Subscribe Us

RUSHWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO LIMEKUWA TATIZO SUGU.

 

Rushwa kwenye miradi ya maendeleo limekuwa tatizo sugu,na wengine wamekuwa wakiliita kansa hivyo ni jukumu la kila mmoja hukakisha analeta usawa kwenye eneo hili.

Hayo yameelezwa na Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU).

Aidha ameongeza kuwa miradi iliyopo ni kwaajili ya kila mtanzania na kila mtu ana haki yakufanya kazi kwenye miradi hiyo lakini wasimamizi wa miradi wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya hivyo ni jukumu la watumishi wote wa sekta hii kuhakikisha wanakabiliana na watu hawa ambao wamekuwa miba kwenye jamii.

"Rushwa kwenye miradi ya maendeleo limekuwa tatizo sugu hivyo ni muhimu kushughulikia tatizo hili hasa kwa wale wasimamizi wa miradi wamekuwa wakitumia vyeo vyao vibaya kwa kuwanyanyasa wananchi  hivyo watumishi wote wa sekta hii ni jukumu lenu kusimamia maadili ya kazi na kutenda haki" Amesisitiza Mhe.Simbachawene

Aidha ameongeza kuwa hatua nyingi zinafanywa dhidi ya mapambano ya Rushwa na Serikali imeipa(TAKUKURU) ajira mpya zaidi ya 600 ili kupambana na rushwa pamoja na watumishi kujituma kwa weledi katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo suala la rushwa ni Agenda kubwa duniani.

Sanjari na hayo amesema kuwa kwa ulimwengu wa sasa katika kufanya kazi za kiuchunguzi watafakari nini cha kuboresha na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzipatia suluhu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)ambaye ni  Kamishna wa Polisi C.P Salum Rashid Hamduni  amesema mafanikio ya mwaka 2022 kupitia chaguzi mbalimbali bilioni 171 wameziokoa kupitia operesheni maana bila operesheni  fedha hizo zingeishia mikononi mwa watu.

Naye Neema Mwakaliele Naibu Mkurugenzi Mkuu (TAKUKURU) amesema mkutano huo unalenga kujenga utendaji kazi wa watumishi wa taasisi hiyo pamoja na kuongoza mapambano dhidi ya rushwa ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa muadilifu na kutenda haki bila upendeleo.

Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU una jumla ya wajumbe 61 ambapo kauli mbiu inasema"Kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu Tutimize wajibu wetu".


0 Comments:

Post a Comment