Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Chuo kikuu huria(open university) ndio chuo kinachotengeneza watu wenye uwezo kwani watu wanaosoma huku asilimia kubwa wanauwezo wa kuchanganua changamoto mbalimbali.
Hayo yameelezwa na Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati akizungumza na jumuiya ya wahitimu wa chuo kikuu huria jijini Dodoma.
"Uzuri wa chuo kikuu huria kila mmoja ni mwalimu wa mwenzake na aliyesoma chuo kikuu huria uwezi kumfananisha na mtu mwingine yeyote sababu huku unafundishwa kujitegemea kwa kutafuta material na mazingira hayo hayo ndio unayokutana nayo kazini hivyo inatengeneza viongozi imara zaidi" Amesisitiza Mhe.Simbachawene
"Wakati nataka kuwa mwanasiasa niliona elimu niliyokuwa nayo pekee haitoshi hivyo nikawa natafuta namna ya kuweza kujiendeleza na dhamira yangu ilikuwa kuwa mwanasheria ndipo nikaambiwa kuwa open university ndio sehemu pekee nayoweza kujiendeleza bila changamoto yoyote ile na niliposajiliwa kozi yangu nilifanya kwa miaka 3 kusema ukweli chuo kikuu huria kimekuja kutusaidia viongozi na walala hoi na hii leo kupitia chuo kikuu huria mimi ni wakili na mambo mengine yakiisha naweza kurudi kwenye taaluma yangu"
Aidha ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita itakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zote za chuo kikuu huria hivyo na yeye kama Waziri mwenye dhamana ataangalia namna ya kuchangia eneo la chuo kupata makao makuu ya nchi Dodoma hivyo amewahakikishia kumaliza suala hilo.
Naye Musa Sima mbunge wa singida mjini ambaye pia ni mhitimu wa masters ya uongozi na utawala bora amesema kwamba taaluma inayotolewa na chuo kikuu huria ni taaluma bora kwani amenufaika sana na kimekuwa msaada mkubwa kwa watanzania kwani wananchi wanaendelea na kazi huku wanasoma na angependa kuwashauri walioko makazini kwamba Maisha yanahitaji taaluma ya ziada na hutaipata sehemu nyingine yoyote zaidi ya chuo kikuu huria.
"Aidha kumekuwa na changamoto ya maprofesa kwani kuna mahali tunatakiwa kubadilika kutoka chini kwenda juu kama tunataka kupanda lazima tuwekeze kwenye sekta hiyo,lakini pia jamii haioni umuhimu kwani hawaoni matokeo ya tafiti zinazofanywa na wataaalamu wetu hivyo ningependa kuwashauri watafiti kushirikisha wananchi ili wawe sehemu ya tukio na kuona faida yake bila kusahau kuwahamasisha wanafunzi kujitegemea na waweze kujiajiri iikiwa ni pamoja na kujihusisha na Kilimo na ufugaji"Amefafanua Sima.
Kwa upande wake Mwenyekiti jumuiya ya chama cha wahitimu wa chuo kikuu huria Tanzania Almas Maige Mbunge wa jimbo la Tabora kaskazini Uyui amesema kuwa mkutano huu ni muendelezo wa majadiliano yaliyo bora,chuo kinapata namna bora ya kihakikisha kila mwanachama anachangia kwa namna yoyote ile iwe kifedha au kwenye miundombinu bora ili kuhakikisha chuo kikuu huria kinakuwa bora zaidi na kuwafikia watu wote ndani na nje ya nchi pamoja na kukidhi soko la ajira.
"Tunatambua kwamba wahitimu wengi ni wawekezaji na nilazima kujadiliana ni namna gani ya kutatua changamoto ya ajira ili kuhakikisha wahitimu wanaweza kuendelea na maisha mengine kwani tunatambua kwamba wahitimu kutoka chuo kikuu huria wengi wanakuwa tayari wameshaajiriwa ni wachache ndio huwa bado wanakuwa wanasoma huku hawana ajira mpaka kumaliza chuo hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kunakuwa na namna bora ya kuhakikisha kila mmoja ananufaika na chuo kikuu huria"Amesema Maige.
Chuo kikuu huria(Opening University) kimeanzishwa kikiwa na lengo la kuhakikisha kila mtanzania anapata haki ya elimu na kuweza kujiendeleza bila kikwazo chochote kile ili kutimiza ndoto za kila mmoja kufikia malengo yake.
Home »
» CHUO KIKUU HURIA NDIO CHUO KINACHOTENGENEZA WATU WENYE UWEZO.
0 Comments:
Post a Comment