Home »
» BENG'I:WANANCHI KOPENI FEDHA KWA MALENGO
BENG'I:WANANCHI KOPENI FEDHA KWA MALENGO
Na Johndickson Gaudin
Katibu mtendaji Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa amewaomba wananchi kuacha kukopa fedha bila malengo badala yake watumie mikopo kama fursa ambazo zitawasaidia kupiga Hatua kimaendelea tofauti na watu wengi ambao wanatumia mikopo pasipo kujua malengo ya mikopo hiyo Jambo ambalo linapekea kushindwa kurejesha mikopo hasa wakina mama ambao wengi wao wanatumia mikopo kununua vitu vya ndani ambavyo havina Uwezo wa kudharisha mapato zaidi.
Hayo ameyasema Leo February 14,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ,Issa amesema kupitia Baraza la Uwezeshaji wananch kiuchumi wameunda njia Mbalimbali ambazo zitawasaidia wananch kunufaika na Baraza Hilo la kuwezesha wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko ya mikopo ya jamii ambayo kwasasa kuna jumla ya mifuko 72 ili kuwanufaisha wanchi wote walio Katika mifuko hiyo ya jamii.
"Baraza linafanya kazi kwa kufuata na kusimamia sera ya Taifa ya Uwezeshaji yenye nguzo mbalimbali ambazo ni Ardhi ,Mitaji,Ushirika,Ubinafsishaji,Masoko,Ujuzi NEEC ndio chombo pekee kinachosimamia Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local Content) hapa nchini,"amesema
Pia amesema Baraza Hilo linashughulikia miundombinu ikiwemo Barabara,Biashara,umeme kwani vitu hivyo kama umeme kwasasa ni muhimu Sana Kwa Dunia ya sasa kwasababu kwasasa watu wengi wanatumia umeme kwaajili ya kuendesha shughuli zao kama Biashara hivyo wao kama secta ya Baraza la Uwezeshaji wananch kiuchumi waendelea kusimamia secta hizo ili Kila mmoja anufaike na Baraza Hilo.
"NEEC inasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme) hapa wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa,NEEC hadi sasa imewezesha kuwapatia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini, inasimamia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoa yote 26, na Halmashauri zote nchini,"amesema.
Amesema watanzania zaidi ya 83,000 wamepata ajira ya kimkakati na Hadi sasa imewezesha kuwapatia Bilioni 3.5 wenye viwanda vya Kati na vidogo Katika miradi 62 Kwenye Mikoa 12 nchin Tanzania na pia amesema Baraza huandaa makongamano kwaajili ya maonesho Kwa lengo la kuendelea kutoa elimu.
0 Comments:
Post a Comment