimo inaweza kuwa kwenye mifugo au kwenye Boda Boda na mama lishe, ndiyo maana tumekutana hapa kwa lengo la kujengana kupitia haya mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amewapongeza Vijana kwa kuwa na mwitikio Mkubwa wamejitokeza zaidi ya Vijana mia Tatu ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali namna ya kupambana na fursa tunataka Vijana wajiajili wenyewe.

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi

  Akizungumza na vijana katika kongamano la Vijana wilaya ya Chamwino

Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora Akitoa pongenzi kwa vijana waliyojitokeza kuuzulia kongamano la vijana jimboni kwake

Madiwani waliyouzulia kongamano la vijana


 



BAHI YAFUNGUA MILANGO KWA WANAFUNZI WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU.

 


Na Kadala Komba- Dodoma

Diwani wa Kata ya Mpamatwa, Sosthenes Mpandu amewataka wanafunzi  kusoma kwa juhudi na kujiamini ili kufanya vizuri katika mitihani yao hatimaye waweze kujiunga na masomo ya elimu ya juu.

Diwani huyo ameyasema hayo hivi karibuni katika mahafali ya  11 ya  kidato cha nne shule ya   Sekondari  Mpamatwa iliyopo Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma  ambapo alisema Serikali ya Awamu za Sita inayoongozwa na  Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imefuta ada kuanzia chekechea hadi kidato cha sita hivyo ni jukumu la wanafunzi kusoma kwa bidii.

Amesema kupitia  mfuko wa Wilaya wa kusomesha watoto wanaotoka mazingira duni kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha tano mradi unatoa fedha ya kijikimu kwa mtoto, magodoro, madafutali  pamoja na nauli ya kwenda shuleni.

 "Nendeni  mkafaulu  mitihani yenu vizuri kwani Wilaya hii ina  mfuko wa Wilaya wa kusaidia watoto wenye hali duni (KOIKA),  na Mimi ndiye Mwenyekiti wa mradi huo hivyo nawaomba mfanye vizuri kidato cha nne ili mradi uweze kukutimizia ndoto zako, kwa sababu usipofanya vizuri  na ukafaulu , ufaulu wa kati tafsiri  yake utampa mzigo mzazi   kukupeleka chuo kwani chuo ni gharama kubwa,” Amesema Diwani huyo.

Vivile vile Diwani Mpandu ameeleza kwamba  Kata hiyo  ina shule za msingi tano  huku akieleza kuwa  matarajio yao ni kuwa  na shule za Sekondari sita na zoezi hilo tayari limeanza Bahi makulu, ili waweze kuwa na shule yao kuwasaidia wanafunzi kuepuka kutembea umbali mrefu kufika shuleni  hivyo ni lengo letu Bahi iwe ya mfano kwa kuwa na shule za sekondari nyingi na shule nyingi za msingi.

"Kwa mwaka huu mradi umewapeleka wanafunzi 35 shule  katika Wilaya yetu ya Bahi waliyofanya vizuri kupitia mfuko huu, ndiyo maana nasema wanafunzi nendeni mkafanye vizuri kwenye mitihani yenu,nawaomba msiniangushe mfano  kuna kijana anaitwa Deogratius Malula alifanya vizuri sana mwaka jana akapata division one amekuwa mfano mzuri kwa  ufaulu wake na sisi  kupitia mfuko tumeweza kumsaidia,” Amebainisha.

Aidha Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Joyce Manyanda amesema  elimu sio lele mama  hivyo wanafunzi hawana budi kujiamini pindi mnapokuwa katika  chumba cha mitihani pamoja na kuwahimza wanafunzi kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani pindi wanapokuwa likizo.

 "Juhudi msiziweke katika masomo tu pia mfanye kazi za nyumbani wakati wa likizo msaidie wazazi na walezi wenu kufanya hivyo kutawajenga pia watoto wasaidieni wazazi kazi za nyumbani kipindi cha likizo kufanya hivyo kutawajenga kujitegemea siku zijazo,”Amesisitiza Bi. Joyce.

