Home »
» DK.SWEKE: BAHARI KUU IPO SALAMA TUNATUMIA NDEGE KUFANYA DORIA
DK.SWEKE: BAHARI KUU IPO SALAMA TUNATUMIA NDEGE KUFANYA DORIA
Na. Kadala Komba Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,ameeleza kuwa katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kufuatilia meli ndani ya maji na kutumia doria za ndege kwa ajili ya kuangalia kinachofanyika.
Hayo ameyasema leo Februari 8,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shuguli mbalimbali za Mamlaka hiyo.
Dk. Sweke, amesema Mamlaka hiyo ina jukumu la kutoa leseni kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu kwa meli za ndani na nje pamoja na kulinda,kusimamia na kuratibu shughuli zote za uvuvi wa bahari kuu.
Amesema kuwa makusanyo hayo yamevunja rekodi iliyowekwa na Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka saba iliyopita.
“Makusanyo makubwa ya mwisho yalikuwa ni Sh. bilioni 4 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 lakini yalishuka sana baada ya kuletwa kwa kanuni ambayo ilikuwa inawataka wavuvi kutoa muraba wa dora 0.4 kwa kila kilo moja ya samaki.
“Hali hii ilisababisha makusanyo kushuka sana kutokana na meli nyingi za uvuvi kukimbia na kuacha kufanya uvuvi katika nchi yetu lakini kutokana na hali hiyo tulijifungia na kuondoa kanuni hiyo na sasa matunda yanaonekana kwa kupanda kiasi cha ukusanyaji wa mapato yatokano na utoaji wa leseni za uvuvi na huduma nyingine zinazotolewa na mamlaka hii”amesema Dk. Sweke
“Mifumo hii tunayotumia sasa pamoja na kufanya doria kwa kutumia ndege zimesaidia sana kukomesha vitendo vya uvuvi harafu bahari kuu”amesema Dk. Sweke
Hata hivyo amesema toka Mamlaka kuanzishwa imefanikiwa kukamata meli moja iliyokuwa na samaki tani 100 ya samaki wasiolengwa.
Aidha kipindi cha mwezi Julai 2022, hadi Februari mwaka huu Mamlaka hiyo imekusanya Sh.bilioni 4.1 ikiwa ni mapato yatokanayo na utoaji wa leseni kwa ajili ya meli za uvuvi na huduma nyingine.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8,2023 jijini Dodoma
WAANDISHI wa habari wakati wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,
Related Posts:
RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA SENSA NA MUONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO HAYO JIJINI DODOMANa. Kadala Komba Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo … Read More
NAIBU WAZIRI MERYPRICA MAHUNDI AMETOA OYO KALI KWA WALE WANAOCHEPUSHA MAJI Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na wanan… Read More
UCHIMBAJI MAKAA YA MAWE KULETA TIJA KWA WATANZANIANaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa amebainisha kuwa, biashara ya Makaa ya Mawe inatarajia kuleta tija kwa Watanzania kutokana na uhitaji mkubwa wa madini hayo ndani na nje ya nchi. Dkt. Kiruswa ameeleza hayo Novemba… Read More
WAZIRI SIMBACHAWENE, AMPONGEZA MAMA TUNU PINDANa Mwandishi wetu Kuimba kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuewa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa. Kauli hiyo imetolewa na W… Read More
TANROADS YATUMIA SHILINGI TRILIONI 1.37 KUKAMILISHA MIRADI 14 KWA KIPINDI CHA SERIKALI AWAMU YA SITA.Na Moreen Rojas, Dodoma Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema imefanikiwa kukamilisha jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 katika kipindi cha awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania … Read More
0 Comments:
Post a Comment