Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI IMEZINDULIWA KATA YA MPAMANTWA WILAYA YA BAHI

Na. Kadala Komba Bahi Mkuu wa Takukuru Halmashauri Wilaya ya Bahi Erick Kilawe Amesema hii Programu ya TAKUKURU RAFIKI imeanzishwa Maalumu hili kutoa fursa kwa kila Mtanzania kushirikiana na Serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo ni kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Hayo yamejili Jijini Dodoma Wilaya ya Bahi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Takukuru Rafiki ikizinduliwa kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Wilaya na kata amesema Programu hii inaakisi maana ya rafiki kwa kubeba dhana ya kuwa karibu na ushirikiano wa dhati na karibu na kila mwananchina wadau kwa itatekelezwa kwa kuwa na vikao katika ngazi ya kata kwa lengo la kutambua kero zilizopo kwenye utoaji au upokeaji wa huduma kama za Afya au Elimu pamoja na mchakato wa kutekeleza miradi ya maendeleo ujenzi wa miundombinu ya maji. Kwaupande wake Mchunguzi mkuu Takukuru Emmanuel Masawe Ametoa wito kwa Wananchi na wadau kushirikiana kuzuia vitendo vya Rushwa katika utoaji wa huduma kwa umma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Programu hii ya "TAKUKURU RAFIKI" Usikae pembeni tushirikiane katika ili kwa pamoja tunaijenge Tanzania. Aidha Mhe. Diwani kata ya mpamatwa ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuwapatia semina namna ambavyo taasisi hiyo inanyo fanaya kazi kwa karibu na wananchi katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuu wa Takukuru Halmashauri Wilaya ya Bahi Erick Kilawe
Mhe. Diwani kata ya mpamatwa
MATUKIO MBALIMBALI KWENYE PICHA YA UZINDUZI WA PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI

DHAMANI YA MAZAO CHINI YA PANDA KWA WASTANI WA 12%KWA MWAKA 2020/2021

Na Johndickson Gaudin. Bodi ya usimamizi wa stakabadhi imefanikiwa kuongeza bei ya mazao Mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ikiwa nipamoja kuongeza mapato ya wakulima na mapato ya serikali kwa wastani wa 200%huku ikiongeza kukuza huduma za fedha vijijini,kufanikisha uanzishaji wa Soko la Bidhaa Tanzania. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala (WRRB),Asangye Bangu wakati wa mkutano na waandishi wa habari Leo februari 15,2023 ambapo amesema Baada ya kuanzishwa kwa Mfumo huo mwenendo wa bei na ushalishaji ulibadilika na kuanza kuwa na mwenendo chanya. Aidha Mtendaji huyo amesema kwa upande wa uzalishaji, tokea kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2020/21 ukuaji wa uzalishaji umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa 12% kwa mwaka ukilinganisha na ukuaji wa 2% kwa mwaka kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo waStakabadhi za Ghala. "Mwaka 2021, Bodi imewezesha kuanza kutumika kwa Mfumo mkoa wa Songwe katika zao la Ufuta na Morogoro katika zao la Kakao licha ya upinzani mkubwa uliokuwa ukiletwa na wanafaika wa mifumo holela katika maeneo hayo. "Mkoa wa Morogoro kwa mara ya kwanza wakulima waliuza kakao yao kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kufanikiwa kupata bei wastani wa Shilingi 4,892.50 ongezeko hili la bei lilikuwa ni la wastani wa asilimia 244.6 kutokea wastani wa Shilingi 2,000.00 bei waliyokuwa wakipata kupitia mifumo holela.",amesema. Kwaupande mwingine mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wakulima wa kahawa mkoa wa Kagera kuhakikisha wanakuwa wazapendo katika kuuza mazao kwakuzingatua na kufata utaratibu ili kuweza kuuza zao Hilo kwa bei elekezi. Pia amewataka wanaoendesha na kusimamia maghala mikoa yote nchini kuhakikisha Wana mfumo wa CCTV camera ili kuwezesha kuona kuona kinachoendelea kwenye maghala hayo ili kuhakikisha wanafata Sheria zinazo waongoza kama taasisi.

BALAA MCHUNGAJI ATINGA MADHABAHUNI NA BUNDUKI

Mchungaji wa Kanisa la House on the Rock, Uche Aigbe ametiwa mbaroni na jeshi la polisi nchini Nigeria kwa kosa la kubeba bunduki aina ya AK-47 wakati wa mahubiri ya Jumapili wakati akitoa mahubiri kuhusu "silaha za kiroho". Jeshi la polisi limethibitisha kumshikilia mchungaji huyo na ofisa mmoja wa polisi ambaye ndiye mmiliki wa bunduki hiyo. Kwa mujibu wa kanisa lake, mchungaji Uche Aigbe awali aliomba msamaha kwa tukio hilo. "Anatambua kwamba hata kwa nia nzuri, kubeba bunduki kuelezea ujumbe wake hairuhusiwi na ameonyesha kujutia kosa hilo," ujumbe wa Kanisa la House on the Rock liliandika katika taarifa yake iliyotoa kufuatia tukio la mchungaji huyo kuingia madhabahuni na bunduki. Kanisa limeongeza kuwa linapinga aina zote za vurugu na linashirikiana kikamilifu na mamlaka wanapofanya uchunguzi wao kuhusu tukio hilo. Sheria nchini Nigeria mtu yeyote haruhusiwi kubeba bunduki bila kupewa leseni na Inspekta Jenerali wa Polisi.

