Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

*GEITA TUPO NJIANI UWT MOTOO MOTOO*


*ZIARA YA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA BARAZA KUU LA UWT PAMOJA NA WAJUMBE WA NEC MKOA WA GEITA*

Ikiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Mary Chatanda na Makamu MNEC. Zainab Shomari ikiwa kwenye kivuko cha Busisi kuelekea mkoani Geita

*UWT IMARA. JESHI LA MAMA. KAZI IENDELEE.*





Naibu Waziri Nderiananga akutana na kufanya mazungumzo na RC Morogoro

 


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga  akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP)inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

SACP MISIME AWATAKA ASKARI POLISI KUBADILIKA KIFIKRA NA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI

 
Na, Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) David  Misime amefunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa,Wakaguzi na Askari wa Polisi kutoka Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma.

SACP Misime amewaeleza Askari hao kuwa mafunzo hayo ni mfululizo  wa mafunzo yanayotolewa kwa Askari  katika Vyuo ndani ya nchi, nje ya nchi na kazini kwa lengo la kuwabadilisha kifikra (mindset change) ili kutoa huduma bora kwa jamii.


SACP Misime amefungua mafunzo hayo Septemba 20, 2023   katika ukumbi wa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Yakifanyika kwa engo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu.


"Mkibadilika kifikra na kuhudumia wananchi kwa Nidhamu,Haki,Weledi na Uadilifu mtakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya wananchi kifua mbele na kwa kutumia Falsafa ya Polisi,wananchi waka waamini na kuongeza imani kwa Jeshi la Polisi ili waoneshe ushirikiano katika kubaini na kuzuia uhalifu".Amesema Misime.

Pamoja na hayo, Misime amewapongeza Askari kwa kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kazi kubwa wanayofanya huku akiwataka kwenda kuyafanyia kazi yale waliojifunza ili wananchi waweze kuona mabadiliko ya kifikra na  kiutendaji kulingana na mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi.

Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto  kutoka  Makao  Makuu  ya Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman amewasisitiza Askari wa Kike kuzingatia maadili, kutunza familia, kujijengea  uwezo wa kujiamini, kuwa wasafi na kuachana na vyanzo vyote vya mawazo kama vile kujiingiza katika mikopo isiyo na msingi ambayo muda mwingi huwapelekea kuwa ni watu wenye mawazo.

Hata hivyo, ACP Faidha Suleiman ambaye ni mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Makao makuu ya Polisi amewataka askari kuhakikisha wanafuata na  kutekeleza miradi ya Polisi Jamii katika majukumu yao ya kila siku kwani miradi hiyo inagusa kila kitengo cha Jeshi la Polisi.

Amesisitiza katika kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto katika familia zao na jamii kwa ujumla ikiwemo wao wenye kutokujifanyia ukatili.

Naye Mkuu wa Dawati la mtandao wa Polisi wananwake (TPF Net) Makao Makuu ya Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Eva Stesheni amewataka askari kujifunza namna ya kuandika ripoti ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi  pamoja na kuwasidia katika utunzaji wa kumbukumbu za nyaraka kwa kuwa na mpango kazi ulio mzuri ilikufikia malengo sahihi , Kuwasilisha taarifa, mawazo  na kuendeleza ujuzi  hususani kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto.





Picha na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi







CHUO KIKUU HURIA NDIO CHUO KINACHOTENGENEZA WATU WENYE UWEZO.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Chuo kikuu huria(open university) ndio chuo kinachotengeneza watu wenye uwezo kwani watu wanaosoma huku asilimia kubwa wanauwezo wa kuchanganua changamoto mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati akizungumza na jumuiya ya  wahitimu wa chuo kikuu huria jijini Dodoma.