MWSHO

 

Diwani wa Kata ya Mpamatwa, Sosthenes Mpandu akizungumza  katika mahafali ya  11 ya  kidato cha nne shule ya   Sekondari  Mpamatwa   

 




NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAJI ATEMBELEA MKOA WA KIGOMA

Na Mwandishi wetu Kigoma 

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma. Mradi huu unatumia ziwa Tanganyika kama chanzo cha maji, katika eneo la fukwe ya Amani, Kata ya Bangwe Kigoma.

Mhe. Mahundi amesema hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo inatia matumaini, na amewaagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kigoma (KUWASA) kuhakikisha inafuatilia kwa karibu ujenzi wake kwa mkandarasi ili mradi huo ukamilike mapema ili wananchi wapate huduma.

Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma ya majisafi na salama. Aidha, amewahakikishia wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na Mji mdogo wa Mwandiga wasiwe na mashaka. Maji ya kutosha yanawafikia muda sio mrefu.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma Mhandisi Mbike Jones amesema mradi huo unatarajia kukamilika Desemba 2022 na utaweza kuhudumia wananchi zaidi ya 280,000 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na mji mdogo wa Mwandiga.

Amesema kwa sasa mahitaji ya wananchi wa maeneo wanayoyahudumia ni lita za ujazo Milioni 24 kwa siku wakati mradi huo unatarajiwa kuzalisha lita milioni 42 kwa siku. Gharama ya mradi huo inatarajiwa kufikia Euro 16,323,152.67 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 42 ikiwa ni ufadhili kutoka Jumuia ya Ulaya (EU)#SHINENEWSBLOG


 


 

 

JUMUIYA YA MARIDHIANO YAMTUNUKU RAIS SAMIA TUZO YA HESHIMA

Na. Kadala Komba Dodoma

JUMUIYA ya Maaridhiano mkoa wa Dodoma imemkadhi Tuzo Rais Samia Suluhu Hassani,kutokana na kuutambua mchango wake mkubwa wa kuiongoza nchi pamoja na Watanzania kwa amani.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano Mkuu maalum wa kuombea nchi uliofanyika mkoani hapa.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma Askofu Dk Evence Chande,alisema pamoja na kumkabidhi rais pia wengine waliokabidhiwa ni pamoja na Mkuu wa mkoa na Wakuu wa wilaya za Dodoma.

Alisema Jumuiya ya Maaridhiano imewakabidhi viongozi hao Tuzo hizo kutokana na kutambua mchango wao mkubwa kuwatumikia watanzania na kuifanya nchi kuendelea kuwa na amani kwa watu wake.

“Sisi Jumuiya ya Maaridhiano Tanzania mkoa wa Dodoma,tunahihakikishia serikali chini ya Rais na wasaidizi wake kuwa tutadumisha amani,na kutoa elimu kupitia madhehebu ya dini tunazoabudu ili watanzania waepende nchi yao na viongozi wao”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyumule alisema kuwa serikali inatambua na kutegemea Jumuiya hiyo ya Maaridhiano katika kuhubiri amani kwa waumini wao kupitia madhehebu yao.

Aidha serikali inatambua Jumuiya hiyo katika kujuhudi zake za kuhakikisha zinatatua kero mbalimbali zinazowakosesha amani kwa baadhi ya watu ikiwemo kwenye migogoro inayohusu ndoa,ardhi na ile inayosababisha kukosa haki za kimsingi.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwenye mkutano huo kwa kuwataka Watanzania pia kuendelea kuwapenda na kuwaamini viongozi wao huku wakiwaombea,ili waweze kuifanyaka kazi zao kwa misingi ya kiroho.

Alisema viongozi wa serikali wanahitaji msaada mkubwa wa kusaidiwa katika kuombewa kwenye nafasi zao,hivyo watanzania waendelee kuwaamini na kuwapenda ili kazi zao ziwe nyepesi katika kuwatumia bila kujali itikadi yoyote.

