Home »
» TAASISI YA KUMBUMBU YA MWALI NYERERE IMEKUJA NA MIKAKATI HII
TAASISI YA KUMBUMBU YA MWALI NYERERE IMEKUJA NA MIKAKATI HII
Na Sifa Lubasi Dodoma
TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Dodoma imeweka mkakati wa kuanzisha kituo cha utamaduni kwa ajili ya kukusanya na kufanya shughuli za kiutamaduni
Taasisi hiyo kwa mkoa wa Dodoma inaongozwa na Mwenyekiti wa taasisi Mkoa Peter Mavunde na Katibu wa taasisi Mkoa ni Anamringi Macha ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara.
Àkizungumza wakati wa kikao juzi, Katibu wa Mkoa Anamringi Macha alisema miongoni mwa mikakati ni kuanzisha kituo cha utamaduni kwa ajili ya kukusanya na kufanya shughuli za kiutamaduni na hivyo kuwezesha kituo hicho kuwa na kitega uchumi.
Alitaja mikakati mingine ni kubuni, kuandaa na kutekeleza mipango mikakati ya kuinua mapato ya Taasisi ikiwemo ada ya uanachama, ada ya kila mwezi na maandiko ya mradi ya muda mrefu na mfupi.
Katika hatua nyingine, wajumbe wametumia nafasi hiyo kumpongeza Anamringi Macha aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara na kumtakia utekelezaji mwema wa majukumu aliyokabidhiwa na chama tawala
Katika kikao hicho wajumbe pia walipokea taarifa kutoka makao makuu ya taasisi ya kumteua Peter Mavunde kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi Taifa, huku Rehema Omary Hamis akichaguliwa na wajumbe hao kuwa mtunza hazina wa Mkoa.
mwisho.
0 Comments:
Post a Comment