Na Timotheo Mathayo, Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasihi Wafanyabiashara wa mafuta ya dizeli na Petroli nchini kuwa waaminifu wakati wakiendelea kutoa huduma kwa Watanzania.
Dkt. Biteko ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa EWURA jijini Dar es Saalam Septemba 14, 2023 na kukukumbushia kuwa, pamoja na kuwa ni Wafanyabishara lakini pia wanatoa huduma kwa Wananchi.
‘’Naomba Wafanyabiashara wenye leseni za biashara ya mafuta nchini watambue kuwa wana wajibu wa kuhudumia watanzania ili wapate bidhaa hiyo, tunajua kuwa kiwango cha uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kimepungua lakini Serikali inaendelea kulifanyia kazi,” amesema Dkt. Biteko.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko amesema, Serikali inafanya kazi kubwa ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa mafuta nchini inamalizika.
Dkt. Biteko ameitaka EWURA kuhakikisha inapitia mfumo mzima wa upangaji wa bei ya mafuta ili kuwezesha bei zinazopangwa zilingane na uhalisia wa maisha.
“Wazalishaji wa mafuta duniani wamepunguza uzalishaji lakini mahitaji ya mafuta yameongezeka kwa sababu ya shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa ikiwemo ununuzi wa magari na ujenzi wa viwanda vya kuzalisha malighafi mbalimbali,” amesema Dkt. Biteko.
Aidha, amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo Serikali imeanza kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya Gesi Asilia - CNG ili kuhamasisha wananchi kuanza kutumia magari yanayotumia mfumo wa Gesi Asilia ikiwemo magari ya Serikali.
Amefafanua kuwa faida zitakazopatika kama magari yaliyokuwa yakitumia mafuta yakianza kutumia mfumo wa uendeshaji unaotumia Gesi Asilia - CNG, gharama za uendeshaji wa magari hayo zitapungua na mafuta yaliyokuwa yakitumiwa na magari hayo yatatumika kuendesha mitambo iliyopo viwandani.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na watendaji wengine kutoka wizara ya Nishati na EWURA.
Home »
» DKT. BITEKO AWASIHI WAFANYABIASHARA WA PETROL NA DIZELI KUWA WAAMINIFU.
DKT. BITEKO AWASIHI WAFANYABIASHARA WA PETROL NA DIZELI KUWA WAAMINIFU.
Related Posts:
WALIMU WA SHULE BINAFSI NA SERIKALI WAMEUNGANA KWA PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO MASHULENINa. Kadala Komba Dodoma Mwenyekiti wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Ester Manyanda Akizungumza na Waandishi wa Habari lengo la kukutana pamoja Walimu wa Shule Binafsi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Do… Read More
JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWANa Kadala Komba- Dodoma JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWA Jamii imeaswa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya utumiaji dawa za binadamu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo usu… Read More
PESA INAWEZA KUWA MBARAKA AU LAANA*Pesa si laana yenyewe kama yenyewe; bali ni kitu chenye thamani kubwa kwa sababu ikitumiwa ipasavyo, inaweza kufanya mema katika kuleta wokovu wa roho za watu, katika kuwabariki wengine ambao ni maskini kuliko sisi wenyewe. … Read More
SHULE YA VIPAJI NCHINI FOUNTIN GATE KUWATAMBULISHA WACHEZAJI KWA MSIMU WA 2022 \2023 Na. Kadala Komba Dodoma Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Mtendaji Mkuu wa Shule ya vipaji ya Fountion Gate Thabiti Kandoro Amesema tupo kwenye maandalizi ya uzinduzi wa Mpango w… Read More
“MBEYA INAENDA KUFANANA NA HADHI YA MAJIJI, TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA” DKT. TULIA*Na. Mwandishi Wetu Mbeya Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi wa Mbeya Mjini kumshukuru na kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa… Read More
0 Comments:
Post a Comment