"Uzuri wa chuo kikuu huria kila mmoja ni mwalimu wa mwenzake na aliyesoma chuo kikuu huria uwezi kumfananisha na mtu mwingine yeyote sababu huku unafundishwa kujitegemea kwa kutafuta material na mazingira hayo hayo ndio unayokutana nayo kazini hivyo inatengeneza viongozi imara zaidi" Amesisitiza Mhe.Simbachawene

"Wakati nataka kuwa mwanasiasa niliona elimu niliyokuwa nayo pekee haitoshi hivyo nikawa natafuta namna ya kuweza kujiendeleza na dhamira yangu ilikuwa kuwa mwanasheria ndipo nikaambiwa kuwa open university ndio sehemu pekee nayoweza kujiendeleza bila changamoto yoyote ile na niliposajiliwa kozi yangu nilifanya kwa miaka 3 kusema ukweli chuo kikuu huria kimekuja kutusaidia viongozi na walala hoi na hii leo kupitia chuo kikuu huria mimi ni wakili na mambo mengine yakiisha naweza kurudi kwenye taaluma yangu"

Aidha ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita itakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zote za chuo kikuu huria hivyo na yeye kama Waziri mwenye dhamana ataangalia namna ya kuchangia eneo la chuo kupata makao makuu ya nchi Dodoma hivyo amewahakikishia kumaliza suala hilo.

Naye Musa Sima mbunge wa singida mjini ambaye pia ni mhitimu wa masters ya uongozi na utawala bora amesema kwamba taaluma inayotolewa na chuo kikuu huria ni taaluma bora kwani amenufaika sana na kimekuwa msaada mkubwa kwa watanzania kwani wananchi wanaendelea na kazi huku wanasoma na angependa kuwashauri walioko makazini kwamba Maisha yanahitaji taaluma ya ziada na hutaipata sehemu nyingine yoyote zaidi ya chuo kikuu huria.

"Aidha kumekuwa na  changamoto ya maprofesa kwani kuna mahali tunatakiwa kubadilika kutoka chini kwenda juu kama tunataka kupanda lazima tuwekeze kwenye sekta hiyo,lakini pia jamii haioni umuhimu kwani hawaoni matokeo ya tafiti zinazofanywa na wataaalamu wetu hivyo ningependa kuwashauri watafiti kushirikisha wananchi ili wawe sehemu ya tukio na kuona faida yake bila kusahau kuwahamasisha wanafunzi kujitegemea na waweze kujiajiri iikiwa ni pamoja na kujihusisha na Kilimo na ufugaji"Amefafanua Sima.


Kwa upande wake Mwenyekiti jumuiya ya  chama cha wahitimu wa chuo kikuu huria Tanzania Almas Maige Mbunge wa jimbo la Tabora kaskazini Uyui amesema kuwa mkutano huu ni muendelezo wa majadiliano yaliyo bora,chuo kinapata namna bora ya kihakikisha kila mwanachama anachangia kwa namna yoyote ile iwe kifedha au kwenye miundombinu bora ili kuhakikisha chuo kikuu huria kinakuwa bora zaidi na kuwafikia watu wote ndani na nje ya nchi pamoja na kukidhi soko la ajira.

"Tunatambua kwamba wahitimu wengi ni wawekezaji na nilazima kujadiliana ni namna gani ya kutatua changamoto ya ajira ili kuhakikisha wahitimu wanaweza kuendelea na maisha mengine kwani tunatambua kwamba wahitimu kutoka chuo kikuu huria wengi wanakuwa tayari wameshaajiriwa ni wachache ndio huwa bado wanakuwa wanasoma huku hawana ajira mpaka kumaliza chuo hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kunakuwa na namna bora ya kuhakikisha kila mmoja ananufaika na chuo kikuu huria"Amesema Maige.

Chuo kikuu huria(Opening University) kimeanzishwa kikiwa na lengo la kuhakikisha kila mtanzania anapata haki ya elimu na kuweza kujiendeleza bila kikwazo chochote kile ili kutimiza ndoto za kila mmoja kufikia malengo yake.

MATUKIO KATIKA PICHA















*Tume yatangaza matokeo Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara*




Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali, Bw. Missana Kwangura amemtangaza Bi. Bahati Ndingo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 44,334 kati ya kura 56,095 halali zilizopigwa kwenye vituo 490 vya kupigia kura.

Bi. Ndingo amewashinda wagombea wengine 12 ambao walikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika jana tarehe 19 Septemba, 2023.

Kwenye uchaguzi huo ushindani mkubwa ulionekana ukiwa baina ya Bi. Ndingo na Bw. Modestus Kilufi aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, aliyepata kura 10,014.

Akitangaza matokeo hayo Wilayani Mbarali leo tarehe 20 Septemba, 2023 Bw. Kwangura amesema wapiga kura yalioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jimbo la Mbarali ni 185,836 ambapo kati yao 56,662 ndio waliopiga kura. Ameongeza kuwa kura halali ni 56,095 na kura zilizokataliwa ni 567.

