Home »
» PROF.MKENDA :BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA KWA WANAFUNZI NA WASIMAMIZI WA MITIHANI KIDATO NNE MWAKA 2022 .
PROF.MKENDA :BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA KWA WANAFUNZI NA WASIMAMIZI WA MITIHANI KIDATO NNE MWAKA 2022 .
Na. Mwandishi wetu Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imesema imedhamiria kukomesha vitendo vya wizi wa mitihani huku ikiridhishwa na uamuzi wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa wanafunzi 337 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao ya kidato cha nne mwaka 2022.
Hayo yamesemwa leo Februari 8,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof.Adolf Mkenda,wakati akitoa ufafanuzi kwa waaandishi wa habari kufuatia Video iliyosambaa mitandaoni ikionesha Wazazi wa wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari Thaqaafa iliyopo Jijini Mwanza wakiandamana kudai Watoto wao hawajatolewa matokeo ya Kidato Cha Nne.
Prof.Mkenda amesema Wizara hiyo itapeleka marekebisho ya sheria ya baraza hilo bungeni ili hatua zaidi zichukuliwe kwa wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani.
“Mtihani wa darasa la saba tulivyorudia tulitumia mabilioni ya fedha za watanzania kwa hiyo ni uhujumu uchumi kudanganya kwenye mitihani, polisi wanafanya uchunguzi kwenye hili tunaamini hatua zitachukuliwa na wizara imeridhika na hatua zilizochukuliwa na baraza,
”amesema Prof.Mkenda
Amesema kuwaa kati ya watahiniwa 560375 waliofanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2022 matokeo ya watahiniwa 337 sawa na asilimia 0.06 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wamefutiwa matokeao kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujaza matusi,kuingia kwenye chumba cha mitihani na maandishi,kuingia na simu na smartwatch.
Prof.Mkenda amesema kuwa serikali imeridhishwa na uamuzi uliofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA) kuhusu wanafunzi 337 waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani hiyo.
“Sisi uongozi wa baraza tumekutana na kila kundi la wale ambao matokeo yao yamefutwa, tumejiridhisha na tungependa kutoa matokeo yafuatayo wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne ni 560,335 kati ya hao wanafunzi waliofutiwa matokeo ni 337.”
“Hii ni asilimia 0.06 ya watahiniwa wote ni asilimia ndogo sana lakini inagusa watanzania wenzetu wanafunzi wengine 20 matokeo yao hayajafutwa yamezuiwa bado uchunguzi unaendelea na utakapokamilika baraza litachukua hatua stahiki,”amesisitiza
.
Amesema kuwa Wizi wa Mitihani ni kosa kubwa sana ni sawa na uhujumu uchumi na hatukubaliani nalo na wezi wa mitihani lazima wakamatwe na washughulikie kisheria kwa sababu haivumiliki.
‘Tayari barua zimeandikwa kwa Mamlaka husika juu ya Wasimamizi wa mitihani hiyo kwani Kuna uchunguzi unaonesha Usimamizi ulikuwa Mbovu huku Polisi wakiendelea kufanya uchunguzi, kwa kuhoji wanafunzi na Walimu ambapo wanafunzi wamekiri.’amesema Prof.Mkenda
Related Posts:
UTPC KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA WANACHAMA NA WADAU. Na Moreen Rojas,Dodoma.Rais wa UTPC Deogratius Nshokolo amesema katika kipindi cha 2023_2025 UTPC inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya wanachama na wadau wengine wa habari nchini.Rais wa UTPC ameyasema hayo w… Read More
Naibu Waziri Nderiananga akutana na kufanya mazungumzo na RC Morogoro Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Ku… Read More
*RAIS SAMIA AMEIBEBA KWA DHATI AJENDA YA MATUMIZI NISHATI MBADALA – NAIBU WAZIRI KAPINGA* *Lilian Lundo, Veronica Simba na Zuena Msuya - Songea*Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameibeba kwa dhati ajenda ya matumizi ya … Read More
*MAADHIMISHO YA SIKU YA MWALIMU BUKOMBE 2023*Leo Oktoba 6, 2023 Sherehe ya Siku ya Mwalimu Duniani inaadhimishwa katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambayo itahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa pamoja na Walimu kutoka wilayani Bukombe. Mgeni rasmi kat… Read More
*GEITA TUPO NJIANI UWT MOTOO MOTOO**ZIARA YA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA BARAZA KUU LA UWT PAMOJA NA WAJUMBE WA NEC MKOA WA GEITA*Ikiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Mary Chatand… Read More
0 Comments:
Post a Comment