*Na Grace Semfuko - MAELEZO na Dorina Makaya -Wizara ya Nishati.*
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono Ajenda ya Maendeleo ya Mwaka 2063 iliyowekwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika- AU ambayo ina mikakati ya kufikia Afrika yenye ustawi na umoja.
Dkt. Biteko ameyasema hao leo Septemba 15, 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Husein Mwinyi kufungua Mkutano wa nne wa Kamati Maalum ya Kitaalam, kuhusu Sekta ya Uchukuzi, Miundombinu ya Kikanda ya Bara la Afrika pamoja na Nishati ambapo ameongeza kuwa, jiografia ya Bara hilo ni ya kimkakati na inaturuhusu kuunganishwa na ulimwengu kwa njia ya anga, usafiri wa barabarani na majini na hivyo kuna kila sababu ya Afrika kuendelea kuwa katika umoja huo.
*“Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono ajenda ya mtangamano wa Afrika iliyowekwa na AU, ajenda ya 2063 inatupa Dira ya Afrika tunayoitaka ili kufikia Afrika yenye ustawi na umoja, utekelezaji wa mikakati ya ajenda hiyo ni nyenzo muhimu sana ya kutufanya tuyafikie malengo yetu hivyo majadiliano yenu ambayo yanaongozwa na kaulimbiu ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu ili kufikia malengo ya 2063 ni muhimu sana kwenye mkutano huu”* amesema Dkt. Biteko
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Khalid Salum amesema mkutano huo ni fursa nyingine ya kupokea taarifa kuhusu maendeleo yaliyopatikana tangu mkutano uliopita uliofanyika kwa njia ya mtandao mwezi juni mwaka 2021 ambapo kwa sasa, pamoja na mambo mengine, watajadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kufikia malengo ya Bara la Afrika.
*”Ninatambua kwamba uwepo wenu kwenye mkutano huu ni ishara yetu ya pamoja ya kuendeleza miundombinu na kupata suluhisho la changamoto za nishati na miundombinu Barani Afrika”* amesema Dkt. Khalid.
Kwa upande wake Kamishna wa Miundombinu kutoka katika Kamisheni ya Umoja wa Nchi za Afrika-AU Dkt. Amani Abou-Zeid amesema Afrika haina budi kuharakisha maendeleo ya miundombinu ili kuleta ushindani na katika ushiriki wa watu wa Bara hilo katika soko la kimataifa la bidhaa.
*“Kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya Afrika ni jambo la kipaumbele, haijalishi kuwa miundombinu yetu ni mizuri kiasi gani, sote tunajua kuwa tunahitaji kuharakisha ujenzi wa miundombinu yetu ili kuwe na matarajio makubwa kwa watu wetu, hii ni kwa ajili ya kuleta ushindani katika ushiriki wetu kwenye soko la kimataifa”* amesema Dkt Amani.
*Mwisho.*
Home »
» *Tanzania yaunga mkono Ajenda ya AU 2063- Dkt Biteko.*
*Tanzania yaunga mkono Ajenda ya AU 2063- Dkt Biteko.*
Related Posts:
WAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUTOA USHAURI WENYE TIJAUkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Bw. Paison Mwamnyasi, amewataka Wakaguzi wa Ndani kuzingatia sheria, kanuni, viwango na miongozo ya Serikali Mtandao wanapofanya ukaguzi kwenye miradi na Mifumo ya TEHAMA, ili waweze kutoa us… Read More
TANZANIA, UINGEREZA KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA Na WMJJWM, DodomaSerikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekubaliana na Kamisheni ya Uingereza kushirikiana ili kuimarisha usawa wa kijinsia nchini.Hayo yamebainika wakati wa k… Read More
SAKATA LA BANDARI MSUKUMA AWATOA HOFU WATANZANIA. Na Moreen Rojas,Dodoma.Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amewatoa hofu watanzania kuhusiana na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya viongozi wa siasa kuhusu mkataba wa bandari unaotarajiwa kupiti… Read More
NHC KUSHIRIKI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI Na Eleuteri Mangi, WUSM, DodomaKatibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah ambapo wamej… Read More
DKT. YONAZI APONGEZA HATUA ZA UJENZI WA ENEO LA MNARA WA MASHUJAA. KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amepongeza maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.Dkt. Yonaz… Read More
0 Comments:
Post a Comment