Wengine waliokuwa wanagombea Ubunge kwenye Jimbo hilo na idadi ya kura walizopata ni Halima Abdalah Magambo (AAFP) aliyepata kura 336, Osward Joseph Mndeva (DP) aliyepata kura 130, Zavely Raurent Seleleka (UDP) aliyepata kura 158, Exavery Town Mwataga (CCK) aliyepata kura 118 na Morris Thomas Nkongolo (TLP) aliyepata kura 139.

Wengine ni Mary Moses Daudi (UPDP) aliyepata kura 113, Fatuma Rashidi Ligania (NLD) aliyepata kura 105, Bariki Oswald Mwanyalu (Demokrasia Makini) aliyepata kura 207, Hashim Abasi Mdemu (ADC) aliyepata kura 173, Mwajuma Noty Mirambo (UMD) aliyepata kura 113 na Husseni Hasani Lusewa kutoka Chama cha ADA- TADEA aliyepeata kura 155.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Francis Mtega kilichotokea tarehe 01 Julai, 2023 kwa ajali ya kugongwa na trekta dogo (power tiller).

Sanjari na uchaguzi huo wa Ubunge, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanya uchaguzi mdogo kwenye kata sita za Tanzania Bara ambapo matokeo yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa kata zilizofanya uchaguzi yanaonesha kuwa Bw. Helman Masila wa CCM ameshinda kwenye Kata ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Bw.  Kayombo Christopher Fabian ameshinda kwenye Kata ya Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Matokeo mengine yanaonesha kuwa Bw. Ng’wanza Venance Mathias ameshinda kwenye Kata ya Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw. Peter Dastan Massawe wa CCM ameshinda katika Kata ya Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Bw. Simon Rogath Massawe wa CCM ameshinda katika Kata ya Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Bw. Diwani Twaibu Ngonyani wa CCM ameshinda katika Kata ya Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Mwisho.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUIMBA WIMBO WA UCHOCHEZI.

 
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Sifa Bujune, Mkazi wa Isyesye mkoani Mbeya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijiji hapa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi.

Sifa Bujune pamoja na wenzake wanashikiliwa tangu Septemba 13, 2023 wakituhumiwa kuandaa wimbo uliopewa jina la “Tanzania Inaelekea Wapi?” unaodaiwa kuwa na maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali.

Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambole, amethibitisha kufikishwa Mahakaman8 kwa Mwimbaji Sifa Bujune na mtayarishaji wa muziki Hezekia George pamoja na wenzao kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.


MAJALIWA: TANZANIA KUWA WAZALISHAJI WAKUBWA WA NISHATI

 
 

 




WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Septemba 20, 2023  amefungua Kongamano la Tano na Maonesho ya Nishati Tanzania na amesema kwamba Serikali imedhamiria kuwa mzalishaji mkubwa na nishati.

“Tunaendelea na utafutaji wa gesi, tunataka tuwe wazalishaji wakubwa wa nishati, tuwe na umeme wa kutosha utakaopatikana kwa urahisi na nafuu na ziada tutauza nje ya nchi.“

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo baada ya kufungua kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Amesema kuwa Tanzania haitegemei kuzalisha umeme kwa kutumia maji pekee bali inaendelea kuweka mkazo katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati nyingine kama gesi na jua.

Waziri Mkuu amesema katika kongamano hilo la kimataifa la nishati ambalo limehusisha  viongozi na wadau kutoka katika mataifa mbalimbali Duniani litajadili namna bora ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nishati.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa kuzisisitiza nchi zote wanachama kuhakikisha taasisi za mafunzo zinatoa  programu maalum za mafunzo katika sekta za nishati ili kuongeza idadi ya watu walio na ujuzi na maarifa kwenye sekta hiyo.

Amesema kuwa nishati ni sekta muhimu katika kufikia lengo la uanzishwaji wa viwanda na katika kuimarisha na kuwezesha uzalishaji na shughuli nyingine za kiuchumi. “Lazima tufanye kazi kwa ushirikiano na wadau wote ili kufungua fursa kwa Watanzania wote.”