MWISHO.

 


 

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiangalia tuzo maalumu aliyotunukiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania kwa kazi nzuri anazolifanyia Taifa la Tganzania. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo,Askofu Dkt. Israel Maasa  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maridhiano kwnye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

 

 



 

BILIONI 1.7 ZIMETUMIKA KUJENGA BWENI LA WANAFUNZI WA KIKE

Na. Moreen Rojas, Dodoma.


Taasisi ya Afrika ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela inadhamiria kupendekeza ujenzi wa bweni la  wanafunzi wa kike wenye watoto wadogo na mahitaji maalum ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.7 zimetumika katika ujenzi huo.

Hayo yamesemwa na  Makamu Mkuu wa chuo Prof.Emmanuel Luoga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo.

Prof.Luoga amesema kuwa wameamua kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike wenye watoto wadogo na wenye mahitaji maalumu ili kuwawekea mazingira wezeshi yatakayowasaidia kusoma bila changamoto yoyote ambapo bweni hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 pindi awamu zote tatu za ujenzi utakapokamilika.


Aidha ameeleza kuwa wanafunzi wa kike wanapoingia vyuo vikuu kwa ajili ya shahada ya pili au ya tatu wanakuwa tayari wameshaanza majukumu ya kifamilia kwahiyo bweni hilo litasaidia kukidhi mahitaji yao.

Prof.Luoga ameongeza kuwa kipaombele kingine cha taasisi hiyo ni kuimarisha mifumo ya tehama katika chuo hicho na kuangalia uwezekano wa kuandaa wataalam watakaosaidia taifa katika kutoa elimu ya masafa ili kukabidiliana na upungufu wa walimu wa sayansi hapa nchini.

Taasisi ya afrika ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela ilianza rasmi kudahili wanafunzi mwaka 2021 na kujikita katika kufanya utafiti na ufundishaji katika ngazi ya uzamiri na uzamifu ambapo katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 serikali imetenga zaidi ya bilion 42 zitakazo tumika kwa ajili ya mishahara na matumizi mengine pamoja na miradi ya maendeleo.
Mwisho.
 
 
Makamu Mkuu wa chuo Prof.Emmanuel Luoga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi
 

 

ULAJI WA VYAKULA VYENYE SUMUKUVU UNAVYOATHIRI AFYA

Na mwandishi wetu , Simiyu

MADHARA ya sumukuvu huweza kujitokeza ndani ya muda mfupi, baada ya muda mrefu kutegemea na kiasi 
cha sumukuvu hiyo iliyopo kwenye chakula kilicholiwa,idadi ya milo ya chakula kilichochafuliwa na umri pamoja na hali ya afya ya mlaji.

Pia madhara ya Sumukuvu yanayotokea ndani ya muda mfupi husababishwa na ulaji wa kiasi kikubwa cha sumukuvu ikiwa  ni pamoja na kuathirika kwa ini, figo, mfumo wa fahamu, uwezo wa damu kuganda na hata kuweza kusababisha kifo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani  yenye Kaulimbiu isemayo 'Uzalishaji bora, Lishe bora, Mazingira bora na Maisha bora kwa wote, Habaki Mtu Nyuma' ambayo yanafanyika mkoani Simiyu  Kaimu Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), Khassim Msuya amesema kuwa Sumukuvu zinapokuwepo kwenye mazao au bidhaa hazionekani kwa macho, na kwamba huendelea kubaki hata baada ya chakula kupikwa au kusindikwa. 

Ameeleza kuwa madhara husababisha  kupungua kwa kinga ya mwili,kushuka kwa uzalishwaji wa maziwa na mayai,upungufu wa damu
,Kukosa hamu ya kula,kuharibika kwa mimba, Kuathiri mfumo wa uzazi, Kuharisha,Kutapika naVifo. 

