Subscribe Us

KATAMBI AMEWATAKA WAKURUGENZI WAKUU WA MIFUKO YA PENSHENI KUHAKIKISHA MWANACHAMA ANALIPWA NDANI YA SIKU 60.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe.Patriobas Katambi amewataka Wakurugenzi wakuu wa Psssf na Nssf kuhakikisha kila mwanachama analipwa ndani ya siku 60 za kisheria kwa wanachama wote ambao nyaraka zao zimewasilishwa kwenye mfuko kwa ukamilifu.

Mhe.Katambi ameyasema hayo wakati akielezea changamoto wanazokutana nazo baadhi ya wanachama na wastaafu wanapofuatilia mafao kwenye mifuko ya pensheni katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma.

Aidha amewataka Wakurugenzi Wakuu wa mifuko hiyo kuhakikisha mameneja wote wa mikoa wanasikiliza na kutoa elimu kuhusu taarifa za wanachama(michango na mafao)pamoja na kuhakikisha hakuna malalamiko ya wanachama katika mikoa wanayoongoza.

"Wakurugenzi wakuu nataka kuhakikisha waajiri wote wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi,kila meneja wa mkoa awasilishe majina ya waajiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo"Amesisitiza Katambi

Aidha ameongeza kuwa Watumishi wa mifuko watapandishwa vyeo kwa kuzingatia utendaji na uwajibikaji katika kuwahudumia wateja(wanachama).

" Nafahamu Pssf na mamlaka za serikali za mitaa mko katika zoezi la kusaini mikataba ya kulipa madeni ya michango ya wanachama,hivyo ninaagiza mfuko na wahusika kukamilisha haraka zoezi hilo kabla ya tarehe 30 Juni 2023"

"Jana katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni nilitoa namba yangu ya simu, hadi kufikia leo asubuhi nimepokea jumbe za simu 28 ambapo zinahusu Nssf na Psssf 20 na tayari zimefanyiwa kazi na kukamilika" Amesema Katambi

Kupitia simu janja unaweza kujisajili na kwenye application ya mfuko na kuweza kuangalia michango yako kama inawasilishwa,kupata taarifa yako ya malipo ya pensheni na taarifa nyingine ya uanachama wako kwenye mfuko wa Psssf.



Sanjari na hayo Nssf taarifa kupitia simu janja mwanachama anaweza kujisajili kwenye mfuko application ya mfuko na kuweza kupata taarifa ya michango yako na kupata taarifa mbalimbali zinazomhusu mwanachama.

Aidha mifuko yote tayari ina dawati la malalamiko katika ofisi zake nchi nzima.


0 Comments:

Post a Comment