Amesema ili kuwaendeleza wafanyabiaahara wa ndani na Watanzania kushiriki katika sekta ya nishati, Serikali itaendelea kuhakikisha kanuni na taratibu zinazofaa zinawekwa ili kuwezesha ushirikishwaji katika mnyororo wa thamani wa maendeleo kwenye sekta ya nishati

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema wameendelea kutekeleza mipango mbalimbali waliojiwekea katika kuhakikisha umeme unapatikana wakati wote nchini.

Dkt. Biteko amesema zaidi ya kampuni 100 za nishati kutoka katika maeneo mbalimbali duniani zinashiriki katika kongamano hilo ambalo lilitanguliwa na mkutano wa viongozi wa nishati.

Matukio Katika Picha ziara ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kutembelea mradi wa JNHPP .

 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko leo Septemba 16, 2023, ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project ( JNHPP) ambao ujenzi wake umefikia asilimia 91. 72, huku bwana likiwa na ujazo wa mita 164.81 sawa na lita bilioni 14.66 sawa na asilimia 47.8.

Katika ziara hiyo ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Maharage Chande na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.







*Tanzania yaunga mkono Ajenda ya AU 2063- Dkt Biteko.*


*Na Grace Semfuko - MAELEZO na Dorina Makaya -Wizara ya Nishati.*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono Ajenda ya Maendeleo ya Mwaka 2063 iliyowekwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika- AU ambayo ina mikakati ya kufikia Afrika yenye ustawi na umoja.

Dkt. Biteko ameyasema hao leo Septemba 15, 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Husein Mwinyi kufungua Mkutano wa nne wa Kamati Maalum ya Kitaalam, kuhusu Sekta ya Uchukuzi, Miundombinu ya Kikanda ya Bara  la Afrika pamoja na Nishati ambapo ameongeza kuwa, jiografia  ya Bara hilo ni ya kimkakati na  inaturuhusu kuunganishwa na ulimwengu kwa njia ya anga, usafiri wa barabarani na majini na hivyo kuna kila sababu ya Afrika kuendelea kuwa katika umoja huo.

*“Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono ajenda ya mtangamano wa Afrika iliyowekwa na AU, ajenda ya 2063 inatupa Dira ya Afrika tunayoitaka ili kufikia Afrika yenye ustawi na umoja, utekelezaji wa mikakati ya ajenda hiyo ni nyenzo muhimu sana ya kutufanya tuyafikie malengo yetu hivyo majadiliano yenu ambayo yanaongozwa na kaulimbiu ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu ili kufikia malengo ya 2063 ni muhimu sana kwenye mkutano huu”* amesema Dkt. Biteko

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Khalid Salum amesema mkutano huo ni fursa nyingine ya kupokea taarifa kuhusu maendeleo yaliyopatikana tangu mkutano uliopita uliofanyika kwa njia ya mtandao mwezi juni mwaka 2021 ambapo kwa sasa, pamoja na mambo mengine, watajadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kufikia malengo ya Bara la Afrika.

*”Ninatambua kwamba uwepo wenu kwenye mkutano huu ni ishara yetu ya pamoja ya kuendeleza miundombinu na kupata suluhisho la changamoto za nishati na miundombinu Barani Afrika”* amesema Dkt. Khalid.

Kwa upande wake Kamishna wa Miundombinu kutoka katika Kamisheni ya Umoja wa Nchi za Afrika-AU Dkt. Amani Abou-Zeid amesema Afrika haina budi kuharakisha maendeleo ya miundombinu ili  kuleta ushindani na katika ushiriki wa watu wa Bara hilo katika soko la kimataifa la bidhaa.

*“Kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya Afrika ni jambo la kipaumbele, haijalishi kuwa miundombinu yetu ni mizuri kiasi gani, sote tunajua kuwa tunahitaji kuharakisha ujenzi wa miundombinu yetu ili kuwe na matarajio makubwa kwa watu wetu, hii ni kwa ajili ya kuleta ushindani katika ushiriki wetu kwenye soko la kimataifa”*  amesema Dkt Amani.

