Home »
» MLIPUKO WA INJILI WAZINDULIWA DODOMA
MLIPUKO WA INJILI WAZINDULIWA DODOMA
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Waumini wa dini ya Kikristo nchini wamehimizwa kushiriki katika kazi ya Mungu ya kueneza injili Ulimwenguni kote ili watu wamjue Mungu na kubadilisha mienendo yao mibaya pamoja na kuwa na jamiii yenye maadili mema.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Jimbo la Kati mwa Tanzania (CTF) Mchungaji Festo Mng’ong’o kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato wakati akizindua programu ya Mlipuko wa Uinjilisti ambayo imeanza Februari 11 mwaka 2023 katika Kanisa la Chang’ombe SDA inayolenga kila muumini kuleta mshiriki mpya kanisani hadi ifikapo 2025.
Amesema kila muumini ana wajibu wa kufanya kazi ya Mungu kulingana na talanta aliyopewa ili kuvuta watu wengi kufahamu Mungu na kurekebisha tabia zisizo njema.
“Haya ni maandalizi ya wakazi wa Dunia kumlaki Yesu anapokuja kwa sababu ishara zote , matukio yanayotokea yanaonyesha kwamba Dunia imefikia mwisho hivyo wito wa Mungu ni kila jamaa, kabila afikiwe na ujumbe huu na kanisa limejipanga kufanikisha hilo,”Amesema Mchungaji Mng’ong’o.
Naye Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Miyuji, Lameck Barinda ameahidi kuhamisha waumini katika kanisa lake kuhakikisha kila muumini anafanya sehemu yake kwa kufundisha watu wengine habari njema wakati wa kujiandaa kumpokea Yesu anapokuja mara ya pili.
“Kanisa la Miyuji tumejipanga kufanya ushuhudiaji nyumba kwa nyumba na tuna mpango wa kufanya mikutano mitatu ya injili kwa mwaka huu,”Ameeleza Barinda.
Kwa upande wake Paul Samson ambaye ni Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe akaeleza kuwa kama viongozi wa kanisa hilo ni kuwajibika kuwaleta watu kwa Yesu huku akiwasihi waumini kujihusisha kila mmoja kwa wakati wake kufanya kazi ya Mungu.
“Viongozi tumejipanga kuwatembelea waumini walioyumba kiimani na tunawatia moyo wumini kila mmoja mahali alipo iwe ni kazini, maeneo ya biashara au nyumbani kazi kubwa ni kuwaongoza watu kumjua MUngu,”Amefafanua Mzee Paul.
Aidha Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Veyula, Benjamin Yonathan akabainisha kuwa kanisa limejipanga kufanya mikutano miwili ya injili itakayohusisha wakazi wote wa maeneo hayo kwa pamoja kujifunza neno la Mungu.
“Naamini ndilo kusudi tuliloitiwa na Mungu kueneza injili, tunaamini kazi yake itakwenda mbele na ushindi utapatikana kwa kila kundi watoto, wanakwaya, wanawake, vijana pamoja na wenye ulemavu,”Amesema Mzee Yonathan.
Programu hiyo ya Mlipuko wa Uinjilisti imeanza rasmi Februari 11 mwaka 2023 hadi kufikia 2025 ikiwa na kauli mbiu isemayo “ Jihusishe Yesu Anakuja”
Katibu wa Jimbo la Kati mwa Tanzania (CTF) Mchungaji Festo Mng’ong’o kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya Mlipuko wa Uinjilisti katika Kanisa la Chang’ombe Februari 11, 2023 Jijini Dodoma.
Related Posts:
WANAHABARI NA WATUMISHI WAMEJERUHIWA HIFADHI YA NGORONGORO … Read More
SERIKALI IMETOA SHILINGI TRILLIONI 1.7 KWA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI(REA). Na Moreen Rojas,Dodoma.Serikali imetoa jumla ya shilingi trillioni 1.7 kwa Wakala wa Nishati Vijiini (REA)kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati nchini.Aidha Serikali imetoa billion 12 kwa ajili y… Read More
DKT. YONAZI: SEKTA YA KILIMO KUCHAGIZA PATO LA TAIFA. Na. Mwandishi Wetu -Dar es Salaam Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini kwa kuzingatia umuhimu na tija ya sekta hiyo katika maendeleo ya Taifa. Kauli hiyo imetolewa … Read More
WAKULIMA WATUMIA FURSA KUJIFUNZA MBINU ZA KILIMO CHA KISASA SIKU YA MKULIMA SHAMBANI ARUSHAMATUKIO YA PICHA 18 AUGUST 2023 SIKU YA MKULIMA MKOANI ARUSHA KIJIJI CHA OLDONYONG’RO KINGORI. Na. Mwandishi wetu Arusha Zana Bora za Kisasa katika Kilimo ya Mtama na Karanga &nb… Read More
𝗩𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗔𝗦𝗜𝗦𝗜 𝗭𝗔 𝗨𝗠𝗠𝗔 𝗪𝗔𝗘𝗟𝗘𝗭𝗔 𝗙𝗔𝗜𝗗𝗔 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗕𝗔𝗗𝗜𝗟𝗜𝗦𝗛𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗔𝗔𝗥𝗜𝗙𝗔 𝗞𝗜𝗗𝗜𝗝𝗜𝗧𝗔𝗟𝗜 𝗞𝗨𝗣𝗜𝗧𝗜𝗔 𝗠𝗙𝗨𝗠𝗢 𝗪𝗔 𝗚𝗼𝗩𝗘𝗦𝗕 Viongozi wa taasisi mbalimbali za umma wameeleza faida za kubadilishana taarifa kidijitali kupitia Mfumo wa pamoja wa ubadilishanaji taarifa serikalini ujulikanao kama ‘Government Enterprises Service Bus’ (GovESB).Wakiz… Read More
0 Comments:
Post a Comment