Mratibu wa Miradi Women Wake Up(WOWAP) Nasra Suleimani ameiasa jamii
kuhakikisha wanasaidia kutimiza ndoto za watoto wa kike ikiwa ni pamoja
na kutokomeza mimba za utotoni na vikwazo vyote ambavyo vinamkuta mtoto
wa kike katika kukwamisha ndoto zake za kufikia kielimu.
Bi.Nasra
ameyasema hayo wilaya ya chemba katika kijiji cha kwamtoro kata ya
kwamtoro kwenye mkutano wa nje na Wazazi wa kijiji hicho kwa lengo la
kuhamasishaji jamii pamoja na kuwapatia Elimu namna bora ya kuwasaidia
watoto wa kike kutimiza ndoto zao kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa
ujumla.
"Tumekuwa tukiufanya mradi huu kwa nguvu kubwa katika
mashule lakini kutoka na ambavyo tumekuwa tukipata mrejesho kutoka kwa
wanafunzi namna ambavyo wazazi wamekuwa hawana ukaribu na watoto wao,
hivyo tukasema tunahaja ya kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kuwafikia
wazazi hivyo leo tuko hapa kuhakikisha tunaongea na wazazi na tumefanya
mkutano wa hadhara na wazazi na wamepata elimu vizuri na tunategemea
basi kupitia elimu hii waliyoipata leo wataenda kuwa sehemu ya chachu ya
kuhakikisha kwamba wanaweza kuzifanyia kazi zile changamoto za mtoto wa
kike ambazo wanazipata katika majumba yao na katika ngazi ya familia
ili kuhakikisha mtoto wa kike anafanya vizuri katika kutimiza ndoto
zake" Amesisitiza Bi.Nasra
Aidha ametoa Wito kwa jamii
kuhakikisha wanalea watoto wa kike vizuri kwani suala la malezi sio la
shule peke yake wala mashirika peke yake bali wazazi ndio watu wa kwanza
kabisa na wao ndio wanatumia nafasi kubwa ya kuaminika na watoto hivyo
imani yangu kupitia mkutano huu utaleta mabadiliko makubwa na watoto
watakuwa wamefurahi kwani ni sehemu ambayo wamekwenda kutekeleza zile
changamoto ambazo wamekuwa wakiwaletea katika mradi huu tangu wameuanza.
Kwa upande wake Luhaga Makunja ambaye ni mwezeshaji women wake
up amesema kuwa dhumuni la mkutano huo ni kuwahamasisha wazazi kutatua
vikwazo vinavyosababisha watoto wadogo hususani ni wasichana kukatiza
masomo yao ambapo wameweza kuongelea vikwazo vilivyopo katika jamii
wanaposhindwa kuwaunga mkono watoto wa kike waliokatisha masomo
kutokana na ujauzito ambapo hivi sasa sharia inawaruhusu kuendelea na
masomo baada ya miaka miwili lakini bado changamoto kubwa imekuwa upande
wa wazazi na jamii.
"Kumekuwa na dhana mbaya kwa jamii na
mtazamo hasi kwa jamii kwamba mwanafunzi ambaye alishapata mimba
anaporudi shuleni kunakuwa na mazingira yakukatisha tamaa wenzao
kuwazomea na kukosa mahitaji muhimu na kuweza kuboresha mazingira ya
shuleni ili waendelee na masomo na kutimiza ndoto zao"
Aidha
ameongeza kuwa wazazi wanaunga mkono hili jambo ila wanashauri Serikali
kuwatengea shule maalumu na madarasa maalumu ili kuepuka mazingira
ambayo yanafanya washindwe kuchangamana na wale wanafunzi wengine ambao
wako shuleni hivyo wazazi wamesema watahimizana kuweza kuwafikia watoto
wa kike mashuleni ikiwa ni nia ya kutoa elimu kuhusiana na stadi za
maisha na kuweza kuchukua hatua stahiki na kuweza kuepuka mimba
zisizotarajiwa na makundi yanayoweza kuwapotosha.
Sambamba na
hilo Afisa Mtendaji wa kata ya kwamtoro Evaresto Mahenge amesema
wanaishukuru team ya women wake up kwa mafunzo waliyofanya kwenye kata
yake anaimani yatawasaidia watoto wa kike kufikia ndoto zao
kielimu,elimu hii itaenda kuwa chachu kwa wazazi kwa sababu elimu hii
imewahamasisha wazazi hivyo wataenda kupambana kuhakikisha wanamsimamia
mtoto wa kike katika harakati zake za masomo,itakuwa ni chachu kwa
wanafunzi wengine ambao waliacha shule kwa muda kutokana na changamoto
mbalimbali ambao watafutiliwa na kurudishwa mashuleni na kutimiza
malengo yao.
Kwa upande wake Mwasiti Issa ambaye ni mzazi katika
kijiji cha kwa mtoro amelishukuru shirika la women wake up kwa kutoa
elimu ya kuelimisha watoto wa kike kujizua kujihususha na anasa pamoja
na mambo mabaya na kuhakikisha wanongea nao na kuwakusanya kuongea nao
na kuwaelimisha madhara ya mimba za utotoni.
Sanjari na hayo
Tizo Wambura ambaye ni mkazi wa kijiji cha kwamtoro ambaye pia ni
mwanakamati wa shule ya msingi kwamtoro wamelishukuru shirika hilo kwa
semina ya malezi au makuzi ya mtoto wa kike katika jamii na kama
kiongozi anaahidi kuendelea kutoa semina mashuleni lakini pia mahali
popote ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa watu katika viahatarishi ambapo
wakipata elimu hii itaweza kuwasaidia na kuweza kuijenga jamii iliyo
bora.
Mratibu wa Miradi Women Wake Up (WOWAP) Nasra Suleimani akizungumza na wazazi wilaya ya Chemba katika kijiji cha kwamtoro kata ya kwamtoro kwenye mkutano |
Mratibu wa Miradi Women Wake Up (WOWAP) Nasra SuleimaniAkiwa amesimama mkono wake wa kushoto ni Alwino Alois Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwamtoro na kulia kwake ni Hassan Hussen Mwenyekiti wa mtaa wa kwamtoro akifatiwa na Afisa Mtendaji wa kata ya kwamtoro Evaresto Mahenge mwisho kabisa ni Luhaga Makunja ambaye ni mwezeshaji women wake up
Wazazi wakichangia jambo kwanye mkutano wa Shirika la Women Wake Up
0 Comments:
Post a Comment