*Mwisho.*


MHE. MHAGAMA AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI UDIWANI RUVUMA

 
WANANCHI  wa Kata ya Mtyangimbole, Kijiji cha IKalangiro kilichopo Wilaya ya Songea Vijijini wametakiwa kutofanya makosa katika marudio ya uchaguzi mdogo wa  Udiwani katika Kata hiyo utakaofanyika Septemba 19 mwaka huu na kuombwa kumchagua mgombea anayetokana na Chama cha Mapinduzi, Twahibu Diwani Ngonyani.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Peramiho  Mhe. Jenista Mhagama wakati akizindua kampeni hizo  katika Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma ambapo alikutana na viongozi wa Chama pamoja wanachama wa CCM Kata.

Alisema kuwa, chama cha Mapinduzi kimewaletea mgombea sahihi ambaye atawatumikia wananchi na kushirikiana na Serikali  kutatua kero zao ili kuwaletea maendeleo kulingana na kasi ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Wananchi mnawajibu wa kuhakikisha mnachagua mgombea anayetoka na CCM katika uchaguzi huu wa marudio ili kukamilisha mafiga matatu na kunufaika na chama chenu chenye nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo," alisema Mhe. Jenista.

Aidha Mbunge huyo alisema, Ilani inayotekelezwa kwa sasa ni ya Chama cha Mapinduzi na kuwataka kumchagua Twahibu Diwani Ngonyani  ili aweze kuisimamia Ilani hiyo kwa vitendo akisema kuwa, jukumu la chama cha Mapinduzi ni kuleta maendeleo na kuwataka kukikopesha imani chama hicho kwa kumchagua mgombea wake nacho kitawalipa maendeleo.

“Serikali imejipanga kutatua  kero za maji na katika huduma za afya kuna mikakati ya ujenzi wa vituo vya afya kwa lengo la kuwapungiza adha wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma muhimu hali inayorudisha nyuma maendeleo,” Ameeleza Mhe. Jenista

Katika hatua nyingine Mbunge huyo aliwataka wakinamama kuhakikisha wanawahimiza vijana na kinababa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kumchagua mgombea anayetokana na CCM akieleza kuwa ni nia njema ya Serikali kuhakikisha inaboresha miundo mbinu ya barabara, upatikanaji wa mbolea kwa wakulima kwa bei nafuu ili kulima kilimo chenye tija.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Songea Vijijini Bw. Thomas Masolwa amewahimiza kumchagua Twahibu kwa ajili ya maendeleo yao ni siyo wagombea wengine kutokana na uzoefu wake ndani ya Chama hivyo atakuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.

Naye  Mgombea wa Udiwani katika Kata ya Mtyangimbole Bw. Twahibu Diwani Ngonyani  akinadi sera zake ameahidi kushirikiana na wananchi wa Kata hiyo pindi watakapomchagua  kwa  kumpa ushindi wa kishindo.





Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati akizindua Kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Mtyangimbole, Kijiji cha IKalangiro kilichopo Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

DKT. BITEKO AWASIHI WAFANYABIASHARA WA PETROL NA DIZELI KUWA WAAMINIFU.

 

Na Timotheo Mathayo, Dar es Salaam.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasihi Wafanyabiashara wa mafuta ya dizeli na Petroli nchini kuwa waaminifu wakati wakiendelea kutoa huduma kwa Watanzania.

Dkt. Biteko  ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa EWURA jijini Dar es Saalam Septemba 14, 2023 na kukukumbushia kuwa, pamoja na kuwa ni Wafanyabishara lakini pia wanatoa huduma kwa Wananchi.

‘’Naomba Wafanyabiashara wenye leseni za biashara ya mafuta nchini watambue kuwa wana wajibu wa kuhudumia watanzania ili wapate bidhaa hiyo, tunajua kuwa kiwango cha uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kimepungua lakini Serikali inaendelea kulifanyia kazi,” amesema Dkt. Biteko.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko amesema,  Serikali inafanya kazi kubwa ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa mafuta nchini inamalizika.

Dkt. Biteko ameitaka EWURA kuhakikisha inapitia mfumo mzima wa upangaji wa bei ya mafuta ili kuwezesha bei zinazopangwa zilingane na uhalisia wa maisha.

“Wazalishaji wa mafuta duniani wamepunguza uzalishaji lakini mahitaji ya mafuta yameongezeka kwa sababu ya shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa ikiwemo ununuzi wa magari na ujenzi wa viwanda vya kuzalisha malighafi mbalimbali,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo Serikali imeanza kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya  Gesi Asilia - CNG ili kuhamasisha wananchi kuanza kutumia magari yanayotumia mfumo wa Gesi Asilia ikiwemo magari ya Serikali.

