Subscribe Us

ASKOFU MWAKIPESILE AKABIDHIWA GARI LA UTUMISHI

Na Johndickson Gaudin,Dodoma Wakati Tanzania na Dunia ikiazimisha siku ya wanawake duniani kama ilivyo tamaduni ulimwenguni kote siku ambayo huadhimishwa kila ifikapo machi 8 ya kila mwaka ,Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT Brown Mwakipesile ameeleza mchango wa wanawake katika jamii na kanisa kwa ujumla ambapo amesema kama nchi upo mfano mzuri wa kuutazama kupitia Rais Dkt Samia Suluh Hassan ambaye amekuwa mfano mzuri kwa wanawake wengine nchini. Ameyasema hayo katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya hafra fupi ya kumkabidhi Askofu huyo Gari kwaajili ya kazi ya kanisa iliyo fanyika Jijini Dodoma hii leo machi 8 2023 katika uwanja wa Makao Makuu ya EAGT. Aidha amewakumbusha wanawake wote nchini kujali malezi ya watoto na kuacha tabia yakuwaruruhusu watoto kuzurura na kushidwa kujua watoto wanafanya nini kwa wakati gani “Wanamke inabidi watambue wajibu wao wa kulea kwakuwa wao ndiyo wanajua uchungu wa mtoto kwamaana wana beba mimba miezi tisa atukatai kuwepo kwa majukumu lakini yasipitilize kiasi cha kuwasahau watoto . Kile kinachokuwa chema kinakuwa na mipaka yake lazima tuwe na mipangilio ya maisha yetu tujue tunacho paswa kufanya tusiwe kawa wanyama ambao wanaweza kufanya kila kiytu”, amesema. Katika hatua nyingine Askofu huyo amesema wao kama kanisa wanaendelea kuubili na kufundisha neno la mungu ili mwanadamu abaki kumuheshimu mungu na kutambua wajibu wake kwaajili ya kumtumikia mungu.
Gari alilokabithiwa Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT Brown Mwakipesile na Kanisa kwenye ofisi za EAGT Kisasa Meriwa
Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT Brown Mwakipesile Akizungumza na Waandishi wa habari namna alivyo pokea Zawadi ya Gari
Viongozi pamoja na wachungaji wa kanisa la EAGT Wakikabithi Gari Askofu Brown Mwakipesile

0 Comments:

Post a Comment