STORY
SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Serikali itaendelea kulinda kwa nguvu na gharama zote uhuru wa wananchi wa kutoa mawazo, imani na uchaguzi katika dini, hivyo itahakikisha kunakuwa na amani na utulivu ili uhuru huo wa kuabudu na kutoa mawazo uwepo muda wote.
Dkt.Biteko amesema hayo tarehe 19 Novemba, 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kumpongeza Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul Ruzoka na kumpokea rasmi Askofu Mkuu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa. Sherehe zilizofanyika katika Jimbo Kuu Kanisa Katoliki Tabora.
"Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan muda wote amekuwa akisisitiza haki kwa wananchi wote, na ili kuishi katika misingi ya utangamano haki lazima itawale. Rais anataka wananchi wasikilizwe; tunaweza kutofautiana katika maoni na mitazamo lakini kamwe tusivunje umoja wa kitaifa, tuwaunganishe watanzania na tupambane kuwaondoa wananchi katika umaskini na kuwaletea nafuu kubwa ya maisha." Amesema Dkt.Biteko
Dkt. Biteko amesema kuwa, Mheshimiwa Rais, msisitizo wake ni kupeleka maendeleo kwa wananchi wote bila kuangalia tofauti zao, ikiwemo maji, barabara, umeme, shule na pia lengo lake ni kuendelea kuwaunganisha wananchi ili kuleta umoja nchini.
Vilevile, Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt.Samia yupo tayari muda wote kushirikiana na taasisi za kidini nchini kuwaletea maendeleo wananchi.
Ameendelea kusema kuwa, Serikali itaendelea kuhubiri haki na maridhiano kama msingi wa amani wa nchi na pia itaendelea kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maendeleo kwani bila kazi hakuna Taifa.
Katika hatua nyingine, Dkt.Biteko amesema kuwa, Rais ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Askofu Mkuu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa kama ambavyo amekuwa akitoa ushirikiano kwa mtangulizi wake Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul R. Ruzoka.
Kwa upande wa Askofu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa na Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul R. Ruzoka wameshukuru kwa ushirikiano ambao Serikali imeendelea kuutoa kwao na wameahidi kutoa pia ushirikiano kwa Serikali.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Burian na Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamis Kigwangala. Pia walihudhuria Viongozi mbalimbali wa Madhehebu ya Dini kutoka ndani na nje ya nchi, na Waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Tabora.
Regards,
Henry KIlasila
Home »
» SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO
SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO
Related Posts:
MBUNGE WA JIMBO LA BAHI MHE. KENNETH NOLLO AMSHUKURU MHE.RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO BAHI Na. Kadala Komba Bahi Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo kwa wananchi wa wil… Read More
WAZIRI ULEGA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WA MIZANI KUPISHA UCHUNGUZI Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Balozi Aisha Amour, kuwasimamisha kazi wasimamizi wote wa Mizani waliokuwa zamu katika Mizani zilizopo katika barabara kuu ya T1 ina… Read More
MAAFISA ELIMU KATA, WALIMU WAKUU, WALIMU WA MAZINGIRA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA WAJENGEWA UWEZO JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI KATIKA MAZINGIRA YA SHULE BAHI Na. Kadala Komba Bahi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Za… Read More
MSAKO MKALI WALIOGUSHI VYETI VYA JKT Na. Angel Haule Dodoma Jeshi la kujenga taifa JKT kimetoa onyo kwa watu wanaogushi vyeti vya Jeshi Hilo vinavyoonesha wamepitia mafunzo ya JKT na kutumia kama sifa ya kuombea kazi sehemu mbalimba Nchini, wakati watu hao… Read More
RC SENYAMULE AIPA KONGOLE BAHI USIMAMIZI WA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI Ikiwa ni miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan kwenye kiti cha Urais na yamefanyika Maendeleo makubwa chanya Kupitia shamlashamla hizo za miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosema… Read More
0 Comments:
Post a Comment