Na. Mwandishi wetu Mpwawa
Kamati ya siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa Ndg. Pili Mbaga, imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Mpwapwa leo Novemba 13, 2023.
Akizungumza katika ziara hiyo Ndg.Mbaga ametoa pongezi kwa uongozi wa Serikali chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Sophia Kizigo kwa kuzingatia na kufuatilia hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Aidha, ametoa maagizo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji kuhakikisha wanafanya mikutano na ziara za kuwaeleza wananchi juu ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata Hivyo, Ndg.Mbaga amesisitiza Suala la utunzaji wa mazingira na kumpongeza Mkuu wa Wilaya kwa hatua mbalimbali anazoendelea kuzichukua katika kuhakikisha mazingira yanakua safi. Pia, amehimiza kutunzwa kwa miradi yote iliyo kamilika ili idumu kwa muda mrefu .
Vilevile amesisitiza suala la kuandika michango ya wananchi katika ripoti za utekelezaji wa Miradi.
Mbali na hayo, ametumia fursa hiyo kutoa taarifa kwa viongozi wa Serikali na Chama juu ya ujio wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) Ndg .Mary Chatanda Novemba 22,2023.
Kamati hiyo imefanikiwa kukagua Jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Wilaya hiyo, Mradi wa Daraja la Tambi, Shule Mpya ya Sekondari Kimaghai, Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Makutupa, hali ya Huduma ya utekelezaji wa miradi ya maji chini ya Wakala wa Usambazaji maji na usafi mazingira Vijijini (RUWASA) pamoja na umeme chini ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
0 Comments:
Post a Comment