Na Eleuteri Mangi
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) katika sekta ya michezo nchini ili kuendelea kutoa ajira kwa watu wengi zaidi hatua inayosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Bw. Yakubu amesema katika kikao chake na Mtaalamu wa michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) Dkt. Shiraishi Tomoya Juni 01, 2023 jijini Dodoma.
“Uwepo wako hapa nchini utasaidia wananchi kuongeza hamasa ya michezo na watu wengi wakishiriki watakwepa magonjwa yasiyoambukiza, Rais yuko mstari wa mbele katika michezo, naamini uwepo wako hapa nchini utasaidia kukuza michezo na kuifanya kuwa maarufu na watu wengi kushiriki” amesema Bw. Yakubu.
Kwa upande wake Dkt. Shiraishi Tomoya amesema ana uzoefu wa nchi za Afrika Mashariki na anaiona michezo katika miaka 10 ijayo michezo inakuwa sehemu ya jamii ambapo watu wote watashiriki na kuimarisha afya zao.
Dkt. Shiraishi Tomoya ni mtaalamu na mshauri wa michezo na maendeleo atakuwepo nchini na kufanya kazi katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na atakuwa nchini kwa muda wa miaka mitatu kutoka 2023 hadi 2027.
Home »
» TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI
TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI
Related Posts:
MBUNGE WA JIMBO LA BAHI MHE. KENNETH NOLLO AMSHUKURU MHE.RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO BAHI Na. Kadala Komba Bahi Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo kwa wananchi wa wil… Read More
WAZIRI ULEGA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WA MIZANI KUPISHA UCHUNGUZI Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Balozi Aisha Amour, kuwasimamisha kazi wasimamizi wote wa Mizani waliokuwa zamu katika Mizani zilizopo katika barabara kuu ya T1 ina… Read More
ALIYENG'OA BENDERA YA CUF ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI Na Mwandishi Wetu,, Kondoa MTU mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa bendera na mabango ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa mapokezi ya Ma… Read More
MSAKO MKALI WALIOGUSHI VYETI VYA JKT Na. Angel Haule Dodoma Jeshi la kujenga taifa JKT kimetoa onyo kwa watu wanaogushi vyeti vya Jeshi Hilo vinavyoonesha wamepitia mafunzo ya JKT na kutumia kama sifa ya kuombea kazi sehemu mbalimba Nchini, wakati watu hao… Read More
WANACHAMA WAPYA 20 WA CUF WAKABIDHIWA KADI Na Mwandishi Wetu, Kondoa MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara) Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua wa… Read More
0 Comments:
Post a Comment