Home »
» NSSF IMEJIPANGA KUANZA KUTOA MAFAO KWA SEKTA ISIYO RASMI
NSSF IMEJIPANGA KUANZA KUTOA MAFAO KWA SEKTA ISIYO RASMI
Na. Kadala Komba Dodoma.
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)umewataka wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huo kwa kupeleka michango yao na hatimaye kuwa kwenye mfumo wa mafao hali itakayosaidia kupunguza umasikini.
Hayo yameelezwa jijini hapa leo ,Februari 8,2023 na Mkurugenzi Mkuu NSSF,Masha Mshomba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko na mwelekeo wa utendaji katika mwaka wa fedha 2022/23 .
Amesema wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kama vile Mama Lishe, bodaboda, wafugaji, wakulima n.k wanapaswa kubadili mtazamo wa maisha ili kuepukana na changamoto za uzeeni kwa Kujiunga na NSSF kwani watapata pensheni ya uzeeni kama wale walio katika sekta rasmi .
"Tunajiimarisha zaidi kwani mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi utasaidia kuimarisha na kuboresha maisha ya watanzania,Kila mtanzania anapaswa kuelewa kuwa pensheni ya uzeeni ni haki ya kila Mtanzania hivyo ni wakati sasa kwa wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na NSSF ili kufaidika na Mafao mbalimbali yatolewayo ikiwemo pensheni ya uzeeni,mikopo na bima ya afya,"amesema Mkurugenzi huyo.
Katika hatua nyingine Mshomba ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, mfuko huo unatarajia kukusanya michango ya shilingi trilioni 1.6 ambayo ni ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na michango ya shilingi trilioni 1.4 iliyokusanywa na Mfuko katika mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022.
Amesema Mfuko umeendelea kuimarisha mifumo na usimamizi wa fedha ili kuepuka mianya ya upotevu wa fedha, kuendelea kumudu gharama za uendeshaji pamoja na kulipa mafao stahiki kwa wastaafu na wanufaika wengine.
"Katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, Mfuko unatarajia kulipa mafao yenye thamani ya shilingi bilioni 769.3 ambayo ni ongezeko la asilimia 17 ukilinganisha na shilingi bilioni 659.8 zilizolipwa katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022,"amesema Mshomba.
Ili kujiiamarisha kiuchumi zaidi amesema kuwa kufikia Julai mosi mwaka huu mfumo huo utaweza kuzalisha sukari kupitia kiwanda cha sukari cha Mkulazi.
Amesema kiwanda hicho kitapunguza changamoto ya uhaba wa sukari inayojitokeza mara kwa mara na kulazimu serikali kutegemea wazalishameeleza kuwa mfuko huo katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, unatarajia kukusanya michango ya shilingi trilioni 1.6 ambayo ni ongezeko la asilimia 14 .
Mshomba ameeleza kuwa Mradi huo unatarajiwa kutoa fursa ya soko kwa wakulima wa nje wanaolima miwa katika mashamba yenye takribani hekta 450, miundombinu mingine kwa ajili ya wananchi wanaouzunguka mradi huo,ajira zaidi ya 2,315 za moja kwa moja, megawati 15 za umeme zinazotarajiwa kuingizwa katika gridi ya Taifa kupitia kituo cha kupokelea na kupoza umeme Msamvu.
Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo Mshomba ameeleza kuwa ukuaji wa Mfuko kwa Kiwango Kikubwa Katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mfuko umekuwa kwa kiasi kikubwa ambapo thamani ya Mfuko imeongezeka na kufikia shilingi trilioni 6.6 mwezi Desemba 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 39 kutoka shilingi trilioni 4.7 iliyofikiwa mwezi Machi 2021
Mkurugenzi Mkuu NSSF,Masha Mshomba akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika mkutano na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.
Related Posts:
*KABLA YA KUPAMBANA NA MCHAWI WA MAISHA YAKO BADILISHA KWANZA MIND-SET YAKO, BADILISHA KWANZA MITAZAMO YAKO YA NDANI*Biblia inasema hivi*Hosea 4:6(a) Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;*Kwenye hili andiko Mungu hasemi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWASABABU YA SHETANI AU WACHAWI , isipokuwa anasema hivi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KU… Read More
MITAA ISIYO NA UMEME IFIKAPO DESEMBA 2022 IWE IMESAMBAZIWA UMEME Imeelezwa kuwa, Mitaa 28 ambayo bado haina umeme katika Jimbo la Handeni mjini ipo katika mpango wa kupatiwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini… Read More
MKUU WA MKOA DODOMA AMEWATAKA WAAJIRI KUBAINI MBINU ZA KUPUNGUZA AJARI MAENEO YA KAZI Na Moren Rojas DodomaMkuu wa mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE amewataka waajiri kubaini mbinu za kupunguza ajali kwa wafanyakazi ili kupunguza ajali kazini.Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo kwa Madaktari juu ya ta… Read More
EURO BILIONI 10.1 ZATUMIKA MRADI UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA TANZANI.Na. Kadala Komba Dodoma Kilimo ni sekta inayotegemewa sana Tanzania kwa ajili ya kutoa malighafi kwa ajili ya taifa letu.Tarehe 16 mwaka 2021 mwezi wa 2 Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba wa kuteke… Read More
VIONGOZI WA UVCCM BAHI WAMEONYWA KUTOBWETEKA Na Peter Mkwavila BAHI. VIONGOZI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) wa wilayani Bahi,wameonywa kutobweteka na kulewa na madaraka,badala yake wafanye kazi za kujiingizia kipato pamoja na kukisaidia chama cha Mapinduz… Read More
0 Comments:
Post a Comment