BENG'I:WANANCHI KOPENI FEDHA KWA MALENGO

Na Johndickson Gaudin Katibu mtendaji Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa amewaomba wananchi kuacha kukopa fedha bila malengo badala yake watumie mikopo kama fursa ambazo zitawasaidia kupiga Hatua kimaendelea tofauti na watu wengi ambao wanatumia mikopo pasipo kujua malengo ya mikopo hiyo Jambo ambalo linapekea kushindwa kurejesha mikopo hasa wakina mama ambao wengi wao wanatumia mikopo kununua vitu vya ndani ambavyo havina Uwezo wa kudharisha mapato zaidi. Hayo ameyasema Leo February 14,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ,Issa amesema kupitia Baraza la Uwezeshaji wananch kiuchumi wameunda njia Mbalimbali ambazo zitawasaidia wananch kunufaika na Baraza Hilo la kuwezesha wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko ya mikopo ya jamii ambayo kwasasa kuna jumla ya mifuko 72 ili kuwanufaisha wanchi wote walio Katika mifuko hiyo ya jamii. "Baraza linafanya kazi kwa kufuata na kusimamia sera ya Taifa ya Uwezeshaji yenye nguzo mbalimbali ambazo ni Ardhi ,Mitaji,Ushirika,Ubinafsishaji,Masoko,Ujuzi NEEC ndio chombo pekee kinachosimamia Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local Content) hapa nchini,"amesema Pia amesema Baraza Hilo linashughulikia miundombinu ikiwemo Barabara,Biashara,umeme kwani vitu hivyo kama umeme kwasasa ni muhimu Sana Kwa Dunia ya sasa kwasababu kwasasa watu wengi wanatumia umeme kwaajili ya kuendesha shughuli zao kama Biashara hivyo wao kama secta ya Baraza la Uwezeshaji wananch kiuchumi waendelea kusimamia secta hizo ili Kila mmoja anufaike na Baraza Hilo. "NEEC inasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme) hapa wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa,NEEC hadi sasa imewezesha kuwapatia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini, inasimamia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoa yote 26, na Halmashauri zote nchini,"amesema. Amesema watanzania zaidi ya 83,000 wamepata ajira ya kimkakati na Hadi sasa imewezesha kuwapatia Bilioni 3.5 wenye viwanda vya Kati na vidogo Katika miradi 62 Kwenye Mikoa 12 nchin Tanzania na pia amesema Baraza huandaa makongamano kwaajili ya maonesho Kwa lengo la kuendelea kutoa elimu.

TBA YAISHUKURU SERIKALI KUIWEZESHA KUKAMILISHA MIRADI YA KIMKAKATI.

Na Johndickson Gaudin Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)kupitia serikali ya awamu ya sita wameendelea kutekeleza majukumu ya miradi ya kimikakati kupitia Fedha zilizo tolewa katika bajeti ya mwàka 2021_2022 na 2022_2023 ikiwa nipamoja na kukamilisha miradi mbalimbali ikijumuidha miradi iliyo kamilika ikiwa ni zaidi ya miradi 8. Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa (TBA) Daud Kondoro wakati akizungumza na wandishi wa habari leo Februari 14,2023 Jijini Dodoma, kuhusu utekelezaji wa majukumu wa wakala hao katika kipindi cha miaka miwili. Kondoro amesema miradi iliyotekelezwa katika kipindi husika kuwa ni mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Dodoma,ujenzi wanyumba 20 za viongozi jijini Dodomapamoja na ukarabati wa nyumba za watumishi wa umma ulio garimu takribani billion 7.8 “Naishukuru sana serikali ya Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuiwezesha TBA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni Pamoja na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali. katika kipindi cha miezi 18, tayari imetoa sh. bilioni 54.2 ajili ya utekelezaji wa miradi. “Mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi jijini Dodoma ambao umegharimu sh.bilioni tisa mradi huu ulitekelezwa ili kukabiliana na uhaba wa nyumba za makazi ya viongozi uliojitokeza mara baada ya serikali kuhamia Dodoma ,”amesema Kondoro . Mtendaji huyo amesema serikali imeshatoa sh.bilioni 15.5 kwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 150 ambao umefikia asilimia 81 na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 150 za awamu ya pili ukiwa umefikia asilimia tatu. Ametaja mradi mwingine kuwa ni ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma katika eneo la magomeni kota, awamu ya kwanza na ya pili ambao unagharimu sh.bilioni 7.8 ambapo ujenzi wa jengo la ghorofa nane lenye uwezo wa kuchukua familia 16 tayari limeshakamilika kwa asilimia 99.

MLIPUKO WA INJILI WAZINDULIWA DODOMA

Na Mwandishi wetu- Dodoma Waumini wa dini ya Kikristo nchini wamehimizwa kushiriki katika kazi ya Mungu ya kueneza injili Ulimwenguni kote ili watu wamjue Mungu na kubadilisha mienendo yao mibaya pamoja na kuwa na jamiii yenye maadili mema. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Jimbo la Kati mwa Tanzania (CTF) Mchungaji Festo Mng’ong’o kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato wakati akizindua programu ya Mlipuko wa Uinjilisti ambayo imeanza Februari 11 mwaka 2023 katika Kanisa la Chang’ombe SDA inayolenga kila muumini kuleta mshiriki mpya kanisani hadi ifikapo 2025. Amesema kila muumini ana wajibu wa kufanya kazi ya Mungu kulingana na talanta aliyopewa ili kuvuta watu wengi kufahamu Mungu na kurekebisha tabia zisizo njema. “Haya ni maandalizi ya wakazi wa Dunia kumlaki Yesu anapokuja kwa sababu ishara zote , matukio yanayotokea yanaonyesha kwamba Dunia imefikia mwisho hivyo wito wa Mungu ni kila jamaa, kabila afikiwe na ujumbe huu na kanisa limejipanga kufanikisha hilo,”Amesema Mchungaji Mng’ong’o. Naye Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Miyuji, Lameck Barinda ameahidi kuhamisha waumini katika kanisa lake kuhakikisha kila muumini anafanya sehemu yake kwa kufundisha watu wengine habari njema wakati wa kujiandaa kumpokea Yesu anapokuja mara ya pili. “Kanisa la Miyuji tumejipanga kufanya ushuhudiaji nyumba kwa nyumba na tuna mpango wa kufanya mikutano mitatu ya injili kwa mwaka huu,”Ameeleza Barinda. Kwa upande wake Paul Samson ambaye ni Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe akaeleza kuwa kama viongozi wa kanisa hilo ni kuwajibika kuwaleta watu kwa Yesu huku akiwasihi waumini kujihusisha kila mmoja kwa wakati wake kufanya kazi ya Mungu. “Viongozi tumejipanga kuwatembelea waumini walioyumba kiimani na tunawatia moyo wumini kila mmoja mahali alipo iwe ni kazini, maeneo ya biashara au nyumbani kazi kubwa ni kuwaongoza watu kumjua MUngu,”Amefafanua Mzee Paul. Aidha Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Veyula, Benjamin Yonathan akabainisha kuwa kanisa limejipanga kufanya mikutano miwili ya injili itakayohusisha wakazi wote wa maeneo hayo kwa pamoja kujifunza neno la Mungu. “Naamini ndilo kusudi tuliloitiwa na Mungu kueneza injili, tunaamini kazi yake itakwenda mbele na ushindi utapatikana kwa kila kundi watoto, wanakwaya, wanawake, vijana pamoja na wenye ulemavu,”Amesema Mzee Yonathan. Programu hiyo ya Mlipuko wa Uinjilisti imeanza rasmi Februari 11 mwaka 2023 hadi kufikia 2025 ikiwa na kauli mbiu isemayo “ Jihusishe Yesu Anakuja”
Katibu wa Jimbo la Kati mwa Tanzania (CTF) Mchungaji Festo Mng’ong’o kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya Mlipuko wa Uinjilisti katika Kanisa la Chang’ombe Februari 11, 2023 Jijini Dodoma.