Amefafanua kuwa faida zitakazopatika kama magari yaliyokuwa yakitumia mafuta yakianza kutumia mfumo wa uendeshaji unaotumia Gesi Asilia - CNG, gharama za uendeshaji wa magari hayo zitapungua na mafuta yaliyokuwa yakitumiwa na magari hayo yatatumika kuendesha mitambo iliyopo viwandani.  

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na watendaji wengine kutoka wizara ya Nishati na EWURA.





MAJALIWA : ONGEZENI USHIRIKI WA WAHANDISI WAZAWA KWENYE UJENZI MIRADI

 
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha wahandisi wazawa wanashiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali nchini.
 
Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Tanzania, unaolenga kupunguza ukosefu wa ajira kutoka 9% hadi 8% ifikapo 2025/26, Serikali inatarajia kutimiza azma yake ya kuhakikisha inazingatia ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya ujenzi ili kukuza ujuzi.
 
Ameyasema hayo leo (Alhamisi Septemba 14, 2023) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya siku wahandisi, katika ukumbi wa Mlimani city, Dar es Salaam.
 
“Wizara ya Ujenzi pamoja na bodi ya wahandisi inalifanyia kazi suala la ushiriki mdogo wa wazawa katika miradi ya maendeleo, hii ni changamoto ambayo mmeiibua, Serikali sasa imeliweka kwenye mpango wa kuhakikisha changamoto inafanyiwa kazi ili kuongeza idadi ya wazawa kushiriki katika kazi za ndani”
 
Amesema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha wahandisi wazawa wananufaika kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali “miradi hii ni fursa kwenu, natoa rai mjipange na kufanya juhudi za makusudi kila mmoja kwenye eneo lake ahakikishe kwa uzalendo alionao na mapenzi kwa nchi yake kuwa kinara katika sekta unayosimamia ili kulijenga taifa letu”
 
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi iandae mpango mahsusi wa kuwaendeleza wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa kwa wingi zaidi wanapohitimu masomo “Suala hili litekelezwe kwa ushirikiano na wadau wengine wa uhandisi”
 
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenye amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi katika sekta mbalimbali za kiuchumi kupitia uanzishaji wa viwanda, uendelezaji wa miundombinu ya kilimo, nishati, maji, uvuvi, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano
 
“Katika mwaka 2023/2024 Serikali imetenga miradi maalum ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa ajili ya wakandarasi wanawake, ambao zabuni zitashindanishwa kwa makandarasi wanawake tu”
 
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Mhandisi Menye David Manga Amesema kuwa bodi inatarajia kufanya mageuzi makubwa ya teknolojia ili kuhakikisha wahandisi waliosajiliwa na wenye sifa wanakuwepo wa kutosha kwa ajili miradi mbalimbali nchini ili kujenga dhana halisi ya ushirikishwaji wa wazawa ‘local content’ “Tutakuwa na mageuzi katika sheria na kanuni zetu ili kuongeza usajili wa wahandisi”


NAIBU WAZIRI KAPINGA AIHIMIZA TANESCO KUBORESHA UPATIKANAJI UMEME MTWARA NA LINDI

 
Naibu Waziri Kapinga amelihimiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania - TANESCO kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wa kutosha.

Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo leo tarehe 14/09/2023 wakati alipotembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia  cha Mtwara.

Kituo hicho kina mitambo 13 yenye uwezo wa kuzalisha umeme MW 30.4 lakini
kwa sasa kinazalisha MW 19 kutokana na mitambo mitatu kuwa katika Matengenezo na kinahudumia mikoa ya Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga ametembelea kituo hicho ili kuangalia halisi hali ya mitambo na uzalishaji wa umeme kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri Kapinga amemuelekeza  Meneja wa Kituo hicho cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia  cha Mtwara, kuhakikisha wanafanya jitihada za kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme mkoani humo ili kukidhi hamu ya wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi ya kupatiwa umeme wa kutosha.

Naibu Waziri Kapinga amesema, jukumu kubwa walilonalo  nikuhakikisha kuwa Watanzania wanapata Nishati ya Uhakika.