"Mazao yanayochafuliwa na kuvu ni kama vile nafaka (mahindi, mtama, ulezi, mchele, ngano, uwele), mbegu za mafuta (alizeti, pamba), karanga, korosho, jamii ya mizizi iliyokaushwa (mihogo na viazi), viungo vilivyokaushwa, kahawa, mazao yanayotokana na mifugo (maziwa, mayai)," alisema Msuya.

Ameongeza kuwa athari za sumukuvu kiuchumi ni kukataliwa kwa bidhaa za chakula katika soko la ndani na nje ya nchi,Kuathiri utoshelevu wa chakula,kuathiri uzalishaji wa mifugo,kuongezeka kwa gharama za matibabu,kupungua kwa nguvu kazi na uzalishaji mali na kuongezeka kwa gharama za udhibiti.
 
 
 

"Dalili zinazoashiria kuwa mazao yamechafuliwa na kuvu wanaozalisha sumukuvu ni pamoja na ukungu, kuvu, harufu ya uvundo, punje kutengeneza vumbi, punje kugandamana au punje kubadilika rangi, na kuwa na rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu, kijani, chungwa au njano," ameeleza Mratibu huyo.

Amefafanua kuwa vichochezi vya uchafuzi wa sumukuvu kwenye mazao ya chakula na uwepo wa mazingira wezeshi kwa kuvu kuota na kuzalisha sumukuvu ni pamoja na hali ya hewa ,joto-ridi (temperature), unyevunyevu, ukame, mafuriko na mvua zisizotarajiwa wakati mazao yanapokaribia kukomaa na wakati wa kuvuna. 

Amesema inashauriwa mkulima kutumia mbegu zenye ukinzani dhidi ya magonjwa au zile zinazoweza kustahimili hali ya mazingira ya shamba husika.

 " Inashauriwa kutumia mbegu zinazoota na kutoa mazao kwa kipindi kifupi (mbegu za muda mfupi kulingana na eneo husika) ili kupunguza au kuepuka muda hatarishi kwa kushambuliwa na kuvu na kuchafuliwa na sumukuvu," amesema.

Pia mkulima anashauriwa kwa kadiri inavyowezekana kubadilisha mazao kwa mzunguko kati ya yale yanayoathiriwa na yasiyoathiriwa na kuvu,Mfano kupanda mahindi msimu mmoja na jamii ya mikunde msimu unaofuata

Akizungumzia mafanikio ya TANIPAC, Mratibu huyo amesema hadi sasa 
wakulima 61,410 wamepatiwa elimu juu ya udhibiti wa sumukuvu baada ya mavuno ambapo lengo lilikuwa ni kuwafikia wakulima hao  60,000.

" Kwa upande wa vijana  tumewawezesha vijana 420 kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wamejengewa uwezo kwenye kutengeneza Vihenge chuma (Metal silos) ambayo ni mbinu ya kuzuia mazingira wezeshi ya ukuaji wa kuvu, lengo lilikuwa 400 pamoja na Maafisa ugani 1,351 na Wanahabari 217,"alisema Msuya.

Mratibu huyo amefafanua kuwa tulifundisha vijana 420 na sasa tunawafanyia program atamizi Kwa Kuwafundisha maswala ya ujasiriamali Ili waweze kutengeneza vihenge kibiashara. 

Mratibu huyo ameeleza kuwa lengo ni kutengeneza vihenge 10,000. Mradi utapromote vihenge kuhusu hiyo technolojia na kueajulisha wananchi na kuweza kuwapa fursa ya kutengeneza vihenge hivyo.


CHANGAMOTO ZA MRADI

Mratibu huyo amesema kuwa Virusi vya Korona (COVID -19), ilizuia mikusanyiko hivyo mradi ulichelewa kutoa elimu ya ana kwa ana kwa  wakulima  ambapo kutumia vyombo vya habari  kufikia wakulima hao.

Amefafanua kuwa  mradi  huo wa TANIPAC ni wa miaka mitano  ambapo ulianza mwaka 2019  na yanatarajiwa kukamilika mwaka  2024, ambao unaotekelezwa Tanzania Bara na Visiwani – Zanzibar (Unguja na Pemba).

