Home »
» MKATABA UJENZI MRADI WA MAJI CHANZO CHA MTO KIWIRA WASAINIWA MBEYA
MKATABA UJENZI MRADI WA MAJI CHANZO CHA MTO KIWIRA WASAINIWA MBEYA
Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya-UWSSA) imesaini mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 117.5 na mkandarasi kampuni ya China Railway Construction Engeneering Group kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka chanzo cha maji cha mto Kiwira. Mradi huo unatarajia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika jiji la Mbeya kutoka lita milioni 66.5 zinazozalishwa kwa siku hadi lita milioni 184 kwa siku.
Akizungumza jijini Mbeya katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema fedha zote za utekelezaji wa mradi huo zimetolewa na serikali. Amesema Wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha fursa ya vyanzo vya uhakika vya maji inatumika kuondoa changamoto ya majisafi sehemu mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Ujenzi na Ufuatiliaji Miradi Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema awamu ya kwanza ya utekekezaji wa mradi huo itakamilika katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Februari 25 mwaka huu hadi Februari 24, 2025.
Naye Mbunge wa Mkoa wa Mbeya kupitia Viti Maalum Wanawake Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wa Mbeya wanapata maji ya uhakika kupitia chanzo hicho.
Amewahakikishia wananchi wa mbeya kuwa serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia ni sikivu, itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili akinamama wa Mbeya waondokane na changamoto ya huduma ya majisafi na salama.
Related Posts:
MWAROBAINI WA VITENDO VYA UKATILI NA USHOGA UMEPATIKANA ASKOFU MALEKANA Na. Kadala Komba DodomaMwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana Amesema tunaamini taifa la leo na kanisa la leo limejengwa juu ya Watoto tusipofanya bidii kuwatahadharish… Read More
ZAIDI YA BILIONI 11 ZIMELIPWA KAMA KIFUATA JASHO NA MACHOZI Na. Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma.Serikali imelipa kiasi cha shilingi bilioni 11,085,850,400 kama kifuta jasho na kifuta machozi kuanzia Mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Machi, 2024, kwa wananchi waliothirika na changam… Read More
TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI … Read More
NDUGAI AMEFIKA SHULE YA BAHI MISHENI KUWAPONGEZA WALIMU NA WANAFUNZI Na. Kadala Komba Bahi Spika wa bunge mstafu Job Ndugai akiwasalimia wazazi na walimu wa kijiji cha Bahi sokoni SPIKA WA BUNGE MSTAFU JOB NDUGAI SAMBAMBA NA MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. ROSEMARY SENYAMULE WAMETEMBELE… Read More
*TOFAUTI ZA DINI, SIASA ZISIWAGAWE WATANZANIA - DKT. BITEKO*📌 Awataka waumini kushirikiana na Askofu Pangani📌Serikali kuendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini📌 Rais Samia apewa tuzo kwa uongozi uliotukuka na kulinda amani*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*N… Read More
0 Comments:
Post a Comment