Na. WAF - Dodoma
Wizara ya Afya kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI hadi sasa imeweza kusambaza vifaa vya mtu kujipima mwenyewe maambukizi ya Virusi vya UKIMWI zaidi ya Mil. 1.6 kuanzia Mwaka 2021 nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo kwenye kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi alikua ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuongeza nguvu za kusambaza vifaa hivyo vya watu kujipima wenyewe Virusi vya UKIMWI ili kuweza kutambua hali zao wenyewe na kwa haraka kuhusu ugonjwa huo.
Waziri Ummy amebainisha kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kupanua wigo wa vituo vya kupima na kutoa huduma za matunzo (CTC) kwa watu wenye UKIMWI ambapo hadi sasa tuna vituo 8,529.
“Nitoe rai kwa watu wote wanaoishi na VVU kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI ili kuweza kujilinda wao wenyewe lakini pia kuwalinda wengine” amesisitiza Waziri Ummy.
Pia, Waziri Ummy amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kutoa huduma za kupima, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU hapa nchini ili vituo vyote vinavyotoa huduma za Afya viwe pia vituo vya kupima na kutoa matunzo (CTC) kwa 95% ifikapo Mwaka 2025.
Aidha, Waziri Ummy amesema chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia, Serikali itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vitendanishi kwaajili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kuendelea kufuatilia taarifa zote kuhusu uwepo wa dawa mpya ambazo ni bora zaidi.
Mwisho, Waziri Ummy amelipongeza Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA) kwa kuanzaa mdahalo wa kuadhimisha Miaka 20, “Sekta ya Afya inatambua mchango wao mkubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI”. Amesema Waziri Ummy
Home »
» VIFAA VYA KUJIPIMA UKIMWI MILIONI 1.6 VIMESAMBAZWA NCHINI
VIFAA VYA KUJIPIMA UKIMWI MILIONI 1.6 VIMESAMBAZWA NCHINI
Related Posts:
“KINA MAMA EPUKENI KAUSHA DAMU” MHE. UMMYNa Mwandishi wetu –Kilimanjaro Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewatahadhalisha wanawake kutochukua mikopo i… Read More
KATIBU WA CCM PILI MBAGA AMEWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAPUUZA WAPOTOSHAJI WA BANDARI Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE … Read More
MKUU WA MKOA SENYAMULE AMELIPONGEZA SHIRIKA LA DASPA KWA KUZALISHA MBEGU BORA Mhe.Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule amelipongeza Shirika la DASPA kwa kuwa wazalishaji wa mbegu bora ikiwa ni njia nzuri ya kuimarisha maisha ya mkulima kwa kumpatia lishe na kipato.Mhe.Senyamule ameyasema hayo wakati w… Read More
ZAO LA MTAMA LA MACIA LILIMWE KWA WINGI ILI KUONDOKANA NA BAA LA NJAA Na.Kadala Komba Dodoma Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma (JUWACHA) na Shirika la Uzalishaji Mbegu DASPA Janeth Nyamayahasi amesema kuwa tukililima vizuri zao la mtama la macia … Read More
WAKULIMA WASHAURIWA KULIMA KWA KUTUMIA VIFAA VYA KISASA. Na Moreen Rojas,Dodoma.Wakulima nchini washauriwa kulima kwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati.Hayo yameelezwa na Ndg.Ramadhani Mrutu ambaye ni Afisa mauzo kutoka kampuni ya Rel… Read More
0 Comments:
Post a Comment