Home »
» RC KINDAMBA AWATAKA MA-DED KUSIMAMIA UKUSANYAJI FEDHA
RC KINDAMBA AWATAKA MA-DED KUSIMAMIA UKUSANYAJI FEDHA
Na. Mwandishi wetu Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo wasimamie fedha zinazokusanywa zipelekwa benki ili kuepuka wakusanyaji kuzitumia fedha hizo.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito huo umetolewa leo Jumanne Februari 7, 2023 wakati wa kikao cha tathmini za utendaji wa Halmashauri za mkoa wa Songwe.
RC Kindamba ameongeza kuwa utekelezaji hafifu wa vikao vya kisheria vinavyosababisha malalamiko mengi ambapo vingeshughulikiwa chini kabisa.
Ametaja moja ya kazi ya kiongozi katika watu anaowaongoza ni kisikiliza na kutatua kero kwa wakati zinazowakabili wananchi.
Ametaja kazi nyingine kuwa ni kusimamia ukusanyaji wa mapato, ulinzi na usalama.
"Tuendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi na kusimamia kwa nguvu eneo la ukusanyaji wa mapato"
Amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kusimamia kwa weledi miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati.
Related Posts:
WANANCHI WAALIKWA MIAKA 60 YA JKT Na Moreen Rojas,Dodoma.Waziri wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)Mhe.Innocent Bashungwa amewaalika wananchi wa mkoa wa Dodoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo yatakayofanyika tarehe 10 julai siku ya jumatatu … Read More
BAHI KINARA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA BOOST Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe madarasa 51, Vyoo 63 na nyumba 1 ya waalimu ikiwa ni sawa na shule 7 zilizokamilika katika Wilaya ya Bahi. Ak… Read More
HUAWEI AT MWC SHANGHAI 2023:BOOSTING 5G EVOLUTION TOWARDS 5.5G REVITALIZE THE DIGITAL ECONOMYHuawei has shown up in full force for MWC Shanghai 2023, with their activities all falling under their theme of "GUIDE to the Intelligent World". This year, the company's activities include an experiential tour that takes aud… Read More
SERIKALI HAIPO TAYARI KUMPOTEZA MTU Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Serikali haipo tayari kuona Mwananchi yeyote anapoteza uhai wake kwa sababu za ama ujambazi au udereva mbovu barabarani au migogoro ba… Read More
WAPIGA KURA 74,642 KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI KESHO Na Mwandishi maalum - NECWapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara kesho Julai 13,2023.Jumla ya w… Read More
0 Comments:
Post a Comment