Wananchi wa kijiji cha Hurui kata ya Kikore Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wamesema ujenzi wa daraja la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 linalotarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba 2023 litatatua kero ya muda ya mrefu ya kutumia daraja la kamba kuvuka mto na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watoto kutofika shule Pia wakazi wa Kijiji hicho kushindwa kuuza mazao yao kutokana na kukosekana kwa miundombinu hiyo.
Hayo yamebainishwa Leo Novemba 22,2023 baada ya Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Timu iloyoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Joketi Mwegelo na Wataalamu wengine wa Mkoa na Wilaya hiyo kufika katika daraja hilo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Aidha Ndg. Mwegelo wakati akitembelea mradi wa Maji katika Kata ya Kisese amemtaka mkandarasi anaye tekeleza mradi huo kuanza ujenzi wa tanki ndani ya siku saba awe ameshaanza utekelezaji wa mradi huo ili kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi wa Kisese.Wito huo umetolewa baada ya kupita siku ishirini na moja ambazo mkandarasi alitakiwa awe eneo la mradi akiendelea na Ujenzi wa Mradi.
Hata hivyo Ndg. Mwegelo amesema licha ya Viongozi mbalimbali kuwachukulia hatua baadhi ya Viongozi ambao walikuwa wakitekeleza mradi huo lakini bado inaonekana kuendelea kusuasua jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa ukamilishaji wa Mradi huo.
Pia, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Kikore na Kisese kupeleka watoto shule na kuachana na tabia ya kugeuza watoto kufanya kazi za ndani .
Mkoa wa Dodoma umekuwa wa 17 kufikiwa na ziara ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Mary Chatanda na Viongozi wengine ambapo wanatarajia kupita katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ikiwa tayari wamesha kamilisha ziara yao Wilaya ya Kondoa kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) na maendeleo ya miundombinu mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa huo.
Home »
» DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA.
DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA.
Related Posts:
CANADA YATOA SHILINGI DOLA MILIONI 50 KWA AJILI YA MAENDELEO YA ELIMU NCHINI. Na Moreen Rojas,Dodoma.Waziri wa Elimu Prof.Adolph Mkenda amepokea dola za Canada milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini.Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi ya wizara jijini Dodoma ambapo asilimia 25 itatu… Read More
WANANCHI WAASWA KUACHA KUDANGANYA MAENEO YA MAKAZI. Na Moreen Rojas,Dodoma.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewaasa wananchi na wakazi wa Dodoma kuacha kudanganya maeneo ya makazi ili kuepusha migogoro ya ardhi.Mhe.Senyamule ameyasema hayo wakati akizindua … Read More
SERIKALI YA KANADA IMETOA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 240 KUBORESHA SEKTA YA AFYA TANZANIA. Na Moreen Rojas,DodomaWaziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameishukuru Serikalia ya Kanada kupitia Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan wake kwa kusaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tan… Read More
*AWESO AMUONDOA MKANDARASI MRADI WA MAJI KAZURAMIMBA-UVINZA-KIGOMAWaziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amekasirishwa na kitendo cha Mradi wa Maji Kazuramimba kuchukua muda mrefu bila kukamilika wakati wananchi wakiendelea kuteseka na ukosefu wa huduma hii muhimu.Awali cha… Read More
AFISA KILIMO GAIRO AMEWATAKA WAKULIMA NCHINI KUACHA KUFANYA KILIMO CHA MAZOEA Na. Kadala Komba Gairo Wakulima mkoani Morogoro wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea ili kuweza kuepuka hasara zinazojitokeza mara kwa mara badala yake wafuate ushauri unaotolewa na wa taalamu wa kilimo.Hayo yamebain… Read More
0 Comments:
Post a Comment