MPYA YAIBUKA AJALI YA BAHI MUME WA MAREHEMU AMEFUNGUKA CHANZO

Na. Kadala Komba Dodoma Mkazi wa Kijiji cha Bahi sokoni, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Mage Noni(46), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Dodoma-Singida. Ajali hiyo imetokea leo Februari 12, 2023 majira ya asubuhi ambapo gari lenye namba za usajili T 466 DUF lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Singida liliacha njia na kumgonga Mkazi huyo na kufariki papo hapo. Mume wa Mage, anayefahamika kwa jina la Juma Mbaso, amethibitisha kifo cha mke wake na kueleza kuwa alikuwa anakwenda shambani lakini akiwa pembezoni mwa barabara gari hilo iliacha njia na kumgonga. Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Edwadi Sandai, amesema kuna dereva wa gari iliyokuwa nyuma ya gari lililomgonga Mage ambaye alikuwa kwenye mwendo na tairi lilipasuka hali iliyosababisha afunge breki na kugonga gari hiyo ikahama njia na kusababisha kifo hicho. “Hili eneo ambalo ajali imetokea ni makazi ya watu lakini magari yanapita kasi sana japo kuna kibao kinaonesha mwendo wa kupita magari ni spidi 50 lakini dereva alikuwa zaidi ya huo mwendo,"amesema. Taarifa zaidi zitakujia kuhusu ajali hii baada ya kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

TAASISI YA KUMBUMBU YA MWALI NYERERE IMEKUJA NA MIKAKATI HII

Na Sifa Lubasi Dodoma TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Dodoma imeweka mkakati wa kuanzisha kituo cha utamaduni kwa ajili ya kukusanya na kufanya shughuli za kiutamaduni Taasisi hiyo kwa mkoa wa Dodoma inaongozwa na Mwenyekiti wa taasisi Mkoa Peter Mavunde na Katibu wa taasisi Mkoa ni Anamringi Macha ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara. Àkizungumza wakati wa kikao juzi, Katibu wa Mkoa Anamringi Macha alisema miongoni mwa mikakati ni kuanzisha kituo cha utamaduni kwa ajili ya kukusanya na kufanya shughuli za kiutamaduni na hivyo kuwezesha kituo hicho kuwa na kitega uchumi. Alitaja mikakati mingine ni kubuni, kuandaa na kutekeleza mipango mikakati ya kuinua mapato ya Taasisi ikiwemo ada ya uanachama, ada ya kila mwezi na maandiko ya mradi ya muda mrefu na mfupi. Katika hatua nyingine, wajumbe wametumia nafasi hiyo kumpongeza Anamringi Macha aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara na kumtakia utekelezaji mwema wa majukumu aliyokabidhiwa na chama tawala Katika kikao hicho wajumbe pia walipokea taarifa kutoka makao makuu ya taasisi ya kumteua Peter Mavunde kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi Taifa, huku Rehema Omary Hamis akichaguliwa na wajumbe hao kuwa mtunza hazina wa Mkoa. mwisho.

KITABU HIKI HAKIKOSOI IMANI YOYOTE

Na. Kadala Komba Dodoma Watanzania nataka mnielewe hiki kitabu hakipingi Imani ya Kristo au Dhehebu lolote bali inasaidia kunyoosha Tafsiri na kumpa utukufu mwingi anaostahili Bwana wa Kanisa la Kristo hapa Duniani , ambaye ni mwanzo na mtimilizaji wa Imani Bwana Yesu Kristo. Hayo yamebainishwa na Derek Murusuri Mwandishi wa Vitabu wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha HIDDEN TRUTH ABOUT LORD JESUS CHRIST Jijini Dodoma amesema Maandiko katika kitabu hiki hakikosoi Imani ya Kristo au Dhehebu lolote lile. "Kitabu hiki kinatoa mchango wake kwa unyenyekevu , wa kumfunua Baba ni nani kinabainisha baadhi ya mafungu ya Biblia yanayomfunua na kumthibitisha muumbaji wa Mbingu na nchi, Ambaye pia Ndiye Baba Mungu , Anayekuja kitambulishwa katika Agano jipya kuwa muumbaji wa vitu vyote vilivyopo Mbinguni na Duniani, Niyule Aliye kuja kwetu kama Mwana na Ndiye Yesu Kristo" Pia Mwandishi Murusuri amesikitishwa na kitendo Alichokifanya Mchungaji wa Dhehebu ninaro Abudu pale Dares Saam kuzuia kitabu hiki kisiuzwe kanisani hapo, kwa sababu kwenye kitabu hicho kuna sehemu nimeandika Bwana Yesu Kristo ndiyo Mungu Mwenyewe Alisema katika Ulimwengu Huu ambao umejawa na Imani kwamba Yupo Baba, Mwana pamoja na Roho Mtakatifu" kitabu kinakuja na Kusema Yule Mwana Ndiye Baba, watu hawaamini wanahisi napotosha. Aidha Mwandishi Murusuri Kitabu hiki ni Zawadi kwa watoto wa Mungu, Wenye tamanio na Tashwishwi ya kumfahamu Mungu, wanao mfikiria Bwana Mungu Usiku na Mchana wakitaka kumjua vizuri zaidi ili wampatie Utukufu unaostahili . "Vitabu vya ISAYA,Yohana,Wakolosai,Tito, Ufunuo na Mwanzo, vinatoa ushahidi usio na chembe ya shaka kuwa muumbaji wa vitu vyote vya Mbinguni na Duniani ni Yesu ambaye alikuwa alikuja kwetu kama Mwana na Ndiye aliyetamkwa na Musa kama Mungu muumbaji wa Mbingu na Dunia katika Mwanzo. Sambamba mwandishi Murusuri alitumia nafasi hiyo Kumshukuru sana Mungu kwa kumsaidia kutimiza Ndoto ya kuandika kitabu hicho , kwani hili ni ombi lake la Muda mrefu akiomba kumjua Yesu Kristo na sasa amejifunua kwake kupitia Maandiko matakatifu nakuchukua hatu ya kuandika kitabu hiki cha Hidden Truth About Lord Jesus Christ, kikiwa ni kitabu chake cha pili kitabu cha kwanza kinaitwa MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY Media, Culture and Development pia kipo Mtaani kinafanya vizuri Alisema kwenye Soko .
Derek Murusuri Mwandishi wa Vitabu wakati Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma
Derek Murusuri Mwandishi wa Vitabu pamoja na Waandishi wa Habari
My Son, Kaitira Derek Murusuri, in a cultural attire, sharing the Hidden Truth about Lord Jesus Christ book by Derek Murusuri in the United States as he also promotes his motherland in a foreign land by taking folks to Tanzania, the land of unforgettable experiences for a minute. To God be the glory.

