Home »
» KITABU HIKI HAKIKOSOI IMANI YOYOTE
KITABU HIKI HAKIKOSOI IMANI YOYOTE
Na. Kadala Komba Dodoma
Watanzania nataka mnielewe hiki kitabu hakipingi Imani ya Kristo au Dhehebu lolote bali inasaidia kunyoosha Tafsiri na kumpa utukufu mwingi anaostahili Bwana wa Kanisa la Kristo hapa Duniani , ambaye ni mwanzo na mtimilizaji wa Imani Bwana Yesu Kristo.
Hayo yamebainishwa na Derek Murusuri Mwandishi wa Vitabu wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha HIDDEN TRUTH ABOUT LORD JESUS CHRIST Jijini Dodoma amesema Maandiko katika kitabu hiki hakikosoi Imani ya Kristo au Dhehebu lolote lile.
"Kitabu hiki kinatoa mchango wake kwa unyenyekevu , wa kumfunua Baba ni nani kinabainisha baadhi ya mafungu ya Biblia yanayomfunua na kumthibitisha muumbaji wa Mbingu na nchi, Ambaye pia Ndiye Baba Mungu , Anayekuja kitambulishwa katika Agano jipya kuwa muumbaji wa vitu vyote vilivyopo Mbinguni na Duniani, Niyule Aliye kuja kwetu kama Mwana na Ndiye Yesu Kristo"
Pia Mwandishi Murusuri amesikitishwa na kitendo Alichokifanya Mchungaji wa Dhehebu ninaro Abudu pale Dares Saam kuzuia kitabu hiki kisiuzwe kanisani hapo, kwa sababu kwenye kitabu hicho kuna sehemu nimeandika Bwana Yesu Kristo ndiyo Mungu Mwenyewe Alisema katika Ulimwengu Huu ambao umejawa na Imani kwamba Yupo Baba, Mwana pamoja na Roho Mtakatifu" kitabu kinakuja na Kusema Yule Mwana Ndiye Baba, watu hawaamini wanahisi napotosha.
Aidha Mwandishi Murusuri Kitabu hiki ni Zawadi kwa watoto wa Mungu, Wenye tamanio na Tashwishwi ya kumfahamu Mungu, wanao mfikiria Bwana Mungu Usiku na Mchana wakitaka kumjua vizuri zaidi ili wampatie Utukufu unaostahili .
"Vitabu vya ISAYA,Yohana,Wakolosai,Tito, Ufunuo na Mwanzo, vinatoa ushahidi usio na chembe ya shaka kuwa muumbaji wa vitu vyote vya Mbinguni na Duniani ni Yesu ambaye alikuwa alikuja kwetu kama Mwana na Ndiye aliyetamkwa na Musa kama Mungu muumbaji wa Mbingu na Dunia katika Mwanzo.
Sambamba mwandishi Murusuri alitumia nafasi hiyo Kumshukuru sana Mungu kwa kumsaidia kutimiza Ndoto ya kuandika kitabu hicho , kwani hili ni ombi lake la Muda mrefu akiomba kumjua Yesu Kristo na sasa amejifunua kwake kupitia Maandiko matakatifu nakuchukua hatu ya kuandika kitabu hiki cha Hidden Truth About Lord Jesus Christ, kikiwa ni kitabu chake cha pili kitabu cha kwanza kinaitwa MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY
Media, Culture and Development pia kipo Mtaani kinafanya vizuri Alisema kwenye Soko .
Derek Murusuri Mwandishi wa Vitabu wakati Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma
Derek Murusuri Mwandishi wa Vitabu pamoja na Waandishi wa Habari
My Son, Kaitira Derek Murusuri, in a cultural attire, sharing the Hidden Truth about Lord Jesus Christ book by Derek Murusuri in the United States as he also promotes his motherland in a foreign land by taking folks to Tanzania, the land of unforgettable experiences for a minute. To God be the glory.
Related Posts:
*KABLA YA KUPAMBANA NA MCHAWI WA MAISHA YAKO BADILISHA KWANZA MIND-SET YAKO, BADILISHA KWANZA MITAZAMO YAKO YA NDANI*Biblia inasema hivi*Hosea 4:6(a) Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;*Kwenye hili andiko Mungu hasemi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWASABABU YA SHETANI AU WACHAWI , isipokuwa anasema hivi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KU… Read More
*DKT. KIRUSWA AIAGIZA GST NA STAMICO KUFANYA TAFITI ZA MADINI MUFINDI NA KILOMBERO* Na. Mwandishi wetu Dodoma Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kufanya tafiti za madin… Read More
MITAA ISIYO NA UMEME IFIKAPO DESEMBA 2022 IWE IMESAMBAZIWA UMEME Imeelezwa kuwa, Mitaa 28 ambayo bado haina umeme katika Jimbo la Handeni mjini ipo katika mpango wa kupatiwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini… Read More
EURO BILIONI 10.1 ZATUMIKA MRADI UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA TANZANI.Na. Kadala Komba Dodoma Kilimo ni sekta inayotegemewa sana Tanzania kwa ajili ya kutoa malighafi kwa ajili ya taifa letu.Tarehe 16 mwaka 2021 mwezi wa 2 Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba wa kuteke… Read More
GLOBAL FUND YAUNGA MKONO SERIKALI KUKABILIANA NA MAGONJWA NCHINI.Na mwandishi wetu- DodomaKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kupiga Vita UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND) B… Read More
0 Comments:
Post a Comment