Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Wanafunzi Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wametakiwa kutumia tafiti zao kwa manufaa ya jamii ili kuleta tija na matokeo chanya ya tafiti zao.
Hayo yamesemwa na Bwana. Moses Dulle Mkurugenzi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye amemwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo Mgeni rasmi katika kongamano la kitaaluma ambapo wanafunzi wamepewa tuzo mbalimbali kutokana na tafiti zao ili kuwapa motisha na wengine kuendelea kufanya tafiti hizo ambapo tukio hilo limefanyika ukumbi wa miyuji North jijini Dodoma.
Aidha ameongeza kuwa tafiti nyingi hazitangazwi kutokana na udhaifu kutoka kwa wahitaji na wazalishaji kwa kawaida jamii inabidi iwe na uhitaji wa tafiti fulani kwa ajili ya ubunifu na wakati mwingine inawezekana jamii yenyewe hawana uhitaji hivyo kuwapa ugumu watafiti kutumia tafiti zao lakini jamii inapaswa kuwa na muamko wa kufanya uwekezaji kwenye tafiti hizo.
"Maendeleo ni hatua na hayawezi kuja ghafla ni jukumu la wanafunzi na walimu kuweza kutangaza tafiti zao pamoja na waandishi wa habari kuuliza taasisi zinazofanya tafiti kujua namna wanavyofanya tafiti zao na kuzitangaza kwa wananchi lakini pia ni jukumu la jamii yote kwa ujumla wake kuhamasisha namna watu wanaweza kupata taarifa za utafiti" Amesisitiza Bwana Dulle
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof.Hozen Mayaya amesema chuo kinakuwa na wamewapongeza watu wao mbalimbali na kuwafikishikia umma kwamba wanajenga uwanja wa watu wao,hivyo pamoja na kwamba wanawaleta wanafunzi na kwa sasa hivi wanataaluma 79 ambao wanasoma katika maeneo mbalimbali kati yao 45 walikuwa wanasoma vyeo vya PHD ambao ni vyeo vya juu zaidi.
"Hii maana yake ni kwamba miaka michache ijayo chuo hiki kitakuwa kinatoa wasomi wenye elimu ya juu lakini kwa upande wa kuwapa tuzo wanafunzi ni kuwajengea hamu ambao wanaendelea kusoma ili kufanya vizuri zaidi na kuwa bora kwenye masomo yao na kujifunza kutoka kwa wingine" Amesisitiza Prof.Mayaya
Naye Dorcas Samson ambaye ni mhitimu wa chuo hicho amesema anashukuru kuwa miongoni mwa wahitimu kwani kupitia chuo hicho ameweza kuwa mjasiriamali na hivi sasa anajishughulisha na uongezaji wa thamani kwenye bidhaa za chakula anatengeneza unga wa lishe pamoja na soya ambapo ndoto yake kubwa ni kuwa mjasiriamali mkubwa kutokana na ujuzi alionao na kuajiri wengine.
"Kwa wanafunzi ambao hawajajiunga na chuo cha mipango nawashauri wajiunge na chuo hiki kwani mbali na masomo watafundishwa elimu ya ujasiriamali na kuweza kujiajiri wenyewe na kupunguza wimbi kubwa la kutegemea kuajiriwa na serikali ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati na nchi yetu kupunguziwa lawama kutoka kwa vijana lakini kwa upande wa serikali tunaomba ihakikishe inawasapoti wajasiriamali wadogo na wanaochipukia hasa hasa vijana" Ameongeza Tabitha Yusuph ambaye ni mhitimu na mjasiriamali.
Home »
» WANAFUNZI CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUTUMIA TAFITI ZAO KWA MANUFAA YA JAMII.
0 Comments:
Post a Comment