MKATABA UJENZI MRADI WA MAJI CHANZO CHA MTO KIWIRA WASAINIWA MBEYA

Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya-UWSSA) imesaini mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 117.5 na mkandarasi kampuni ya China Railway Construction Engeneering Group kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka chanzo cha maji cha mto Kiwira. Mradi huo unatarajia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika jiji la Mbeya kutoka lita milioni 66.5 zinazozalishwa kwa siku hadi lita milioni 184 kwa siku. Akizungumza jijini Mbeya katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema fedha zote za utekelezaji wa mradi huo zimetolewa na serikali. Amesema Wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha fursa ya vyanzo vya uhakika vya maji inatumika kuondoa changamoto ya majisafi sehemu mbalimbali nchini. Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Ujenzi na Ufuatiliaji Miradi Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema awamu ya kwanza ya utekekezaji wa mradi huo itakamilika katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Februari 25 mwaka huu hadi Februari 24, 2025. Naye Mbunge wa Mkoa wa Mbeya kupitia Viti Maalum Wanawake Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wa Mbeya wanapata maji ya uhakika kupitia chanzo hicho. Amewahakikishia wananchi wa mbeya kuwa serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia ni sikivu, itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili akinamama wa Mbeya waondokane na changamoto ya huduma ya majisafi na salama.

WAZIRI MHAGAMA AMEZITAKA TAASISI ZOTE KUFUATA SHERIA

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ,Mhe. Jenista Mhagama amezitaka Taasisi zote za umma nchini kuhakikisha zinazingatia na kufuata sheria, na kanuni za Serikali Mtandao . Ameyasema hayo Feb 10 jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha 3 cha Serikali mtandao kilichowashirikisha zaidi ya watumishi wa umma 1600 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Amesema kuwa,ni lazima taasisi zote za umma zihakikishe zinafuata sheria zilizopo ili kuwezesha kufanya kazi kwa weledi na uzalendo kwa ustawi wa nchi na kuweza kuokoa gharama kupitia huduma za kidigitali. “Naagiza mkaanze kufanya vikao vya kitaasisi kila mwaka katika ngazi za wilaya na mkoa katika kuhakikisha mnatathimini huduma ya serikali mtandao katika ngazi za wilaya na mkoa ili huduma hiyo iweze kuboreshwa na kutumia na taasisi zote za umma.”amesema Waziri Jenista . Aidha amewataka kupitia kikao hicho wakatekeleze maazimio yote waliyojiwekea huku akiwataka kuendana na mabadiliko ya kasi ya duniani ya teknolojia yaliyopo hivi sasa kwani hawatakiwi kuwa nyuma . “Wataalamu na wakuu wa idara nawaomba sana mhakikishe mnafanya kazi zenu kwa weledi na uzalendo mkubwa kwa faida ya Taifa letu, huku mkihakikisha kila mmoja anakuwa mwaminifu katika usimamizi wa mifumo ya Tehama. “amesema Waziri Mgahama. Kwa upande wake Mmoja wa washiriki katika mkutano huo,ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe ,Judica Omary amesema kuwa,kikao hicho ni cha tatu kufanyika na wameweza kujadili changamoto mbalimbali na kuweka mikakati na maboresho mbalimbali ikiwemo ya kuongeza matumizi ya mtandao serikali. Amesema kuwa, kikao hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwao watumiaji wa serikali mtandao katika kukuza taaluma zao . Amesema kuwa,wamejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanaenda kutekeleza huduma ya serikali mtandao katika taasisi zao kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa taasisi zao. “Kwa pamoja tumejiwekea mikakati ya kuhakikisha tunaenda kufanya vikao vyetu kidigitali katika vikao mbalimbali ikiwemo vikao vya madiwani na kuondokana na matumizi ya makaratasi.”amesema. Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya serikali mtandao (eGA) ,Mhandisi Benedict Ndomba akielekezea maazimio waliyojiwekea amesema kuwa , kwa pamoja wameweza kujiwekea maazimio mbalimbali ikiwemo kuhakikisha taasisi za umma anatumia huduma ya serikali mtandao katika kuendesha shughuli zake pamoja na vikao vya madiwani ili kuweza kupunguza matumizi ya makaratasi. Amesema kuwa,wamejiwekea maazimio ya kuhakikisha tovuti zote zinaboreshwa ili kuweza kwenda kisasa zaidi ,huku wakizitaka taasisi za umma kutoa kipaumbele kwenye maswala ya Tehama . Aidha amesema kuwa,maazimio mengine ni pamoja na kuhakikisha wakuu wa taasisi za umma kuhakikisha wanasimamia kikamilifu usimamizi wa sheria za serikali mtandao, sambamba na kuiomba serikali kuanzisha upekuzi kwa watumiaji wa huduma za Tehama. Kwa upande wake Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,Xavier Daudi amesema kuwa, wanaenda kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa katika kuhakikisha huduma ya serikali mtandao ina imarika zaidi. “Tunaendelea kusisitiza zaidi matumizi ya Tehama kwani yatasaidia sana kuokoa gharama ya kutumia matumizi ya makaratasi huku tuhakikisha kunakuwepo kwa matumizi sahihi ya huduma mtandao. “amesema.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ,Mhe. Jenista Mhagama wakati akifunga kikao kazi jijini Arusha

MAMA AFARIKI AKIFANYIWA MAOMBI KANISANI

Polisi nchini Uganda wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 59 Rosette Najjuma -ameaga dunia akiwa kanisani jijini Kampala. Kwa mujibu wa naibu msemaji wa polisi wa Kampala Luke Owoyesigyire, Najjuma alizirai na kufariki ibada ikiendelea katika kanisa la Christian Life katika Parokia ya Makerere III mnamo Jumatano - Februari 8,2023. Mwanamke huyo anaripotiwa kufanyiwa vipimo kadhaa katika Hospitali ya Mulago kwa muda wa miaka mitatu iliyopita lakini hakuna ugonjwa uliopatikana. Jamaa zake waliamua kumtafutia msaada wa kanisani na hivyo kumpeleka katika kanisa la Pasta Jackson Ssenyonga. Mwanamke huyo alizirai akifanyiwa maombi mwendo wa saa kumi alfajiri na kuaga dunia kabla ya kufanyiwa msaada wowote wa kimatibabu. Owoyesigyire alisema kuwa mwili wake ulihamishiwa makafani ya Mulago ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

AJARI ZA BARABARANI ZAMUIBUA WAZIRI MASAUNI,ATANGAZA MSAKO WA MADEREVA WA ZEMBE.

