Na. Kadala Komba Dodoma
Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Mary
Chatanda Novemba 24,2023 umeendelea na ziara yake Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi.
Uongozi huo ukiwa katika ziara yake umegawanyika
katika timu mbalimbali ambapo Naibu Katibu Mkuu Ndg , Riziki Kingwande
amefanikiwa kutembelea Kata ya
Ibugule kijiji cha Mapanga
Kata Chibelela
Kijiji Isangha
Kata
ya Mtitaa na Kukagua mradi ya madarasa matano (5) ya shule ya msingi
Isangha Kukagua nyumba ya mtumishi two ni One Kukagua matundu 10 ya choo
Yenye Gharama za Tsh. 233,800,000/= Pamoja na kusikiliza kero za
wananchi .
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mtitaa
amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwalinda
kwani maadili yameporomoka hivyo amewasihii kundokana na desturi ya
kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .
"Wazazi
naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani
ndio viongozi wa leo na kesho yao hatuwezi kukaa kimya na kulifumbia
macho hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa
kukatishwa ndoto zao tumechoka kusikia mara mtoto amelaitiwa mara
kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande .
Sambamba
na hilo, Ndg .Kingwande Amewahimiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi
kutekeleza majukumu yao kwa nafasi zao kuanzia ngazi ya shina , matawi
kata kwa lengo la kuwaaminisha wananchi waone kazi vinazofanywa na
viongozi wa chama cha Mapinduzi, hivyo viongozi wenzangu tujitume katika
kazi ya kuwasaidia wananchi tufanye ziara pamoja na mafunzo kwa
viongozi hili kuwajengea uwezo.
MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA
0 Comments:
Post a Comment