Home »
» TBA YAISHUKURU SERIKALI KUIWEZESHA KUKAMILISHA MIRADI YA KIMKAKATI.
TBA YAISHUKURU SERIKALI KUIWEZESHA KUKAMILISHA MIRADI YA KIMKAKATI.
Na Johndickson Gaudin
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)kupitia serikali ya awamu ya sita wameendelea kutekeleza majukumu ya miradi ya kimikakati kupitia Fedha zilizo tolewa katika bajeti ya mwà ka 2021_2022 na 2022_2023 ikiwa nipamoja na kukamilisha miradi mbalimbali ikijumuidha miradi iliyo kamilika ikiwa ni zaidi ya miradi 8.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa (TBA) Daud Kondoro wakati akizungumza na wandishi wa habari leo Februari 14,2023 Jijini Dodoma, kuhusu utekelezaji wa majukumu wa wakala hao katika kipindi cha miaka miwili.
Kondoro amesema miradi iliyotekelezwa katika kipindi husika kuwa ni mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Dodoma,ujenzi wanyumba 20 za viongozi jijini Dodomapamoja na ukarabati wa nyumba za watumishi wa umma ulio garimu takribani billion 7.8
“Naishukuru sana serikali ya Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuiwezesha TBA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni Pamoja na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali. katika kipindi cha miezi 18, tayari imetoa sh. bilioni 54.2 ajili ya utekelezaji wa miradi.
“Mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi jijini Dodoma ambao umegharimu sh.bilioni tisa mradi huu ulitekelezwa ili kukabiliana na uhaba wa nyumba za makazi ya viongozi uliojitokeza mara baada ya serikali kuhamia Dodoma ,”amesema Kondoro .
Mtendaji huyo amesema serikali imeshatoa sh.bilioni 15.5 kwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 150 ambao umefikia asilimia 81 na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 150 za awamu ya pili ukiwa umefikia asilimia tatu.
Ametaja mradi mwingine kuwa ni ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma katika eneo la magomeni kota, awamu ya kwanza na ya pili ambao unagharimu sh.bilioni 7.8 ambapo ujenzi wa jengo la ghorofa nane lenye uwezo wa kuchukua familia 16 tayari limeshakamilika kwa asilimia 99.
0 Comments:
Post a Comment