Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha wahandisi wazawa wanashiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali nchini.
Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Tanzania, unaolenga kupunguza ukosefu wa ajira kutoka 9% hadi 8% ifikapo 2025/26, Serikali inatarajia kutimiza azma yake ya kuhakikisha inazingatia ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya ujenzi ili kukuza ujuzi.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi Septemba 14, 2023) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya siku wahandisi, katika ukumbi wa Mlimani city, Dar es Salaam.
“Wizara ya Ujenzi pamoja na bodi ya wahandisi inalifanyia kazi suala la ushiriki mdogo wa wazawa katika miradi ya maendeleo, hii ni changamoto ambayo mmeiibua, Serikali sasa imeliweka kwenye mpango wa kuhakikisha changamoto inafanyiwa kazi ili kuongeza idadi ya wazawa kushiriki katika kazi za ndani”
Amesema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha wahandisi wazawa wananufaika kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali “miradi hii ni fursa kwenu, natoa rai mjipange na kufanya juhudi za makusudi kila mmoja kwenye eneo lake ahakikishe kwa uzalendo alionao na mapenzi kwa nchi yake kuwa kinara katika sekta unayosimamia ili kulijenga taifa letu”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi iandae mpango mahsusi wa kuwaendeleza wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa kwa wingi zaidi wanapohitimu masomo “Suala hili litekelezwe kwa ushirikiano na wadau wengine wa uhandisi”
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenye amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi katika sekta mbalimbali za kiuchumi kupitia uanzishaji wa viwanda, uendelezaji wa miundombinu ya kilimo, nishati, maji, uvuvi, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano
“Katika mwaka 2023/2024 Serikali imetenga miradi maalum ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa ajili ya wakandarasi wanawake, ambao zabuni zitashindanishwa kwa makandarasi wanawake tu”
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Mhandisi Menye David Manga Amesema kuwa bodi inatarajia kufanya mageuzi makubwa ya teknolojia ili kuhakikisha wahandisi waliosajiliwa na wenye sifa wanakuwepo wa kutosha kwa ajili miradi mbalimbali nchini ili kujenga dhana halisi ya ushirikishwaji wa wazawa ‘local content’ “Tutakuwa na mageuzi katika sheria na kanuni zetu ili kuongeza usajili wa wahandisi”
Home »
» MAJALIWA : ONGEZENI USHIRIKI WA WAHANDISI WAZAWA KWENYE UJENZI MIRADI
MAJALIWA : ONGEZENI USHIRIKI WA WAHANDISI WAZAWA KWENYE UJENZI MIRADI
Related Posts:
WATU 12 WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI DODOMADodoma WATU 12 wamepoteza maisha baada ya basi a Frester lililokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar es salaam kugongana uso kwa uso na Lori la Texas majira usiku wa kuamkia leo. Ajali hiyo imetokea eneo Kiiji Cha Silwa wilaya… Read More
RC KINDAMBA AWATAKA MA-DED KUSIMAMIA UKUSANYAJI FEDHA Na. Mwandishi wetu Songwe Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo wasimamie fedha zinazokusanywa zipelekwa benki ili kuepuka wakusanyaji kuzitumia fedha hizo. Mkuu huyo… Read More
DK.SWEKE: BAHARI KUU IPO SALAMA TUNATUMIA NDEGE KUFANYA DORIA Na. Kadala Komba Dodoma. MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,ameeleza kuwa katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutum… Read More
PROF.MKENDA :BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA KWA WANAFUNZI NA WASIMAMIZI WA MITIHANI KIDATO NNE MWAKA 2022 .Na. Mwandishi wetu Dodoma SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imesema imedhamiria kukomesha vitendo vya wizi wa mitihani huku ikiridhishwa na uamuzi wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa wanafunz… Read More
NSSF IMEJIPANGA KUANZA KUTOA MAFAO KWA SEKTA ISIYO RASMI Na. Kadala Komba Dodoma. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)umewataka wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huo kwa kupeleka michango yao na hatimaye kuwa kwenye mfumo wa mafao hali itakayosaidia kupun… Read More
0 Comments:
Post a Comment