Amesema, katika uongozi wake, kwa kushirikiana na Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake atahakikisha, anamsadia ipasavyo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko kuhakikisha wanatimiza kiu ya Watanzania kupata Nishati ya Uhakika.

Naibu Waziri Kapinga ameongeza kuwa, ili azma hiyo itimie, wanahitaji kupatiwa ushirikiano kutoka kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kwa pamoja kutekeleza mipango iliyowekwa ya kuwapatia Watanzania Nishati ya Uhakika ikiwezekana kuzidi lengo lililowekwa na Serikali kufikia 2025.

Naibu Waziri Kapinga amesema, mafanikio yake kiuongozi kwa kiasi kikubwa yatategemea ushirikiano mzuri wa Watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kufanya kazi kwa bidii, maarifa, moyo wa kujituma na kwa ushirikiano.

Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia  cha Mtwara, Meneja wa Kituo hicho, Mha. Mtoba Kasika Biseko, ameahidi kuwa, watafanya kazi kwa moyo wa kujituma na watawapatia ushirikiano mzuri viongozi  katika kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, aliambatana na Kamishna wa Umeme wa Wizara ya Nishati, Mha. Innocent Luoga, Naibu Mkurugenzi, Usambazaji Umeme wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania - TANESCO Mha. Athanasius Nangali na Meneja TANESCO  Mkoa wa Mtwara Mha.


Tawakali Rwahila.


WADAU WA MALEZI YA WATOTO WAKUTANA KUBORESHA MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO

 
Wadau wanaoshughulika na malezi na makuzi ya watoto wametakiwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya Programu Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT -MMMAM) ili kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto wa Mkoa wa Dodoma

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu wakati wa ufunguzi kikao cha wadau hao kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo Septemba 14, 2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kujadili afua mbalimbali za namna ya kuboresha malezi na makuzi ya watoto.

"Mradi huu unagusa maeneo tofauti tofauti ikiwemo lishe ya Mtoto, malezi kuanzia ujauzito hadi miaka 8 na fursa za ujifunzaji wa malezi ya awali ya Mtoto. Dodoma ina takribani wadau 410 wanaoshirikiana na Serikali katika kufanikisha program hii, hivyo ni muhimu kushirikiana kwani bado hatujafanya vizuri kama Mkoa kwenye takwimu za lishe kwa watoto" Amesema Bw. Gugu

Aidha, ameongeza kwa kuwaasa kina mama na walezi kuzingatia nafundisho ya lishe yanayotolewa na wataalamu kuanzia kipindi cha ujauzito hadi malezi ya Mtoto.

" Kwa kipindi cha 2022/2023 jumla ya kina mama / walezi 191,662 kati ya 200,981 walio na watoto wenye umri wa miezi 0 - 23 walipewa unasihi juu ya ulishaji wa watoto uliofanywa na watoa huduma ya afya sawa na asilimia 104.60 hii ninaonyesha ni kwa namna gani unapomlinda mtoto kwa kumpa lishe bora, itasaidia katika makuzi yake"  Ameongeza Bw. Gugu.

Akizungumzia lengo kuu la kikao hicho, Mratibu wa Malezi na makuzi ya watoto Bi. Stella Matemu amesema,
" Lengo kuu la kikao hicho ni kuwatambua wadau pamoja na kujadili afua mbalimbali zinazopatikana kwenye mradi huu ulioazinduliwa rasmi mwaka 2021 kitaifa ambapo kwa Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa Septemba 2022 ukihusisha maeneo matano ambayo yanahusiana na malezi na makuzi ya Mtoto kuanzia miaka 0 - 8 nayo ni Elimu, afya, lishe , malezi na mwitikio." Bi. Matemu

Hata hivyo, mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Watoto na Makundi maalumu Bw. Joel Mwakapala amesema kuwa asilimia 90 ya ubongo wa mtoto unakua akiwa katika umri wa miaka 0 hadi 8 huku akielezea namna program hii inavyoleta matokeo chanya kwa jamii.

" Uwepo wa program hii umesaidia kuboreshwa kwa mazingira wezeshi ya kufanya uratibu wenye ufanisi na pia mifumo ya utoaji huduma Jumuishi za MMMAM na uthibiti ubora imeimarishwa" Amesema Bw. Mwakapala.

MWISHO