Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ayaandikie Barua Mashirika ambayo hayajapeleka Wafanyakazi Kushiriki michezo ya SHIMUTTA Mwaka 2023 na kueleza sababu zakutoshiriki ili Serikali ione hatua zakuchukua.
Dk Biteko ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili.
Aidha ameongeza kuwa watumishi wa Umma wafanye kazi kwa Weledi na kutoa huduma Bora kwa watanzania pamoja na kuondoa hali ya watanzania kuona taasisi zao ni kero kwa Wananchi hivyo watatue kero hizo kwakutimiza wajibu wao.
"Tumekubaliana kufanya jambo fulani basi tulifanye, na kama tunaona halifai basi bora tuliache, kuliko tunakubaliana kufanya kitu halafu hatukifanyi; haiwezekani viongozi wote hapa wanalalamika, Katibu Mkuu analalamika, Naibu Waziri analalamika na mimi nilalamike?, hapana sijaumbwa hivyo, sioni sababu yoyote ya kutamkika au ya kuandikika, kwamba kuna mashiriki ya umma 248 na hapa yapo mashirika 57 tu; haiwezekani." Amesisitiza Dkt.Biteko
Aawali, Mwenyekiti wa Kamati ya SHIMMUTA, Roselyne Massama amemweleza Naibu Waziri Mkuu kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya muitikio mdogo wa Mashirika ya Umma kushiriki mashindano hayo jambo ambalo linazorotesha mashindano hayo.
Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzu amesisitiza michezo maofisini na serikali ya awamu ya sita inasisitiza michezo ambapo watumishi wawe na muendelezo wa michezo maeneo ya kazi ili kutokomeza magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Kwa upande wake Naibu Waziri,Sanaa na Michezo Hamisi Mwijuma amesema
serikali itoe tamko juu ya Mashirika ambayo hayawaruhusu Wafanyakazi kushiriki michezo kwani michezo ni njia nzurii ya kudumisha uhusiano na haswa kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kwani kwa kipindi hichi cha serikali ya awamu ya sita michezo imeenda kimataifa zaidi kupitia sekta ya michezo haswa mpira wa miguu haswa timu kongwe simba na yanga na Tanzania kujulikana kimataifa kupitia sekta hii.
Kwa upande wake Afisa uhifadhi mwandamizi Carlos Ernest Mbilo kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania(TAWA) amesema mashindano hayo yatadumisha uhusiano na taasisi mbalimbali na kwa upande wao mchezo mpira wa miguu wanafanya vizuri na upande wa netiboli wamepoteza mechi 1 na wanafanya vizuri kujituma lakini kikubwa ni nidhamu ili kuhakikisha wanapata vikombe vyote.
Naye Patrick Gandye Mwenyekiti wa michezo kutoka mfuko wa taifa wa jamii(NSSF) amesema michuano ilianza tangu jumamosi umuhimu mkubwa wa mashindano haya ni kujenga ukaribu na mashirika mengine ya serikali na taasisi ambazo hazijashiriki kama mgeni rasmi inabidi wafanye hima waweze kushiriki kwenye haya mashindano ikiwemo taasisi binafsi pamoja na mashirika ya serikali.
"Tuna mechi moja dhidi ya WCF tunaamini tutafuzu katika hatua inayofuata,tunaamini mwaka huu tutafanya vizuri licha ya kukutana na magwiji wa mchezo hivyo tunaamini tutachukua ubigwa,changamoto ni kwamba hatupati muda wa kutosha wa kufanya mazoezi,kama unavyojua kama mtumishi wa serikali muda ni mchache mno lakini haituzuii kutimiza majukumu yetu ya kimichezo" Amesisitiza Nora Mwidunda Meneja timu ya netiboli NSSF.
Naye Raymond Nyarufugo Mtumishi wa bandari ya Tanzania(TPA) amesema anawasihi taasisi zingine ziweze kuleta wanamichezo,kwa sababu michezo inasaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na magonjwa ya saratani lakini pia kuimarisha uhusiano katika taasisi za umma,kwenye taasisi yao kwa mwaka jana walikuwa washindi wa pili na walifanya vizuri.
Home »
» MASHIRIKA YASIYO TAKA KUSHIRIKI MICHEZO YACHUKULIWE HATUA KALII.
0 Comments:
Post a Comment