Na Johndickson Gaudin Dodom. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema wizara imejipanga kuhakikisha inapambana na kuthibiti Ajari za barabarani zinazoendelea kutokea hapa nchini. Hayo ameyasema wakati wa kikao chake na waandishi wa habari Leo hii februari 10,2023 jijini dodoma ikiwa ni baada ya kutokea kwa Ajari iliyo husisha basi na roli iliyotokea wilaya ya kongwa jijini dodoma iliyo sababisha vifo vya watu 12. Amesema wizara imeanza kuchukua hatua madhubuti ikiwa nipamoja na kukagua leseni za madereva wa magari yote pamoja na maroli ya mizigo ,kukagua vyuo vyote vya udereva nchini na kuangalia mfumo wa utoaji wa leseni nchini. "Uchunguzi wa hawali katika Ajari iliyotokea ulionyesha waliokuwa wanaendesha magari hayo Siyo madereva na kupelekea kutokea kwa Ajari hiyo. "Nataka nitoke onyo Kali kwa madereva na wamiliki wa magari wanao kinzana na Sheria hizi hatua Kali zitachukuliwa pale watakapo bainika kukiuka Sheria na taratibu za usalama barabarani,"amesema. Aidha waziri Masauni amesema kupitia jeshi la polisi wameanza dolia katika maeneo yote nchini kufatilia mwenendo wa madereva,pamoja na kutumia Teknolojia za kisasa ikiwa na kufunga kamera barabarani zitakazo saidia kubainisha uvunjifu wa Sheria za barabarani. Kwaupande wake kamanda Mkuu wa polisi (IGP)Kamiliusi Wambura amewaomba wananchi kusaidia kuwaripoti maafisa wanaoomba na kutoa Rushwa. "Sisi tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuweza kuona tudhibitishe vitendo vya Rushwa nchini na tunaadhibu kwa yeyote anaye omba na kutoa Rushwa ,"amesema kamanda Wambura.

FAIDA FUND YAPATA MAFANIKIO YA MAUZO HAWAMU YA KWANZA

Na. Johndickson Gaudin Dodoma Mfuko wa Uwekezaji wa pamoja FAIDA FUND umefanikiwa kuwa Mfuko wa kwanza wa aina yake kupata mafanikio makubwa katika kipindi cha mauzo ya awali ikilinganishwa na lengo lililowekwa la kuanzishwa kwake. Hayo yamebainishwa leo Februari 9,2023, Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investiments (WHI), Dkt. Fred Msemwa mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Watumishi Housing Investiments katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Dkt. Msemwa amesema Mfuko huo umeyalenga makundi yote ya kijamii na lengo lake likiwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji wa pamoja wakiwemo watoto, wakulima, wavuvi, watumishi wa umma, wafanyakazi, makampuni na taasisi.“Faida Fund imenzishwa chini ya sheria ya masoko ya Mitaji na dhamana sura 79 ya sheria za Tanzania, Mfuko huu unasimamiwa na mamlaka ya masoko na dhamana (Capital Market and Securities Authority - CMSA) ambaye ndiye mdhibiti wa Sekta,” amesema. Amesema mfuko huo umekuja sokoni kuongeza nguvu na kuchochea tabia ya kuwekeza ukiwa na lengo kuwawezesha watanzania kiuchumi kwa kukuza mitaji yao.“Mwekezaji anaweza kufungua akaunti ya uwekezaji kwa kutumia menyu kuu ya serikali ya *152*00# au kwa kutumia WekezaWHI App ambayo inapitikana kwenye simu janja au kwa kutumia mfumo wa FAS (Fund Administration System) ambao umebuniwa na Mamlaka ya serikali Mtandao,”amesema.Aidha ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake WHI imejenga jumla ya nyumba 983 katika maeneo mbalimbali ambazo zimeuzwa kwa watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.Vilevile amesema Watumishi Housing Investiments imeendelea kuwauzia nyumba kwa mkopo nafuu watumishi wa umma ambao walikuwa hawawezi kununua nyumba kwa mkopo kutoka taasisi zingine katika soko.“Hii imewanufaisha watumishi haswa kanda ya kati na chini wakiwemo wauguzi na watumishi wa manispaa, ”amesema.Watumishi Housing Investment (WHI) ni taasisi ya umma iliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), iliyoanzishwa mwaka 2014 kupitia mifuko ya Pensheni kwa watumishi wa umma (PSSSF), Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF), shirika la Nyumba la Tatumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), iliyoanzishwa mwaka 2014 kupitia mifuko ya Pensheni kwa watumishi wa umma (PSSSF), Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF), shirika la Nyumba la Taifa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investiments (WHI), Dkt. Fred Msemwa mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Watumishi Housing Investiments

