Home »
» WALIOTUMIA PICHA YA VIJANA WA JKT WALIOKUWA MAKAMBINI KUWA WANA VVU WAMETAKIWA KUOMBA RADHI
WALIOTUMIA PICHA YA VIJANA WA JKT WALIOKUWA MAKAMBINI KUWA WANA VVU WAMETAKIWA KUOMBA RADHI
Na Kadala Komba, Dodoma.
JESHI la Kujenga Taifa (JKT),limesema kitendo cha baadhi ya mitandao ya kijamii na magazeti kutumia picha za vijana wengine wanaohudhuria mafunzo ya JKT wa wasiohusika katika habari ni udhalilishaji.
Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Februari 6,2023 na Mkuu wa Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,wakati akitoa ufafanuzi kwa umma kupitia waandishi wa habari kuhusu vijana 147 wa JKT kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika habari iliyoripotiwa Bungeni Februari 3,2023 na kamati ya UKIMWI ambapo amesema ni kitendo cha ukosefu wa maadili ya uandishi wa habari na kwamba uhuru wa vyombo vya habari haukutumika ipasavyo.
"Jeshi la kujenga Taifa limesikitishwa na habari hii ya vijana idadi ya 147 kuwa na maambukizi ya VVU na kuambatanishwa na picha ya vijana wengine waliohudhuria mafunzo ya JKT Makambini,"amesema.
Kutokana na hayo Brigedia Jenerali Mabena amevitaka vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii vilivyoripoti habari hiyo kwa kuweka picha za vijana wa JKT ambao si wahusika wa habari hiyo,kuomba radhi na kuondoa picha hiyo mara moja.
Aidha Mabena ametoa ufafanuzi kuwa mafunzo ya vijana wa kundi la lazima yaani wahitimu wa kidato cha sita uendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu.
Amesema kabla ya kuanza mafunzo vijana hufanyiwa usahili wa nyaraka zao pamoja vipimo vya afya ili kufahamu utimamu wa mwili(Physical Fitness).
Ambapo vijana ambao majibu ya vipimo vyao huwa na changamoto za kiafya hufanya mafunzo yao chini ya uangalizi wa wakufunzi ili kuhakikisha wanamaliza mafunzo yao salama.
"Kwa kuwa hilo ni kundi la lazima(Compulsory),vijana wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho(Physical Disabilities)hupokelewa katika kikosi cha Ruvu JKT ambacho kina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo,"amesema.
Vilevile amesisitiza kuwa kigezo cha Afya kwa vijana hao wa kundi la lazima wanaokuja makambini wakiwa na changamoto za kiafya kinazingatiwa kwa kuwaweka chini ya uangalizi.
"JKT linazingatia sheria kanuni na taratibu za kitabibu sambamba na kuzingatia mila na desturi za nchi yetu katika kutekeleza jukumu lake la msingi la malezi ya vijana.
Pamoja na hayo Mabena aliwatoa wananchi hofu kuwa JKT ni salama yenye kuzingatia sheria na taratibu za miongozo ya malezi ya vijana na kundi la lazima na vijana wa kujitolea.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari,Gerson Msigwa amewataka wananchi kutambua kuwa vijana hao waliokutwa na maambukizi ya VVU ni wale ambao bado hawajaingia JKT.
"Wanahabari tuzingatie weledi na niwatake vyombo vya habari walioripoti habari hiyo kwakutumia picha za vijana wa JKT ambao tayari wapo Makambini waombe radhi,"amesema Msigwa.
Mkuu wa Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,wakati akitoa ufafanuzi kwa umma kupitia waandishi wa habari kuhusu vijana 147 wa JKT kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika habari iliyoripotiwa Bungeni Februari 3,2023 na kamati ya UKIMWI
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari,Gerson Msigwa
Related Posts:
VIONGOZI WA UVCCM BAHI WAMEONYWA KUTOBWETEKA Na Peter Mkwavila BAHI. VIONGOZI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) wa wilayani Bahi,wameonywa kutobweteka na kulewa na madaraka,badala yake wafanye kazi za kujiingizia kipato pamoja na kukisaidia chama cha Mapinduz… Read More
MKUU WA MKOA DODOMA AMEWATAKA WAAJIRI KUBAINI MBINU ZA KUPUNGUZA AJARI MAENEO YA KAZI Na Moren Rojas DodomaMkuu wa mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE amewataka waajiri kubaini mbinu za kupunguza ajali kwa wafanyakazi ili kupunguza ajali kazini.Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo kwa Madaktari juu ya ta… Read More
*KABLA YA KUPAMBANA NA MCHAWI WA MAISHA YAKO BADILISHA KWANZA MIND-SET YAKO, BADILISHA KWANZA MITAZAMO YAKO YA NDANI*Biblia inasema hivi*Hosea 4:6(a) Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;*Kwenye hili andiko Mungu hasemi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWASABABU YA SHETANI AU WACHAWI , isipokuwa anasema hivi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KU… Read More
MITAA ISIYO NA UMEME IFIKAPO DESEMBA 2022 IWE IMESAMBAZIWA UMEME Imeelezwa kuwa, Mitaa 28 ambayo bado haina umeme katika Jimbo la Handeni mjini ipo katika mpango wa kupatiwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini… Read More
EURO BILIONI 10.1 ZATUMIKA MRADI UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA TANZANI.Na. Kadala Komba Dodoma Kilimo ni sekta inayotegemewa sana Tanzania kwa ajili ya kutoa malighafi kwa ajili ya taifa letu.Tarehe 16 mwaka 2021 mwezi wa 2 Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba wa kuteke… Read More
0 Comments:
Post a Comment