Na. Mwandishi wetu Bahi
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dodoma Ndg.Jawadu Mohammed ametoa Rai kwa wasimamizi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuitunza ili wananchi wanufaike zaidi na maendeleo yanayoletwa na kiongozi wao Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kila Halmashauri ili idumu kwa muda mrefu.
Amesema kila mwanachi anapaswa kuwa mwangalifu Katika matumizi ya miradi hii kwani huo ndio uzalendo wa nchi kwa kila mtu kujali na kuzingatia miradi inayoletwa kwenye Halmashauri zao.
“Ni lazima kuzingatia na kuona umuhimu wa kila mradi unaoletwa na kutumia njia zote kuhakikisha kila huduma muhimu inafika kwenye kila Kata ikiwemo huduma ya maji, umeme, N.k.
“Halmashauri ni lazima kuendelea kufanya jitihada za kimaendeleo ili angalau baadhi ya maeneo yenye changamoto zozote za kijamii ziweze kutatuliwa kwa haraka" Amesema Ndugu Mohammed.
Vile vile, amesisitiza suala la upandaji miti kwenye mazingira yanayowazunguka ili kuondoa changamoto za majanga kama mafuriko na kusababisha ukame hivyo, kila mwananchi anajukumu la kupanda mti.
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Ndg. Maranyingi Matukuta amesema miradi inakuja kwenye Mkoa wetu ili tuweze kunufaika nayo hivyo miradi hiyo itunzwe vizuri kwani ni miradi yenye thamani nyingi na ni mizuri.
“Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Halmashauri inayofanya vizuri kwenye miradi hivo, Rais wetu mpendwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ana lengo zuri kwa wananchi wake wa Bahi, hivyo, isimamiwe kwa weledi na watumiaji waitunze” Amesisitiza Ndugu Matukuta
Pia ziara ya kamati hiyo iliweza kutembelea Mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Chiona ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 493, Mradi wa Maji Chali Makulu, Chali Isangha na Chali Igonga inayogharimu kiasi cha Bilioni 02 na kumalizia kwenye Ujenzi w Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Chali inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 544.
Home »
» UZALENDO WAHIMIZWA UTUNZAJI MIRADI BAHI
UZALENDO WAHIMIZWA UTUNZAJI MIRADI BAHI
Related Posts:
KAMATI YA UFUNDI YA SERIKALI MTANDAO YAFANYA KIKAO CHA KWANZA JIJINI DODOMA Kamati ya ufundi ya serikali mtandao imefanya kikao cha kwanza na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya utekelezaji wa majukumu yake, ili kuhakikisha jitihada za serikali mtandao zinaimarika na kuleta ti… Read More
MIKATABA YA UENDELEZAJI BANDARI ITAZINGATIA MASLAHI YA NCHI-MAJALIWA WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha kuwa mikataba ya utekelezaji wa makubaliano ya uendeshaji wa maeneo ya bandari nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya … Read More
MAPOKEZI YA RAIS SAMIA KILIMANJARO Mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan alipowasili Uwanja wa Ndege Kilimanjaro International Airport akiwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Kupiga vita Daw… Read More
DKT. KIKWETE AONGOZA MBIO ZA JKT MARATHON. Na Moreen Rojas,Dodoma. Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali katika Mbio za J… Read More
BISHOP:KOMBA AMEWATAKA WAKRISTO KUWA NA TABIA YA KUMSHUKURU MUNGU Na. Kadala Komba Dodoma Bishop: Sylvanus Komba wa kanisa la Mlima wa Bwana Assemblies of God Tanzania Dodoma Amewataka Wakristo kuwa na Tabia ya kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao .Bishop Komba Alisema Hayo Ju… Read More
0 Comments:
Post a Comment