UDAILI WA WANAFUNZI (DMI) KUONGEZEKA IFIKAPO 2025_2026 HADI WANAFUNZI ELFU

Na Johndickson Gaudin Dodoma Chuo cha Baharia Dar es salaam (DMI) kinatarajia kudaili wanafunzi takribani Elfu 20 Hadi 23 ifikapo mwaka 2025_2026 hii ikiwa ni juhudi za chuo hicho katika kuhakikisha kina zalisha wanafunzi wenye weledi katika sekta ya Ubaharia. Hayo yamebainishwa na kaimu Mkuu Wa Chuo hicho Dkt. Tumain Shaban Kwenye Mkutano na waandishi wa Habari hii Leo February 09 2023 jijini Dodoma ambalo amesema jitihada hizo nikwaajili ya kuhakikisha wanazalisha wanafunzi wengi na kuacha kuchukua mabaharia kutoka nje ya nchi. Dkt.Shaban amesema kupitia serikali ya awamu ya sita chuo hicho kimeweza kupata fedha takribani shilingi bilion 6.5 kwaajili kununulia vifaa vya kufundishia ambavyo ni mashine pamoja na mitambo Mbalimbali"Serikali imefungua zaidi milango ya kupata mikopo Kwa wanafunzi wetu kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu Jambo ambalo limeongeza idadi ya wanafunzi. "Kwa mwaka 2022_2023 wanafunzi 1705 wamepata mikopo ukilinganisha na mwaka 2021_2022 ambapo wanafunzi 850 ndio walipata mikopo " ,amesema Dkt Shaban.Aidha amesema kupitia serikali ya awamu ya sita kimeweza kupata maeneo Mbalimbali ya kujenga matawi ya chuo hicho ikiwa nipamoja na mkoa wa Lindi na Mwanza matawi ambayo yatawezesha kufikisha elimu ya Ubaharia katibu na wananchDkt Shaban ameongeza kuwa chuo hicho kinafanya utafiti na kutoa ushauri elekezi Kwa serikali na taasisi binafsi,pia chuo hicho kinafanya usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri vya majini."Shughuli zinazofanywa ni usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri majini Tathimini ya maji katika vyanzo vya maji baadhi ya vyombo hivyo nipamoja na MV Kigamboni, MV . SAR, M.V MWONGOZO,"amesema Dkt Shaban
kaimu Mkuu Wa Chuo hicho Dkt. Tumain Shaban Kwenye Mkutano na waandishi wa Habari hii Leo February 09 2023 jijini Dodoma

UTEUZI: EPHRAIM BALOZI MAFURU ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU AICC

WATU 12 WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI DODOMA

Dodoma WATU 12 wamepoteza maisha baada ya basi a Frester lililokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar es salaam kugongana uso kwa uso na Lori la Texas majira usiku wa kuamkia leo. Ajali hiyo imetokea eneo Kiiji Cha Silwa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. Katibu Tawala mkoa wa Dodoma Dk Fatma Mganga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo watu 12 wamepoteza maisha. Álisema mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule yuko eneo la tukio.

PROF.MKENDA :BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA KWA WANAFUNZI NA WASIMAMIZI WA MITIHANI KIDATO NNE MWAKA 2022 .

Na. Mwandishi wetu Dodoma SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imesema imedhamiria kukomesha vitendo vya wizi wa mitihani huku ikiridhishwa na uamuzi wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa wanafunzi 337 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao ya kidato cha nne mwaka 2022. Hayo yamesemwa leo Februari 8,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,wakati akitoa ufafanuzi kwa waaandishi wa habari kufuatia Video iliyosambaa mitandaoni ikionesha Wazazi wa wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari Thaqaafa iliyopo Jijini Mwanza wakiandamana kudai Watoto wao hawajatolewa matokeo ya Kidato Cha Nne. Prof.Mkenda amesema Wizara hiyo itapeleka marekebisho ya sheria ya baraza hilo bungeni ili hatua zaidi zichukuliwe kwa wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani. “Mtihani wa darasa la saba tulivyorudia tulitumia mabilioni ya fedha za watanzania kwa hiyo ni uhujumu uchumi kudanganya kwenye mitihani, polisi wanafanya uchunguzi kwenye hili tunaamini hatua zitachukuliwa na wizara imeridhika na hatua zilizochukuliwa na baraza, ”amesema Prof.Mkenda Amesema kuwaa kati ya watahiniwa 560375 waliofanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2022 matokeo ya watahiniwa 337 sawa na asilimia 0.06 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wamefutiwa matokeao kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujaza matusi,kuingia kwenye chumba cha mitihani na maandishi,kuingia na simu na smartwatch. Prof.Mkenda amesema kuwa serikali imeridhishwa na uamuzi uliofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA) kuhusu wanafunzi 337 waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani hiyo. “Sisi uongozi wa baraza tumekutana na kila kundi la wale ambao matokeo yao yamefutwa, tumejiridhisha na tungependa kutoa matokeo yafuatayo wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne ni 560,335 kati ya hao wanafunzi waliofutiwa matokeo ni 337.” “Hii ni asilimia 0.06 ya watahiniwa wote ni asilimia ndogo sana lakini inagusa watanzania wenzetu wanafunzi wengine 20 matokeo yao hayajafutwa yamezuiwa bado uchunguzi unaendelea na utakapokamilika baraza litachukua hatua stahiki,”amesisitiza . Amesema kuwa Wizi wa Mitihani ni kosa kubwa sana ni sawa na uhujumu uchumi na hatukubaliani nalo na wezi wa mitihani lazima wakamatwe na washughulikie kisheria kwa sababu haivumiliki. ‘Tayari barua zimeandikwa kwa Mamlaka husika juu ya Wasimamizi wa mitihani hiyo kwani Kuna uchunguzi unaonesha Usimamizi ulikuwa Mbovu huku Polisi wakiendelea kufanya uchunguzi, kwa kuhoji wanafunzi na Walimu ambapo wanafunzi wamekiri.’amesema Prof.Mkenda

DK.SWEKE: BAHARI KUU IPO SALAMA TUNATUMIA NDEGE KUFANYA DORIA

Na. Kadala Komba Dodoma. MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,ameeleza kuwa katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kufuatilia meli ndani ya maji na kutumia doria za ndege kwa ajili ya kuangalia kinachofanyika. Hayo ameyasema leo Februari 8,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shuguli mbalimbali za Mamlaka hiyo. Dk. Sweke, amesema Mamlaka hiyo ina jukumu la kutoa leseni kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu kwa meli za ndani na nje pamoja na kulinda,kusimamia na kuratibu shughuli zote za uvuvi wa bahari kuu. Amesema kuwa makusanyo hayo yamevunja rekodi iliyowekwa na Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka saba iliyopita. “Makusanyo makubwa ya mwisho yalikuwa ni Sh. bilioni 4 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 lakini yalishuka sana baada ya kuletwa kwa kanuni ambayo ilikuwa inawataka wavuvi kutoa muraba wa dora 0.4 kwa kila kilo moja ya samaki. “Hali hii ilisababisha makusanyo kushuka sana kutokana na meli nyingi za uvuvi kukimbia na kuacha kufanya uvuvi katika nchi yetu lakini kutokana na hali hiyo tulijifungia na kuondoa kanuni hiyo na sasa matunda yanaonekana kwa kupanda kiasi cha ukusanyaji wa mapato yatokano na utoaji wa leseni za uvuvi na huduma nyingine zinazotolewa na mamlaka hii”amesema Dk. Sweke “Mifumo hii tunayotumia sasa pamoja na kufanya doria kwa kutumia ndege zimesaidia sana kukomesha vitendo vya uvuvi harafu bahari kuu”amesema Dk. Sweke Hata hivyo amesema toka Mamlaka kuanzishwa imefanikiwa kukamata meli moja iliyokuwa na samaki tani 100 ya samaki wasiolengwa. Aidha kipindi cha mwezi Julai 2022, hadi Februari mwaka huu Mamlaka hiyo imekusanya Sh.bilioni 4.1 ikiwa ni mapato yatokanayo na utoaji wa leseni kwa ajili ya meli za uvuvi na huduma nyingine.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8,2023 jijini Dodoma
WAANDISHI wa habari wakati wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,