Mratibu huyo ameongeza kuwa pamoja na changamoto ya COVID -19 lakini  wananchi, taasisi na Wizara tayari wanauelewa wa  madhara ya Sumukuvu huku  akitolea mfano Wizara ya Mifugo na uvuvi wameomba kupatiwa elimu ya sumukuvu.

"Watu wanaokuja kwenye banda letu katika maadhimisho haya tayari wana uelewa wa Sumukuvu ila wanataka kujua baadhi ya vipengele wanavyokabiliana navyo," amesema Msuya.


Siku ya Chakula Duniani huadhimishwa Oktoba 16, kila mwaka katika nchi zipatazo 150 ikiwamo Tanzania.

Lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu Usalama wa Chakula, utambuzi na usimamizi wa athari zitokanazo na chakula pamoja na kuboresha afya za binadamu kupitia utoaji wa elimu hiyo.


Shirika la Chakula na Kilimo na Umaja wa Mataifa (FAO), na serikali ya Tanzania kupitia program inayo na Umoja wa Ulaya Agree Connect imegundua kampeni ya kitaifa ya 'Lishe Bora ni Mtaji' ili kujenga tabia ya zinazofaa za milo hapa nchini kwa kutumia vyakuka vinavuopatikana Tanzania.
 
 

Kaimu Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), Khassim Musya akitoa elimu wa wananchi waliofika katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani  yenye Kaulimbiu isemayo 'Uzalishaji bora, Lishe bora, Mazingira bora na Maisha bora kwa wote, Habaki Mtu Nyuma'
ambayo yanafanyika mkoani Simiyu.
 
 
 


 

BILIONI 2.2 ZAREJESHWA NA HALMASHAURI KWENYE MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA KUPITIA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2022

Mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2022 zilizofikia kilele tarehe 14 Oktoba 2022 mkoani Kagera, zimefanikiwa kurejesha fedha za mikopo kwa vijana kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 2.2.

Moja ya ajenda ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 ilikuwa ni kuhakikisha fedha zote zilizorejeshwa na vijana waliopewa mikopo kupitia Mfuko huo na kupotelea katika ngazi za Halmashauri nchini zinarejeshwa katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu

Akiongea wakati wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, -Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alisema serikali kuu kwa nyakati tofauti kuanzaia mwaka wa fedha 1993/1994 imekuwa ikitoa fedha za mikopo kwa vijana kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana.  

“Vijana wetu walitumia fedha hizo katika shughuli zao za kiuchumi na kurejesha kwa wakati katika halmashauri zao.
 Lakini katika hali ya kustaajabisha baadhi ya halmashauri hizo hazikurejesha fedha hizo Serikali kuu kama miongozo ya fedha hizo ilivyozitaka na hivyo kudhoofisha jitihada za Serikali Kuu
 kuwahudumia vijana. "

Mhe. Prof. Ndalichalko alisisitiza kuwa, lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huo ni kuwawezesha vijana wote nchini kupata mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu ili kuanzisha au kuendeleza miradi yao ya uzalishaji mali. 

Aidha alifafanua kuwa Kupitia utaratibu huo, vijana huwezeshwa kujitegemea, kupunguza umaskini wa kipato na kujiajiri wenyewe.

Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Julai mwaka huu imetoa muongozo mpya wa kutoa mikopo kupitia Mfuko huo, ambapo kwa sasa kijana mmoja anaweza kupewa mkopo huo kupitia Halmashauri, hiyo ikiwa ni tofauti na awali ambapo vijana walipata mikopo hiyo wakiwa katika vikundi.

Aidha, kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 kiasi cha fedha bilioni moja kimetengwa kwenye Mfuko huo.


Mfuko wa maendeleo ya Vijana ulianzishwa na serikali mnamo mwaka wa fedha 1994/1994 chini ya sheria ya (The exchequer and Audit ordinance (Cap.439) no. 21 ya mwaka 1961 kifungu cha 17 kifungu kidogo cha kwanza.

