Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.
Dotto Biteko aendelee kushughulikia suala la changamoto ya upatikanaji
wa nishati ya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini.
“...Watanzania
wapate hii huduma, upatikanaji huu ni muhimu kuhusisha taasisi zote za
mafuta na wanunuaji mafuta kwa pamoja ‘bulk’ wakae pamoja na Wizara
zinazohusika ikiwemo Wizara ya Fedha na Idara ya Ofisi ya Uratibu Ofisi
ya Waziri Mkuu waone namna ya upatikanaji wa mafuta.”
Ametoa
maagizo hayo leo (Alhamisi, Septemba 7, 2023) wakati akijibu swali la
Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi katika kipindi cha maswali kwa Waziri
Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Mbunge huyo alitaka kufahamu ni upi mkakati
wa Serikali katika kuhakikisha Taifa linakuwa na mafuta ya kutosha.
“Lakini
pia tupanue wigo wa waagizaji wa mafuta ili tuwe na mafuta mengi
nchini kwa usalama wa Taifa letu. Na kama hili litafanyika ndani ya wiki
moja tutakuwa tumeshapata majibu na kuwapa taarifa
Watanzania.Tutahakikisha nishati hii ya mafuta inapatikana na Naibu
Waziri Mkuu atashughulikia hilo.”
Wakati huo huo, Waziri Mkuu
ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI iendelee na utaratibu wa kubaini maboma
yote kwenye sekta ya afya na elimu ambayo waliyajenga na
hayakukamilika, wahakikishe wanaendelea kutenga fedha kwa ajili ya
kuyakamilisha kwa sababu yametokana na bajeti zao.
Waziri Mkuu
amesema suala la ujenzi wa miradi ya elimu au afya ambayo inahusisha
majengo ni mkakati ulioelekezwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa
kupitia fedha zinazopelekwa kutoka Serikali Kuu ambazo zinapelekwa
kujenga majengo hayo kwa thamani ya jengo kutokana na makadirio
waliyoyatoa, hivyo wanatakiwa wasimame ujenzi ukamilike kama
ilivyokusudiwa.
Aidha, Waziri Mkuu amesema chanzo kingine ni
fedha inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri zenyewe ambapo wao
hupanga mipango ya maendeo yao kupitia bajeti yao na kwenda kujenga,
maboma mengi yanatokana na mipango yao, hivyo wayakamilishe.
“Uzoefu
tulioupata wakati wa ukaguzi wa miradi hii, majengo ambayo
yametekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu yamekwenda kama yalivyo na
pale ambapo hayakukamilika hatua kali zimechukuliwa. Sasa kwa kuwa
maboma mengi yanatokana na mipango yao na kushindwa kuyaendeleza,
mkakati wa Serikali ni kuhakikisha maboma yote yanakamilika.“
Ametumia
fursa hiyo kuziagiza zifanye tathmini ya miradi yake ione maeneo gani
ambayo walianza miradi na wameshindwa kukamilisha na yamebaki maboma ili
wapange bajeti ya kila mwaka kuhakikisha maboma hayo yanakamilika.
“Halmashauri haziwezi kushindwa kupata shilingi milioni 50 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa zahanati.“
Ameyasema hayo wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga aliyetaka kujua ni nini
mpango wa Serikali katika kuhakikisha inakamilisha maboma ya kutolea
huduma za elimu na afya nchini, miradi iliyoanzishwa na Serikali na
nguvu za wananchi ili wananchi hao waweze kuona thamani ya nguvu yao na
ya fedha za Serikali zinazopelekwa katika maeneo yao.
Home »
» WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA NAIBU WAZIRI MKUU CHANGAMOTO YA MAFUTA
WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA NAIBU WAZIRI MKUU CHANGAMOTO YA MAFUTA
Related Posts:
WATU 12 WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI DODOMADodoma WATU 12 wamepoteza maisha baada ya basi a Frester lililokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar es salaam kugongana uso kwa uso na Lori la Texas majira usiku wa kuamkia leo. Ajali hiyo imetokea eneo Kiiji Cha Silwa wilaya… Read More
DK.SWEKE: BAHARI KUU IPO SALAMA TUNATUMIA NDEGE KUFANYA DORIA Na. Kadala Komba Dodoma. MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Dkt.Emmanuel Andrew Sweke,ameeleza kuwa katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutum… Read More
PROF.MKENDA :BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA KWA WANAFUNZI NA WASIMAMIZI WA MITIHANI KIDATO NNE MWAKA 2022 .Na. Mwandishi wetu Dodoma SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imesema imedhamiria kukomesha vitendo vya wizi wa mitihani huku ikiridhishwa na uamuzi wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa wanafunz… Read More
RC KINDAMBA AWATAKA MA-DED KUSIMAMIA UKUSANYAJI FEDHA Na. Mwandishi wetu Songwe Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo wasimamie fedha zinazokusanywa zipelekwa benki ili kuepuka wakusanyaji kuzitumia fedha hizo. Mkuu huyo… Read More
NSSF IMEJIPANGA KUANZA KUTOA MAFAO KWA SEKTA ISIYO RASMI Na. Kadala Komba Dodoma. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)umewataka wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huo kwa kupeleka michango yao na hatimaye kuwa kwenye mfumo wa mafao hali itakayosaidia kupun… Read More
0 Comments:
Post a Comment