NSSF IMEJIPANGA KUANZA KUTOA MAFAO KWA SEKTA ISIYO RASMI

Na. Kadala Komba Dodoma. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)umewataka wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huo kwa kupeleka michango yao na hatimaye kuwa kwenye mfumo wa mafao hali itakayosaidia kupunguza umasikini. Hayo yameelezwa jijini hapa leo ,Februari 8,2023 na Mkurugenzi Mkuu NSSF,Masha Mshomba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko na mwelekeo wa utendaji katika mwaka wa fedha 2022/23 . Amesema wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kama vile Mama Lishe, bodaboda, wafugaji, wakulima n.k wanapaswa kubadili mtazamo wa maisha ili kuepukana na changamoto za uzeeni kwa Kujiunga na NSSF kwani watapata pensheni ya uzeeni kama wale walio katika sekta rasmi . "Tunajiimarisha zaidi kwani mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi utasaidia kuimarisha na kuboresha maisha ya watanzania,Kila mtanzania anapaswa kuelewa kuwa pensheni ya uzeeni ni haki ya kila Mtanzania hivyo ni wakati sasa kwa wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na NSSF ili kufaidika na Mafao mbalimbali yatolewayo ikiwemo pensheni ya uzeeni,mikopo na bima ya afya,"amesema Mkurugenzi huyo. Katika hatua nyingine Mshomba ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, mfuko huo unatarajia kukusanya michango ya shilingi trilioni 1.6 ambayo ni ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na michango ya shilingi trilioni 1.4 iliyokusanywa na Mfuko katika mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022. Amesema Mfuko umeendelea kuimarisha mifumo na usimamizi wa fedha ili kuepuka mianya ya upotevu wa fedha, kuendelea kumudu gharama za uendeshaji pamoja na kulipa mafao stahiki kwa wastaafu na wanufaika wengine. "Katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, Mfuko unatarajia kulipa mafao yenye thamani ya shilingi bilioni 769.3 ambayo ni ongezeko la asilimia 17 ukilinganisha na shilingi bilioni 659.8 zilizolipwa katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022,"amesema Mshomba. Ili kujiiamarisha kiuchumi zaidi amesema kuwa kufikia Julai mosi mwaka huu mfumo huo utaweza kuzalisha sukari kupitia kiwanda cha sukari cha Mkulazi. Amesema kiwanda hicho kitapunguza changamoto ya uhaba wa sukari inayojitokeza mara kwa mara na kulazimu serikali kutegemea wazalishameeleza kuwa mfuko huo katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, unatarajia kukusanya michango ya shilingi trilioni 1.6 ambayo ni ongezeko la asilimia 14 . Mshomba ameeleza kuwa Mradi huo unatarajiwa kutoa fursa ya soko kwa wakulima wa nje wanaolima miwa katika mashamba yenye takribani hekta 450, miundombinu mingine kwa ajili ya wananchi wanaouzunguka mradi huo,ajira zaidi ya 2,315 za moja kwa moja, megawati 15 za umeme zinazotarajiwa kuingizwa katika gridi ya Taifa kupitia kituo cha kupokelea na kupoza umeme Msamvu. Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo Mshomba ameeleza kuwa ukuaji wa Mfuko kwa Kiwango Kikubwa Katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mfuko umekuwa kwa kiasi kikubwa ambapo thamani ya Mfuko imeongezeka na kufikia shilingi trilioni 6.6 mwezi Desemba 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 39 kutoka shilingi trilioni 4.7 iliyofikiwa mwezi Machi 2021
Mkurugenzi Mkuu NSSF,Masha Mshomba akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika mkutano na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.

RC KINDAMBA AWATAKA MA-DED KUSIMAMIA UKUSANYAJI FEDHA

Na. Mwandishi wetu Songwe Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo wasimamie fedha zinazokusanywa zipelekwa benki ili kuepuka wakusanyaji kuzitumia fedha hizo. Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito huo umetolewa leo Jumanne Februari 7, 2023 wakati wa kikao cha tathmini za utendaji wa Halmashauri za mkoa wa Songwe. RC Kindamba ameongeza kuwa utekelezaji hafifu wa vikao vya kisheria vinavyosababisha malalamiko mengi ambapo vingeshughulikiwa chini kabisa. Ametaja moja ya kazi ya kiongozi katika watu anaowaongoza ni kisikiliza na kutatua kero kwa wakati zinazowakabili wananchi. Ametaja kazi nyingine kuwa ni kusimamia ukusanyaji wa mapato, ulinzi na usalama. "Tuendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi na kusimamia kwa nguvu eneo la ukusanyaji wa mapato" Amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kusimamia kwa weledi miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati.

