Subscribe Us

WOWAP WATOA FEDHA TASLIMU KWA WANAFUNZI IKIWA NI MWENDELEZO WA KUSAIDIA WATOTO WA KIKE


Na. Kadala Komba Chemba

 

Mratibu wa Miradi Women Wake Up(WOWAP) Nasra Sulemani amesema Shirika linajihusisha na utetezi wa haki za wanawake na Watoto pamoja na kuwawezesha watoto  vifaa mbalimbali ambavyo huwa tunatoa kwa awamu tofauti kama tulivyofanya katika shule zingine tumetoa mabegi, taa kwa wale wasio na umeme na chupa za kubebea maji pia tunategemea Watoto hao watakua ni wanufaika wa mradi huo ambao wanaenda kuuanza katika shule hiyo kwaiyo kupitia mradi huo tunaomba ushilikiano wenu  wananchi na wadau mbalimbali kutoa matokeo mazuri ya mtoto Alisema.

Mratibu Nasra ameyasema hayo alipokuwa kwenye sherehe za kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba Wilaya ya Chemba shule ya msingi kelema Balai ikiwa ni mwendelezo wa kutoa Eilimu kwa wazazi namna ya bora ya kuwasaidia Watoto wa kike, leo tumekusanyika hapa kwajili ya shughuli ya maafali ya Watoto wetu kama shirika tumeona ni vyema na sisi kuwa sehemu ya sherehe hizi kwa kuchangia kiasi cha fedha taslimu Elfu Hamsini (50,000 ) ambayo tutamkabidhi mkuu wa shule hii Khalfan Hassan  Pamoja na boksi la Biskuti kwa wahitimu wa darasa la saba.

“Tukiwa kama wadau na watetezi wa Watoto wa kike kupitia mradi huu hapa wilaya ya Chemba na kata zake tumekuwa tukifanya hivi  takribani miaka mitatu  katika shule mbalimbali katika kata mbalimbali kwa awamu tunaona mahitaji yameongezeka kata zimeongezeka wahitaji wameongeza kata ambazo zimeongezeka ni Pranga,Soya kupitia kata hizi tumechangua shule ya Kelema Balai kama shule ya kuanza nayo tunategemea  kwamba katika shughuli za utekelezaji wa mradi tutafanya kazi kwa karibu sana na Watoto wa shule hii kwa kuanzisha klabu ya shule kupitia klabu  watawapa mafunzo ambayo yatawajenga katika namna ambayo wataendelea kukaa shule kwa muda unaoitajika”

Sambamba na hilo Mratibu wa Miradi Women Wake Up Nasra Sulemani amesema tunatengemea kupata matokeo mazuri sehemu zote ambazo zimepitiwa na mradi ,  tunasema hivi kwa sababu maeneo ambayo tumefanya mradi tumepata matokeo makubwa ambayo yametupa nguvu ya kusonga mbele kwenye maeneo mengine,  tumeona Watoto walio pata elimu kupitia mradi  wamefanya vizuri sana katika matokeo yao ya mitihani lakini pia wamejengewa uwezo mzuri wa kujiamini na kujieleza kwasabau wamefanikiwa kuwapeleka kwenye platform mbalimbali ambazo ni za kitaifa na kimataifa na kuwakutanisha na watu muhimu ambao wanaweza kuwajenga wengine walipata nafasi ya kuwenda Bunge na kuhuzulia vipindi mbalimbali vya Bunge, wameenda kwenye mikutano mbalimbali ya kimataifa Dar es salaam, kwaiyo wanategemea kwamba kadri wanavyoendelea kufanya mambo hayo tunaenda kuyafanya na Watoto wa shule hii hivyo basi tunatamani sana wazazi washiriki  ili kuona namna gani wanakua ni sehemu muhimu sana ya kusimamia maswara hayo wanayoenda kuyafanya alisema .

 Kwaupande wake Mwzeshaji wa mradi Luhaga Makunja Miradi Women Wake Up(WOWAP)  ameipongeza shule ya msingi Kelema kwa kuendelea kuwasapoti wanafunzi kwenye vipaji leo tumeona Watoto wadogo walivyoonesha vipaji vyao inamaamisha Kelema kwa siku zijazo tutakuwa na watu wakubwa na tegemezi kwenye nchi yetu ila  kama watawatunza Watoto hawa vizuri  wataleta mabadiliko makubwa sana, itakuwa ni ajabu miaka 15 mbele kusikia shule hii ya  Kelema hakuna madaktari au viongozi wakubwa wanaotoka kwenye shule hii.

 “hili safari ya hawa Watoto Kwenda kutimiza ndoto zao  hususani Watoto wa kike sio rahisi kama wanavyoichukulia wanasema wamekuwa na vikwazo wao kuweza kutimiza ndoto zao na kila mtoto anandoto na kipaji lakini wanapoanza safari za ndoto zao wanakutana na vikwazo vingi hususani Watoto wa kike wengi wanakatiza masomo”

Mwzeshaji wa mradi Luhaga alisema  leo hii itasikitishwa sana  tutakaporudi miaka miwili na kusikia yule binti aliekua anaongea pale sana ameacha shule,  Lengo kubwa la sisi kufika hapa ni kuhamasisha wazazi na jamii kuchukua hatua kuweza kupunguza hivyo vikwazo ambavyo vinafanya hao Watoto wanaacha shule na Kwenda kuishi Maisha ya utu uzima kabla ya umri wao.

Mratibu wa Miradi Women Wake Up(WOWAP) Nasra Sulemani akizungumza na wazazi kwenye mahafali ya darasa la saba 


 

Mwzeshaji wa mradi Luhaga Makunja Miradi Women Wake Up(WOWAP)
Mkuu wa shule ya msingi  kelema Balai Khalfan Hassan 




MATUKIO YA PICHA WANAFUNZI SHULE YA KELEMA

 

0 Comments:

Post a Comment