Home »
» MPYA YAIBUKA AJALI YA BAHI MUME WA MAREHEMU AMEFUNGUKA CHANZO
MPYA YAIBUKA AJALI YA BAHI MUME WA MAREHEMU AMEFUNGUKA CHANZO
Na. Kadala Komba Dodoma
Mkazi wa Kijiji cha Bahi sokoni, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Mage Noni(46), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Dodoma-Singida.
Ajali hiyo imetokea leo Februari 12, 2023 majira ya asubuhi ambapo gari lenye namba za usajili T 466 DUF lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Singida liliacha njia na kumgonga Mkazi huyo na kufariki papo hapo.
Mume wa Mage, anayefahamika kwa jina la Juma Mbaso, amethibitisha kifo cha mke wake na kueleza kuwa alikuwa anakwenda shambani lakini akiwa pembezoni mwa barabara gari hilo iliacha njia na kumgonga.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Edwadi Sandai, amesema kuna dereva wa gari iliyokuwa nyuma ya gari lililomgonga Mage ambaye alikuwa kwenye mwendo na tairi lilipasuka hali iliyosababisha afunge breki na kugonga gari hiyo ikahama njia na kusababisha kifo hicho.
“Hili eneo ambalo ajali imetokea ni makazi ya watu lakini magari yanapita kasi sana japo kuna kibao kinaonesha mwendo wa kupita magari ni spidi 50 lakini dereva alikuwa zaidi ya huo mwendo,"amesema.
Taarifa zaidi zitakujia kuhusu ajali hii baada ya kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Related Posts:
SAKATA LA BANDARI MSUKUMA AWATOA HOFU WATANZANIA. Na Moreen Rojas,Dodoma.Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amewatoa hofu watanzania kuhusiana na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya viongozi wa siasa kuhusu mkataba wa bandari unaotarajiwa kupiti… Read More
SERIKALI YAWATAKA WAFUGAJI WA KUKU KIJISAJILISerikali kupitia Bodi ya Nyama Tanzania imetoa rai kwa wafugaji wa kuku wa nyama Tanzania kujisajili kwenye Bodi hiyo ili kutambulika na kurasimisha biashara ili waweze kupata fursa mbalimbali.Hayo yamesemwa na Bi. Afsa… Read More
TANZANIA, UINGEREZA KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA Na WMJJWM, DodomaSerikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekubaliana na Kamisheni ya Uingereza kushirikiana ili kuimarisha usawa wa kijinsia nchini.Hayo yamebainika wakati wa k… Read More
SENYAMULE ATETA NA WAFANYABIASHARA Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekutana na wafanyabiashara wa Mkoa wake kwa lengo la kujadili changamoto za biashara kwa ujumla na kuweka maazimio yenye tija katika kukuza masoko kwa kutumia fursa zilizopo… Read More
MEJA JENERALI MBUGE “TUIMARISHE USHIRIKIANO KUKABILI MAJANGA”Na Mwandishi wetu- SingidaSerikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta mbalimbali katika kukabiliana na maafa ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira sa… Read More
0 Comments:
Post a Comment