Wadau wanaoshughulika na malezi na makuzi ya watoto wametakiwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya Programu Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT -MMMAM) ili kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto wa Mkoa wa Dodoma
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu wakati wa ufunguzi kikao cha wadau hao kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo Septemba 14, 2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kujadili afua mbalimbali za namna ya kuboresha malezi na makuzi ya watoto.
"Mradi huu unagusa maeneo tofauti tofauti ikiwemo lishe ya Mtoto, malezi kuanzia ujauzito hadi miaka 8 na fursa za ujifunzaji wa malezi ya awali ya Mtoto. Dodoma ina takribani wadau 410 wanaoshirikiana na Serikali katika kufanikisha program hii, hivyo ni muhimu kushirikiana kwani bado hatujafanya vizuri kama Mkoa kwenye takwimu za lishe kwa watoto" Amesema Bw. Gugu
Aidha, ameongeza kwa kuwaasa kina mama na walezi kuzingatia nafundisho ya lishe yanayotolewa na wataalamu kuanzia kipindi cha ujauzito hadi malezi ya Mtoto.
" Kwa kipindi cha 2022/2023 jumla ya kina mama / walezi 191,662 kati ya 200,981 walio na watoto wenye umri wa miezi 0 - 23 walipewa unasihi juu ya ulishaji wa watoto uliofanywa na watoa huduma ya afya sawa na asilimia 104.60 hii ninaonyesha ni kwa namna gani unapomlinda mtoto kwa kumpa lishe bora, itasaidia katika makuzi yake" Ameongeza Bw. Gugu.
Akizungumzia lengo kuu la kikao hicho, Mratibu wa Malezi na makuzi ya watoto Bi. Stella Matemu amesema,
" Lengo kuu la kikao hicho ni kuwatambua wadau pamoja na kujadili afua mbalimbali zinazopatikana kwenye mradi huu ulioazinduliwa rasmi mwaka 2021 kitaifa ambapo kwa Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa Septemba 2022 ukihusisha maeneo matano ambayo yanahusiana na malezi na makuzi ya Mtoto kuanzia miaka 0 - 8 nayo ni Elimu, afya, lishe , malezi na mwitikio." Bi. Matemu
Hata hivyo, mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Watoto na Makundi maalumu Bw. Joel Mwakapala amesema kuwa asilimia 90 ya ubongo wa mtoto unakua akiwa katika umri wa miaka 0 hadi 8 huku akielezea namna program hii inavyoleta matokeo chanya kwa jamii.
" Uwepo wa program hii umesaidia kuboreshwa kwa mazingira wezeshi ya kufanya uratibu wenye ufanisi na pia mifumo ya utoaji huduma Jumuishi za MMMAM na uthibiti ubora imeimarishwa" Amesema Bw. Mwakapala.
MWISHO
Home »
» WADAU WA MALEZI YA WATOTO WAKUTANA KUBORESHA MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO
WADAU WA MALEZI YA WATOTO WAKUTANA KUBORESHA MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO
Related Posts:
MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa August 26 2022MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa August 26 2022/Newspaper Front pages for August 26th 2022 … Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 25, 2022… Read More
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI [CCM] DANIEL CHONGOLO TAYARI NAE AMEHESABIWAKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Faith Buruhani (kushoto) wakati wa kuhesabiwa kwenye makazi yake Msasani jijini Dar es salaam leo tarehe 23,… Read More
SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKABILI MAAFA.Na Mwandishi wetu- Dodoma. Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika mapambano dhidi ya maafa ambayo hujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha athari. Hayo yameelezwa na Mkurug… Read More
NAIBU WAZIRI UMMY NA MUMEWE WAHESABIWANaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy nderiananga ,mumewe pamoja na wanafamilia wamekwisha hesabiwa . wewe je Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt… Read More
0 Comments:
Post a Comment