Subscribe Us

DIWANI NDONU AMETOA SIKU SABA KWA WAZAZI WA WANAFUNZI AMBAO HAWAJARIPOTI SHULE

Na. Kadala Komba Dodoma Diwani Kata ya Bahi Mkoa wa Dodoma Mhe.Augustino Ndonu ametoa siku saba kwa wazazi wa wanafunzi ambao bado hawajaripoti shule hadi sasa baada ya kufaulu darasa la saba na kuchanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 kuhakikisha wanafanya hivyo na atakae kaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Mhe Ndonu ametoa agizo hilo wakati akitoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi 59 kwenye kata hiyo kwa wanafunzi wanaohishi mazingira magumu, Miongoni mwa vifaa alivyotoa kwa wanafunzi hao ni pamoja na vitambaa vya kushona sare za shule ikiwa ni kaptula sketi, shati ,viatu,daftari soksi,pamoja na kalamu. “Zaidi ya Million Tatu zimetumika kununua vifaa hivi fedha ambazo zimetoka kwenye Halmashauri yetu kwenye mfuko wa Elimu kwa lengo la kuboresha mzingira ya kupata Elimu Bora leo tumegawa shule 5 zilizopo kwenye kata yetu ,hivyo naagiza kuanzia leo January 24,2023 hadi ifikapo January 30 ,2023 watoto hao wawe wamekwisha ripoti shule na kuanza masomo. Mhe Ndonu amesema baada ya siku hizo wataanza msako na kukamata wazazi wote ambao watakeuka agizo hilo na kulipa faini ya Elfu 50. Pia nakuwaeleza faida za kusomesha mtoto kwamba akifanikia mtoto faida itakua ya mzazi na familia nzima. Kwaupande wake Afisa Elimu Sekondary Bahi Mery Chakupewa amesema kupitia mfuko wa Elimu Bahi ambao umeanzishwa na Halmashauri kwa lengo la kusaidia wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu, mfuko umewezesha wanafunzi kuwa na ufaulu mzuri katika mitihani ya shule za msingi na secondary, sababu wazazi wanatambua uwepo wa mfuko huo hivyo wanaimiza watoto kuanza shule na kumaliza. Aidha Mamos Longoye Mkuu wa shule Bahi B sekondari ameishukuru serikali kwa kuanzisha mfuko huo ambao unawasaidi sana watoto wanaotoka mazingira magumu kuna wanafunzi wanashindwa kuja shule hawana sare za shule na viatu kupitia mfuko huu watoto hao wameludi shule na sasa wanaendelea na masomo. Hapines Sevelina mwanafunzi wa kidato cha kwanza secondary B mnufaika wa mfuko huo ameshukuru kwa serikali kuwasaidi na kuahidi kufanya vizuri katika masomo yake.
Diwani Kata ya Bahi Mkoa wa Dodoma Mhe.Augustino Ndonu wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wanaoishi mazingira magumu.
Diwani Kata ya Bahi Mkoa wa Dodoma Mhe.Augustino Ndonu wakati akikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi
wazazi wa wanafunzi wanaoishi mszingira magumu

0 Comments:

Post a Comment