IDADI YA VIFO VYA WATOTO YA SHUKA HADI 66% MWAKA 2022

Na. Johndickson Gaudin Dodoma Idadi ya watoto wanao hudumiwa na muhudumu wa afya mwenye ujuzi wakati wa kuzaliwa imepanda kutoka asilimia 66% Mwaka 2015-2016 hadi asilimia 85% mwaka 2022 na hivyo kuchangia kupungua vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambavyo ni 43 kati ya watoto 1000 wanaliozaliwa kwa mwaka 2022 ukilinganisha na vifo 67 kati ya watoto 1000 wanaliozaliwa kwa mwaka 2015. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu wakati wauzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya maralia wa mwaka 2022 uliofanyika leo februali 7,2023katika viwanja vya Mtakwimu mkuu wa Serikali jijini Dodoma,na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wananchi.Waziri Ummy amesema Matokeo ya utafiti huo yatasaida kuelewa changamaoto ambazo wananchi wanazipitia katika sekta ya Afya hususani afya ya Mama na Mtoto na mapambano dhidi ya Malaria nakuwezesha kutengeneza mipango mikakati ya kuboresha sekta ya afya. Aidha amesema matokeo hayo yatasaidia katika ngazi ya kitaifa kupima utekelezaji wa viashiria vya afya katika sekta ya afya pia katika maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 , dila yamaendeleo Zanzibar 2050 na mpango wa tatu wa maendeleo ya kitaifa. “Jitihada zetu za kuongeza miundo mbinu ya kutoa huduma ya afya pamoja na kuajiri watumishi wa afya zimeleta matokeo chanya katika kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano.“Tumetoka vifo 67 vya watoto hadi vifo 43 kati ya watoto 1000 wanao zaliwa haya nimatokeo makubwa ya juhudi zinazo fanywa na serikali zetu mbili katika utekelezaji wa malengo tulio jiwekea na tumesema malengo yetu 2025-2026 vifo vya watoto chini ya miaka mitano viwe 40 kwa kila vizazi hai 1000”, amesemaSanjari na hayo waziri Ummy amewataka wadau wa afya kutojirundika mkoa mmojabadala yake kusambaa mikoa yenye changamoto za udumavu wa watoto ikiwa nipamoja na Mkoa wa Shinyanga , Rukwa , Njombe pamoja na Iringa Kwaupande wake Mtakwimu mkuu wa serikali Dkt. Albina Chua amesema utafiti huo utaendea kutumika katika kutimiza sera za afya na sera nyingine zinazotakiwa kuboresha sekta ya afya na kufanikasha mipango ya maendeleo kwa watanzania woteAmesema wamefanya uzinduzi wa ripoti muhumu ya kwanza ambayo haitaji kungoja kufanyiwa uchambuzi na viashiria vya ripoti hiyo vitaenda kusaidia katika sekta ya afya ikiwa nipamoja na vifo vya watoto chini ya miaka mitano “Huduma zimeboreshwa katika vituo vya afya na tumeona jinsi serikali inavyopambana na matokeo haya tumeyakusanya kupitia wahudumu wa afya wenye weledi, ninaimani nitarifa zitakazo endakueleza serikali inavyo tekeleza yote yaliyowekwa kwenye mkakati na wizara ya afya,” amesema dkt.chua Naye Kamisaa wa Sensa Tanzania bara Anne Makinda amesema Utafiti wa ripoti hiyo ni miongoni wa tafiti muhimu ambazo zina ipafursa serikali kutadhimini utekelezaji wa sera na mipango ya kuimarisha afya za wananchi.Makinda amesema matokeo ya utafiti huo yatatoa mtazamo wa hali ilivyo katika sekta ya afya hususani hali ya uzazi na mtoto na viashiria vya maralia, pia yataonyesha jitihada za serikali zilivyofanya kazi kwaajili ya kuimarisha afya ya uzazi na mtoto na jitihada zilizo fikia kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa malaria “Matokeo ya uchambuzi huu yametokana na dodoso la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ingawa utofauti wa utafiti wa ripoti hizi unafanyika kila baada ya miaka mitano huku tafiti za sensa ya watu na makazi zikifanyika kila baada ya miaka 10,” amesema Makinda
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu wakati wauzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto
Mtakwimu mkuu wa serikali Dkt. Albina Chua

WALIOTUMIA PICHA YA VIJANA WA JKT WALIOKUWA MAKAMBINI KUWA WANA VVU WAMETAKIWA KUOMBA RADHI

Na Kadala Komba, Dodoma. JESHI la Kujenga Taifa (JKT),limesema kitendo cha baadhi ya mitandao ya kijamii na magazeti kutumia picha za vijana wengine wanaohudhuria mafunzo ya JKT wa wasiohusika katika habari ni udhalilishaji. Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Februari 6,2023 na Mkuu wa Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,wakati akitoa ufafanuzi kwa umma kupitia waandishi wa habari kuhusu vijana 147 wa JKT kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika habari iliyoripotiwa Bungeni Februari 3,2023 na kamati ya UKIMWI ambapo amesema ni kitendo cha ukosefu wa maadili ya uandishi wa habari na kwamba uhuru wa vyombo vya habari haukutumika ipasavyo. "Jeshi la kujenga Taifa limesikitishwa na habari hii ya vijana idadi ya 147 kuwa na maambukizi ya VVU na kuambatanishwa na picha ya vijana wengine waliohudhuria mafunzo ya JKT Makambini,"amesema. Kutokana na hayo Brigedia Jenerali Mabena amevitaka vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii vilivyoripoti habari hiyo kwa kuweka picha za vijana wa JKT ambao si wahusika wa habari hiyo,kuomba radhi na kuondoa picha hiyo mara moja. Aidha Mabena ametoa ufafanuzi kuwa mafunzo ya vijana wa kundi la lazima yaani wahitimu wa kidato cha sita uendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu. Amesema kabla ya kuanza mafunzo vijana hufanyiwa usahili wa nyaraka zao pamoja vipimo vya afya ili kufahamu utimamu wa mwili(Physical Fitness). Ambapo vijana ambao majibu ya vipimo vyao huwa na changamoto za kiafya hufanya mafunzo yao chini ya uangalizi wa wakufunzi ili kuhakikisha wanamaliza mafunzo yao salama. "Kwa kuwa hilo ni kundi la lazima(Compulsory),vijana wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho(Physical Disabilities)hupokelewa katika kikosi cha Ruvu JKT ambacho kina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo,"amesema. Vilevile amesisitiza kuwa kigezo cha Afya kwa vijana hao wa kundi la lazima wanaokuja makambini wakiwa na changamoto za kiafya kinazingatiwa kwa kuwaweka chini ya uangalizi. "JKT linazingatia sheria kanuni na taratibu za kitabibu sambamba na kuzingatia mila na desturi za nchi yetu katika kutekeleza jukumu lake la msingi la malezi ya vijana. Pamoja na hayo Mabena aliwatoa wananchi hofu kuwa JKT ni salama yenye kuzingatia sheria na taratibu za miongozo ya malezi ya vijana na kundi la lazima na vijana wa kujitolea. Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari,Gerson Msigwa amewataka wananchi kutambua kuwa vijana hao waliokutwa na maambukizi ya VVU ni wale ambao bado hawajaingia JKT. "Wanahabari tuzingatie weledi na niwatake vyombo vya habari walioripoti habari hiyo kwakutumia picha za vijana wa JKT ambao tayari wapo Makambini waombe radhi,"amesema Msigwa.
Mkuu wa Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,wakati akitoa ufafanuzi kwa umma kupitia waandishi wa habari kuhusu vijana 147 wa JKT kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika habari iliyoripotiwa Bungeni Februari 3,2023 na kamati ya UKIMWI
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari,Gerson Msigwa