Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam
Tanzania imeadhimisha Siku ya Yoga Duniani huku Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikisisitiza kuunga mkono sherehe za kitamaduni za mataifa mbalimbali duniani kwa sababu zinasaidia kujenga jamii ya kimataifa kuwa wamoja.
Hayo yamsemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Yoga Duniani ambayo huadhimishwa Juni 18, kila mwaka ambapo kwa Tanzania yamedhuiriwa na watu mbalimbali ambao wamefanya mazoezi ya Yoga kwa pamoja katika viwanja vya Gym Kana jijini Dar es salaam.
“Huu ni mwaka wa tisa sasa tangu Umoja wa Mataifa ulipotambua na kuupa mchezo wa Yoga siku maalum, Ubalozi wa India umeandaa sherehe hizi ambazo zimehuidhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India na Tanzania” amesema Bw. Yakubu
Mchezo wa Yoga asili yake ni India unaosaidia kuufanya mwili kuwa imara kwa kupata mazoezi kuanzia kichwani hadi miguuni hatua inayofanya mwili kuwa imara na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Miongoni mwa washiriki wa maadhimisho hayo ni Balozi wa India nchini Bw. Binaya Srikanta Pradhan na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini nchini Bw. Zlatan Milišić ambapo kwa Tanzania Siku ya Yoga imeadhimishwa katika mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na Kilimanjaro.
Home »
» TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA YOGA DUNIANI
TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA YOGA DUNIANI
Related Posts:
MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa August 26 2022MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa August 26 2022/Newspaper Front pages for August 26th 2022 … Read More
Waziri Simbachawene; tuenzi mambo mema yalioachwa na MremaNa Mwandishi Wetu Kilimanjaro. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameomba wananchi kuenzi mambo mema yaliyoachwa kama alama wakati wa uhai wa Mhe. Augustino Lyatonga Mrema. … Read More
SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKABILI MAAFA.Na Mwandishi wetu- Dodoma. Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika mapambano dhidi ya maafa ambayo hujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha athari. Hayo yameelezwa na Mkurug… Read More
NAIBU WAZIRI UMMY NA MUMEWE WAHESABIWANaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy nderiananga ,mumewe pamoja na wanafamilia wamekwisha hesabiwa . wewe je Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 25, 2022… Read More
0 Comments:
Post a Comment