 Lengo la Mfuko huo ni kuwawezesha vijana kiuchumi  kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu.


 

BILIONI 134.9 ZIMETENGWA KWAJILI YA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA

Na Moreen Rojas

Bohari ya dawa( MSD ) iliyopo chini ya taasisi ya wizara ya Afya imepokea shilingi Bilion 134.9 Kati ya shilingi Bilion 200 zilizolengwa kwa manunuzi ya bidhaa za afya kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Hayo yamesemwa na Mkurugezi mkuu wa bohari ya dawa ( MSD) Mavera Tukai wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma juu ya maboresho ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Amesema bohari ya dawa imetekeleza majukumu manne ambayo ni uzalishaji,utunzaji na usambazaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya pamoja na vituo binafsi vilivyohizinishwa na wizara ya Afya.

Mpaka sasa vituo vya kutolea huduma za Afya ni 7, 153 inchi zima kupitia kanda 10 zilizopo Dodoma, Dar -es- salaam, Mtwara, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Tanga, kagera mbeya na Iringa.

Aidha Amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 bohari ya dawa imeendelea kufanya maboresho ya utekelezaji kama ilivyoelezwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambayo  mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya na utawala bora.

" Maitaji yanayotekelezwa kwa sasa  ni kuingia mikataba ya muda mfupi na wazalishaji wa bidhaa za afya,kufanya mapitio ya ununuzi wa bidhaa za afya , kufanya mapitio ya mabadiliko ya  matokeo ya bidhaa  za afya, kufanya matukio ya usimamizi wa mali pamoja na kuimarisha ushirikiano wa wateja na wadau wa sekta nyingine za afya"Amesema Tukai.


Pia Tukai amesema usambazaji wa bidhaa za afya ufanyika mara 6 kwa mwaka ambapo kila kituo upelekewa bidhaa za afya kila baada ya miezi miwili kwa mujibu wa kalenda ya usambazaji Pamoja na kuimalisha upatikanaji wa dawa hadi kufika 90%.

Mwisho.
 

 

 

*WIZARA YA KATIBA KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA KIDIJITALI – DKT NDUMBARO*



Na. Mwandishi wetu Arusha 
 
 
 
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wizara ya Katiba na Sheria imekusudia kuhakikisha huduma za kisheria zinazotolewa na Wizara na Taasisi zilizo chini yake zinapatikana kwa njia ya TEHAMA. 

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria, Wasaidizi wa Kisheria, Mawakili, Wanasheria na Maafisa wa Jeshi la Magereza ambayo inafanyika kuanzia leo Oktoba 17, 2022 Jijini Arusha.

Dkt Ndumbaro amesema “Kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA kwenye utoaji wa huduma, Wizara ya Katiba na Sheria imekusudia kuhakikisha huduma za kisheria zinazotolewa na Wizara na Taasisi zilizo chini yake zinapatikana kwa njia ya TEHAMA. Hili litawezesha huduma kupatikana kwa wakati na hatimaye kuwezesha vyombo vingine vya utoaji haki kutoa haki kwa wakati na kwa gharama nafuu.”

Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa TEHAMA imekuwa na mchango mkubwa kwenye utoaji wa huduma na utendaji wa Serikali kwa ujumla. Faida zinazopatikana ni pamoja na  kuwepo kwa utunzaji wa kumbukumbu sahihi za wananchi, kuweka  uwazi na uwajibikaji wa utoaji huduma hususan panapokuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi, kurahisisha upatikanaji wa huduma, na vilevile kuondoa mianya ya rushwa kwenye utoaji huduma kwa kuwa  hakuna mwingiliano kati ya mtoa huduma na mteja.

Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa ni vyema kuwa na mifumo mizuri ya kisheria ambayo itarahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati; mifumo ambayo itawezesha wananchi kupata huduma za kisheria popote walipo kwa gharama nafuu katika kuifikia haki. Uwepo wa mifumo, utawapunguzia wananchi muda na gharama za kushughulikia masuala ya kisheria na badala yake watajikita zaidi katika shughuli zingine za kiuchumi na kimaendeleo hivyo basi kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa Wizara ina jukumu kubwa la kutoa elimu ya Katiba  na Sheria kwa wananchi hususan vijana kwani hiyo itawasaidia kujua sheria na kudai haki zao.

Dkt. Ndumbaro amesema “Naamini kwamba Wizara ina jukumu kubwa la kutoa elimu ya Katiba kwani huwezi kwenda kutoa kitu kipya wakati hujui cha zamani, tupate elimu ya Katiba iliyopo sasa ili tujue mazuri yakwenda nayo katika Katiba mpya na kuacha mabaya yaliyopo.”

Akimkaribisha Waziri Ndumbaro kufungua warsha hiyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. David Lyamongi amesema Wasaidizi wa kisheria wapewe kipaumbele katika kutekeleza kazi zao kwani wanasaidia sana jamii hasa wajane na yatima.

Bw. Lyamongi amesema “mchango wa Wasaidizi wa Kisheria ni mkubwa sana katika jamii hususan katika Mkoa wa Arusha kwenye masuala ya kisheria yaliyomshinda mwananchi au kushindwa kwenda mwenyewe mahakamani hivyo kuhitaji uwakilishi.”

Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria nchini Bi. Felistas Mushi amesema mafunzo hayo yamewashirikisha Watoa Huduma za kisheria kutoka kwenye Mashirika kumi na tano, Wasajili Wasaidizi na Maafisa Magereza kutoka mikoa kumi ya Tanzania Bara. Washiriki hao wamechaguliwa kwa sababu wapo karibu na wananchi sanjali na kuwasaidia wananchi wengi wa chini waliopo kwenye maeneo yao, alisema Bi. Mushi.

Awali akitoa maelezo ya utangulizi Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Gabriel Ally amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Bw. Gabriel amesema huduma za TEHAMA zinarahisisha kufikisha huduma za kisheria kwa wananchi popote pale walipo hivyo ni muhimu makundi hayo manne yakazingatia mafunzo hayo katika utendaji kazi wao kwa kuwa zinahusiana na wananchi kwa kiasi kikubwa.

Mafunzo haya yanahusisha mifumo inayohusu usajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria ambazo zinatolewa chini ya Sheria ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017, mfumo wa usajili wa watoa huduma za maridhiano, usuluhishi, na upatanishi kama ilivyobainishwa chini ya Sheria ya Usuluhishi ya Mwaka 2020.  Mifumo mingine ni pamoja na uwasilishaji wa malalamiko, maombi ya huduma za msaada wa kisheria, maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha mashauri mahakamani nje ya muda pamoja na huduma nyingine za kisheria.
 
 

 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro

 

ASKOFU KINYAIYA "WAZAZI PELEKENI WATOTO SHULE"



Na. Kadala Komba Dodoma
 
 
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya amewataka wazazi  kuwapeleka watoto shule badala ya kuwapa kazi ya kuchunga Ng'ombe .

Askofu huyo aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa misa 
ya Sakramenti ya kipaimara iliyofanyika katika  kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Wilaya ya Bahi.

Amesema elimu bora  ni haki ya kila mtoto ambapo hatua hiyo itasaidia watoto kutimiza ndoto zao pamoja na kuongeza pato la familia na kuondokana na umasikini.

"Ni  kweli hizi familia zina utajiri wa mali nyie ni wafugaji wa mifugo na kupitia mifugo mnamiliki mali nyingi lakini mali bila elimu ni shida, wapelekeni watoto shule wakapate elimu darasani, wafundisheni watoto  kusoma pindi wanapokuwa Nyumbani, "Alisema Askofu huyo. 

Pia Askofu Mhashamu aliwasihi watoto kutumia vizuri fursa ya elimu wanapopelekwa shule kwa kusoma bidii  kusoma kwa  bidii  na kutokukubali kukatishwa tamaa. 

