Na. Mwandishi wetu – Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kujiepusha na athari za kuwa kwenye kumbukumbu mbaya za utumishi wao.
Aidha, amesema kuwa hali hiyo inakwamisha jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi na kushiriki katika ujenzi wa taifa.
Mhe. Katambi amesema hayo Septemba 8, 2023 Bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini Costantine John Kanyasu lilihoji, Serikali inatambua utaratibu wa Mgodi wa GGML wa ku-blacklist vijana nchini na ni vijana wangapi wapo blacklisted.
Akijibu swali hilo, Mhe. Katambi, amesema Serikali imewahi kupata malalamiko kuhusu vijana ambao wamesitishiwa ajira zao katika mgodi huo na ufuatiliaji uliofanyika haukubaini suala hilo.
Amesema kilichobainika ni kuwa mgodi huo umeweka utaratibu wa kutunza taarifa za kiutendaji na mienendo ya wafanyakazi wake ikiwemo matendo na matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu ambayo mfanyakazi anakuwa amefanya katika kipindi cha ajira yake.
Kwa upande mwengine, Mhe. Katambi amewataka vijana ambao wana uhakika utumishi wao katika Mgodi huo bila dosari na wanaweza kuthibitisha kuwa wamekuwa black-listed, kuwasiliana na Ofisi yake ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
MWISHO
Home »
» MHE. KATAMBI VIJANA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU NA UAMINIFU
MHE. KATAMBI VIJANA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU NA UAMINIFU
Related Posts:
MKURUGENZI WA MASHTAKA MWAKITALU AMETEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA DODOMANa. Mwandishi wetu Dodoma Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ametembelea Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Maafisa wa Magereza katika kuwatunza wafungwa… Read More
“UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU“UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU NA MWANDISHI WETU - DODOMA Watafiti wa masuala ya kilimo nchini wametakiwa kutumia matokeo ya utafiti wao wanaofanya katika kuboresha mbegu bora za mazao zinazoendana na … Read More
JAMII YAHIMIZWA KUPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI.Na mwandishi wetu- Dodoma JAMII YAHIMIZWA KUPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ameitaka jamii, wadau na kila mmoja kwa nafasi yake kupaza sauti dhidi ya v… Read More
ASKOFU DKT CHANDE AMETOA MSAADA KWA YATIMA NA WAJANE DODOMA Askofu Dkt Evance Chande wa Kanisa la Karmeli Assemblis Of God la jijini Dodoma Leo ni siku muhimu Kwa watoto yatima,wajane na waishio katika mazingira magumu kupatiwa misaada mbalimbali kutoka. ujumbe Dini… Read More
WACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASAWACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASA. Wachakataji wa mazao ya uvuvi nchini wametakiwa kutumia fursa ya teknolojia katika shughuli zao ili kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi na kukabiliana na upotevu wa m… Read More
0 Comments:
Post a Comment