Home »
» BALAA MCHUNGAJI ATINGA MADHABAHUNI NA BUNDUKI
BALAA MCHUNGAJI ATINGA MADHABAHUNI NA BUNDUKI
Mchungaji wa Kanisa la House on the Rock, Uche Aigbe ametiwa mbaroni na jeshi la polisi nchini Nigeria kwa kosa la kubeba bunduki aina ya AK-47 wakati wa mahubiri ya Jumapili wakati akitoa mahubiri kuhusu "silaha za kiroho".
Jeshi la polisi limethibitisha kumshikilia mchungaji huyo na ofisa mmoja wa polisi ambaye ndiye mmiliki wa bunduki hiyo.
Kwa mujibu wa kanisa lake, mchungaji Uche Aigbe awali aliomba msamaha kwa tukio hilo.
"Anatambua kwamba hata kwa nia nzuri, kubeba bunduki kuelezea ujumbe wake hairuhusiwi na ameonyesha kujutia kosa hilo," ujumbe wa Kanisa la House on the Rock liliandika katika taarifa yake iliyotoa kufuatia tukio la mchungaji huyo kuingia madhabahuni na bunduki.
Kanisa limeongeza kuwa linapinga aina zote za vurugu na linashirikiana kikamilifu na mamlaka wanapofanya uchunguzi wao kuhusu tukio hilo.
Sheria nchini Nigeria mtu yeyote haruhusiwi kubeba bunduki bila kupewa leseni na Inspekta Jenerali wa Polisi.
Related Posts:
SAKATA LA BANDARI MSUKUMA AWATOA HOFU WATANZANIA. Na Moreen Rojas,Dodoma.Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amewatoa hofu watanzania kuhusiana na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya viongozi wa siasa kuhusu mkataba wa bandari unaotarajiwa kupiti… Read More
UCHUNGUZI WA KIIKOLOJIA KUHUSU UGONJWA WA VIRUSI VYA MARBURG WAANZA KAGERA. Na Mwandishi wetu - KageraWataalam kutoka Wizara za kisekta chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza uchunguzi wa Kiikolojia kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Marburg baada ya ugonjwa huo kutokomezwa Nchini.&n… Read More
MEJA JENERALI MBUGE “TUIMARISHE USHIRIKIANO KUKABILI MAJANGA”Na Mwandishi wetu- SingidaSerikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta mbalimbali katika kukabiliana na maafa ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira sa… Read More
SERIKALI YAWATAKA WAFUGAJI WA KUKU KIJISAJILISerikali kupitia Bodi ya Nyama Tanzania imetoa rai kwa wafugaji wa kuku wa nyama Tanzania kujisajili kwenye Bodi hiyo ili kutambulika na kurasimisha biashara ili waweze kupata fursa mbalimbali.Hayo yamesemwa na Bi. Afsa… Read More
SENYAMULE ATETA NA WAFANYABIASHARA Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekutana na wafanyabiashara wa Mkoa wake kwa lengo la kujadili changamoto za biashara kwa ujumla na kuweka maazimio yenye tija katika kukuza masoko kwa kutumia fursa zilizopo… Read More
0 Comments:
Post a Comment