Katika hatua nyingine Askofu alipongeza Parokia hiyo kwa juhudi za kimaendeleo ambazo Parokia inaendelea kufanya uhakikisha jamii inakuwa na hofu ya Mungu na maadili. 

 "Parokia hii inakuwa kwa kasi hivyo msikubali kukatishwa tamaa na watu, msije kugeuka nyuma ukigeuka nyuma utakuwa jiwe la chumvi hivyo tunatakiwa kutazama  tulijenge Kanisa, "Alihimiza. 

Kwa upande wake Katibu wa  Halmashauri ya Walei Parokia, Eresta Oiso ameeleza kwamba  jumla ya watoto 1,776 wamepata Sakramenti ya ubatizo, komunio ya kwanza 329 na ndoa 71 zilifungwa pamoja na kutoa  Sakramenti ya kipaimara kwa watoto 301 pamoja na kufungisha ndoa 5.

"Parokia ya Bahi ni miongoni mwa Parokia zilizomo ndani ya Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Dekania ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji inapatikana mpakani mwa jimbo kuu Katoliki Dodoma na jimbo la Singida takribani kilomita  55 kutoka Dodoma mjini, "Ameeleza.

Aidha amebainisha kuwa  Parokia ya Bahi ina Jumla ya vigango 13 , Vigango 11 na jumuiya ndogo ndogo za kikristo 155.
 
 
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya

 





 MATUKIO YA PICHA YA KIPAIMARA
 
 

 

RAIS SAMIA ATEMBELEA JENGO LA MAKUMBUSHO YA HAYATI DKT.JOHN POMBE MAGUFULI,AKAGUA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA CHATO MKOANI GEITA


  •  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua kwenye Kaburi la Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
  •  


  •  


KAMPASI YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUJENGWA KAGERA-WAZIRI MKENDA

 

Na Mathias Canal, WEST-Kagera

 

Katika kuboresha huduma za upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi nchini Serikali imepanga kujenga Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Mkoani Kagera.

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema hayo mbele ya Mgeni rasmi-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan tarehe 13 Octoba 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera.

 

Amesema kuwa Kampasi hiyo itajengwa kwenye vijiji vya Itahwa na Kangabusharo kwenye eneo la ekari 323.45. Kati ya ekari 323.45 zilizotolewa, ekari 231.36 ziko katika kijiji cha Itahwa na ekari 92.09 katika kijiji cha Kangabusharo.


Akizungumza kuhusu Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera, Waziri Mkenda amesema chuo hicho chenye hadhi ya Kimataifa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa thamani ya Yuani za Kichina Milioni 60.18 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 22.4, Fedha hizo zinajumuisha shughuli za ujenzi, uwekwaji wa baadhi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia, mashine na samani katika majengo.

 

Waziri Mkenda amesema kuwa Chuo hicho chenye karakana, vifaa na miundo mbinu ya kisasa kilichojengwa kwa msaada wa Serikali ya China kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma.

 

Waziri Mkenda amesema kuwa Chuo hicho cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera kilichozinduliwa na Mhe Rais ni hatua nyingine muhimu katika mpango wa kukamilisha ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya ngazi ya Mikoa.

 

“Mheshimiwa Rais Tulibakisha mikoa michache sana. Kwa sasa, mikoa mingine ambayo ujenzi unaendelea ni Njombe, Simiyu, Rukwa na Geita na mpango wa ujenzi wa chuo cha Mkoa wa Songwe unaendelea kukamilishwa ili ujenzi uanze” Amekaririwa Prof Mkenda

 

Prof Mkenda amesema kuwa serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya ngazi ya wilaya ambavyo hadi sasa Wilaya 77 zina vyuo na ujenzi wa vyuo katika Wilaya 62 unatarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha 2022/23 ambapo Serikali imetenga shilingi bilioni 100.

 

 


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia