Home »
» ASA YAPONGEZWA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO
ASA YAPONGEZWA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO
Na Mwandishi wetu- Tabora
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameupongeza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kukamilisha Awamu ya Kwanza ya Mradi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la mbegu Kilimi lililopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Mhe. Ummy ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika shamba la mbegu Kilimi linalotekelezwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kupitia Mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ambapo amesema Taasisi hiyo iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo imepiga hatua kwa utekelezaji wa vitendo kwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa na imara ya Umwagiliaji katika shamba hilo.
Amesema matarajio ya Serikali ni kuona uzalishaji wa mbegu unaongezeka kwa wananchi ili kupunguza uagizwaji wa mbegu kutoka Nchi jirani ambapo baadhi ya wakulima hushindwa kumudu gharama.
“Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha tufanya kilimo cha kisasa na kupata fedha za kuendeleza sekta hii muhimu lengo la ziara hii ni kuona Mradi unavyoendelea hivyo nampongeza Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe anafanya kazi kubwa sana akishirikiana na ASA. Pia nimefurahi kuona fedha inayokuja katika mradi inafanya kazi iliyokusudiwa kuongeza tija katika uzalishaji wa mbegu,”Alisema Mhe. Ummy.
Ameeleza kwamba Wizara ya Kilimo imejipambanua kwa kuweka miundombinu ya Umwagiliaji, kuhamasisha vijana kukipenda kilimo tofauti na awali kilichukuliwa kama adhabu.
“Tunawashauri watanzania waendelee kuiamini Serikali wakati tunafanya mapinduzi ya kilimo watumie fursa hii hasa waliopo katika maeneo haya na hata tutakapoanzisha vituo hivi katika maneno mengine basi wakulima watumie fursa hiyo kuboresha kilimo wajikwamue kiuchumi,”Ameeleza.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge amesema maelekezo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri yatafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu ili kukidhi mahitaji ya wakulima hapa Nchini huku akisema kuwa wataendelea kuweka mikakati ya kuimairisha usalama katika mashamba kuepuka uharibifu unaotokana na uingizwaji wa mifugo katika mashamba hayo.
“Awali kulikuwa na changamoto kubwa ya mifugo kuingia katika mashamba lakini tumejitajidi kutoa elimu kwa vijiji vilivyopo katika maeneo haya na tunaendelea kuongeza ulinzi kimsingi mifugo ina madhara makubwa kwa mashamba ya mbegu na uzalishaji wa chakula pale mifugo inapoleta magugu kupitia kinyesi, wanaharibu rutuba ya udongo, kuongezeka kwa magonjwa kwa mazao hali inayoongeza gharama za matunzo,” Alifafanua Dkt. Sophia.
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Nzega Bi. Winfrida Funto amemshukuru Mhe. Ummy kwa kufanya ziara katika Mkoa huo ambayo imetoa hamasa katika sekta ya kilimo hususan kilimo cha umwagiliaji ambacho hongeza tija kwa wakulima na kuondokana na kilimo cha mazoea.
Aidha mmoja wa wakazi katika Kijiji cha Bukamba Mpya Bi. Joyce Masanja ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuratibu Mradi wa AFDP ambao kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) imewasaidia wakulima kupata mbegu bora za asili kutokana na uwepo wa mashamba ya uzalishi wa mbegu na kupatikana kwa urahisi.
==MWISHO==
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akikagua mifumo ya maji inayosambaza maji katika shamba la mbegu Kilimi linalotekelezwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kupitia Mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) alipofanya ziara hiyo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Related Posts:
NAIBU WAZIRI MERYPRICA MAHUNDI AMETOA OYO KALI KWA WALE WANAOCHEPUSHA MAJI Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na wanan… Read More
RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA SENSA NA MUONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO HAYO JIJINI DODOMANa. Kadala Komba Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo … Read More
TANROADS YATUMIA SHILINGI TRILIONI 1.37 KUKAMILISHA MIRADI 14 KWA KIPINDI CHA SERIKALI AWAMU YA SITA.Na Moreen Rojas, Dodoma Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema imefanikiwa kukamilisha jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 katika kipindi cha awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania … Read More
KATAMBI AMEWATAKA VIJANA KUJITAMBUA NA KUTHUBUTUNa. Kadala Komba Dodoma Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, amewataka vijana kujitabua ,kuwa na uthubutu pamoja na kujiwekea malengo ,Amesema uwezi ku… Read More
WAZIRI SIMBACHAWENE, AMPONGEZA MAMA TUNU PINDANa Mwandishi wetu Kuimba kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuewa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa. Kauli hiyo imetolewa na W… Read More
0 Comments:
Post a Comment