Na. Mwandishi wetu
Kumekuwa na malalamiko mengi ya watumishi kukaimishwa ofisi pasi kuwa na sifa zinazotakiwa kuwezesha kukaimu nafasi hizo na hivyo kusababisha matatizo mengi kwa watumishi ikiwemo kushinda kupanda vyeo na kukosa posho za madaraka. Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayesimamia Utumishi na Utawala Bora, Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri huyo ambaye yuko kwenye ziara Mkoani hapo aliyasema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wakati akizungumza nao. Pamoja na hoja mbalimbali , Naibu Waziri alitumia nafasi hiyo ya kikao kuwapongeza Watumishi wa Wilaya hiyo kwa kazi nzuri wanazozifanya hasa katika kusimamia kazi wanazozifanya na fedha za miradi mbalimbali zinazoletwa na Serikali katika maendeleo ya Wilaya hiyo ikiwemo fedha za ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa jengo la utawala Halmashauri, zahanati nk. Ziara hiyo inaendelea wilaya
0 Comments:
Post a Comment