Subscribe Us

WANANCHI NTYUKA WAILALAMIKIA SERIKALI KULIPWA FIDIA YA BARABARA.

 Na. Modern Rojas Dodoma


Wananchi wa mtaa wa ntyuka na chimalaa wailalamikia serikali kuwachelewesha kuwalipa fidia ya mradi wa barabara.

Michael Emily mkazi wa eneo hilo amesema wananchi wanaodai ni takribani 172 na tangu mwaka 2022 mwezi wa 8 waliahidiwa kabla ujenzi haujaanza watalipwa mafao yao lakini mpaka sasa hawajalipwa,kamati ilienda TANROAD lakini hakuna matokeo chanya yoyote mpaka sasa na wakati waliambiwa wasubiri wiki moja,baada ya hapo wakasema wanaotaka kubomolewa kwa hiari wajitokeze sasa wanashangaa imekuaje tofauti.

"Leo wanasema wanataka watu wachache sasa watu wa chache kivipi?hivyo tunamuomba Waziri wa Ujenzi Mhe.Innocent Bashungwa aje aangalie dhulma hii na Rais wetu Mama Samia atusikie" Amesema Ndg.Emily

"Tumekuwa tukifuatilia viongozi wa Mkoa wanatupiga danadana tufanye nini?chuo cha mwalimu Nyerere wamechukua maeneo ya wananchi hawalipa watu wa eneo husika,serikali jamani ituangalie na kama mradi huu umeshindikana usitishwe" Ameongeza Bwana Edward Lamale.


Muhanga mwingine wa barabara Bi.Eva Daniel amesema aliambiwa saa 9 mtendaji atakuwa ameshasaini karatasi kwaajili ya kupata hela lakini matokeo yake anazungushwa tu na kudanganywa na ameambiwa kwa vile nyumba yake iko karibu na barabara aibomoe ahame na hawezi kuhama kwa sababu hana hata mia na kama serikali imewachoka iwaambie wahame na watahama mpaka chama maana kila siku wakikusanyika wanaambiwa meneja yuko kwenye kikao.


"Kwa upande wa mtendaji wa kata kiukweli hayupo na sisi na tunaona kabisa hatufai yuko kinyume na sisi kunawatu wana wito wanataka kufanya kazi na leo waandishi mmekuja hataki kuongea Luna nini kilichojificha?mtendaji wa kata ni tatizo kawapa barua baadhi ya wananchi kwa nini?tunataka mtendaji mwingine sababu huyu hawezi kutumikia wananchi maana ofisi ya kata mara nyingi imefugwa" Amesisitiza Bi.Eva


Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya ufuatiliaji Atnas Matonya amesema miradi mingi ya serikali wanashangaa kwa nini? haina chanzo cha kulipa fidia na watakopowalipa wawalipe na muda kwa sababu wako nje ya makubaliano na mojawapo ya miradi ambayo imekuwa hailipwi ni pamoja na mradi wa mwalimu nyerere takribani hekari 50 waliahidi kulipa watu pamoja na mradi wa udom ujenzi ng'ong'ona.

Baada ya wananchi kutoa kero zao Injinia Colman Gaston ambaye alikuja kwa niaba ya meneja wa TANROAD Mkoa wa Dodoma amewaambia wananchi kuhusu malipo ya mradi wa barabara unaendelea kwani wananchi walifanyiwa uthamini lakini vitabu bado vinafanyiwa kazi hivyo ameagizwa awaambie kwamba suala lao linafanyiwa kazi.


"Hivyo niwaombe wananchi suala la fidia linafanyiwa kazi na niwaombe mvute subira hivyo siku ya leo ntapeleka maombi kwamba wananchi wanataka kumsikiliza na kila mtu apate haki yake kutokana na taratibu zinavyotakiwa" Amesema Injinia Gaston


Naye Yona Andrew Diwani wa kata hiyo amesema uwepo wa mgogoro huo umetokana na ucheleweshwaji wa fidia ya barabara lakini ni takribani miezi 6 sasa ambapo imepelekea wananchi kuwa na taharuki kutokana na mvua kubwa zinazokuja na kuleta maafa zaidi na yeye kama kiongozi alichukua hatua ya kuunda kamati ndogo ili kushughulikia huu mgogoro.



0 Comments:

Post a Comment