Home »
» MAMA AFARIKI AKIFANYIWA MAOMBI KANISANI
MAMA AFARIKI AKIFANYIWA MAOMBI KANISANI
Polisi nchini Uganda wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 59 Rosette Najjuma -ameaga dunia akiwa kanisani jijini Kampala.
Kwa mujibu wa naibu msemaji wa polisi wa Kampala Luke Owoyesigyire, Najjuma alizirai na kufariki ibada ikiendelea katika kanisa la Christian Life katika Parokia ya Makerere III mnamo Jumatano - Februari 8,2023.
Mwanamke huyo anaripotiwa kufanyiwa vipimo kadhaa katika Hospitali ya Mulago kwa muda wa miaka mitatu iliyopita lakini hakuna ugonjwa uliopatikana.
Jamaa zake waliamua kumtafutia msaada wa kanisani na hivyo kumpeleka katika kanisa la Pasta Jackson Ssenyonga.
Mwanamke huyo alizirai akifanyiwa maombi mwendo wa saa kumi alfajiri na kuaga dunia kabla ya kufanyiwa msaada wowote wa kimatibabu.
Owoyesigyire alisema kuwa mwili wake ulihamishiwa makafani ya Mulago ukisubiri kufanyiwa upasuaji.
Related Posts:
MAJALIWA : ONGEZENI USHIRIKI WA WAHANDISI WAZAWA KWENYE UJENZI MIRADI Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha wahandisi wazawa wanashiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali nchini. Amesema kuwa … Read More
DKT. BITEKO AWASIHI WAFANYABIASHARA WA PETROL NA DIZELI KUWA WAAMINIFU. Na Timotheo Mathayo, Dar es Salaam.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasihi Wafanyabiashara wa mafuta ya dizeli na Petroli nchini kuwa waaminifu wakati wakiendelea kutoa huduma kwa Watanza… Read More
*TANESCO, Watanzania wanataka Umeme- Dkt. Biteko.**Na Grace Semfuko, MAELEZO na Dorina Makaya Wizara ya Nishati - Dar es Salaam*Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema watanzania wanataka umeme na hivyo kuwataka Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika… Read More
WADAU WA MALEZI YA WATOTO WAKUTANA KUBORESHA MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO Wadau wanaoshughulika na malezi na makuzi ya watoto wametakiwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya Programu Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT -MMMAM) ili kupunguza udumavu na utapiamlo kw… Read More
NAIBU WAZIRI KAPINGA AIHIMIZA TANESCO KUBORESHA UPATIKANAJI UMEME MTWARA NA LINDI Naibu Waziri Kapinga amelihimiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania - TANESCO kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wa kutosha.Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo leo tarehe 14/0… Read More
0 Comments:
Post a Comment